Viongozi Wakuu Wastaafu CCM nafsi ziwasute msiposimama kusema ukweli 2020

Viongozi Wakuu Wastaafu CCM nafsi ziwasute msiposimama kusema ukweli 2020

TumainiEl

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
7,280
Reaction score
14,342
Tunamshukuru Mungu ametupa pumzi sote tumevuka mwaka 2020. Naipongeza Serikali yangu na watanzania wote kwa amani na upendo baina yetu pamoja na misuko suko yote.

Ndugu wazee wastaafu ktk ngazi ya juu ya Taifa nawaandikia ujumbe huu wala siwafichi wala sipepesi macho ila nasimama kusema nawaomba mzungumze ktk Mahali pasiri kuwa baada ya kazi ngumu kujenga miundombinu yetu nyuma watu hawana furaha na hata pamoja na picha zote zinachezwa na idara nyeti ila mioyo ya watu ina machungu ambayo sio afya kwa chama, serikali na Taifa kwa ujumla.

Mlisikia lile tukio la mama kumchemsha mtoto wake na kula nyama yake nakumtengea mume wake? Ile haikuwa bahati mbaya ile ni meseji mbaya kwa taifa na ule ndio uhalisia wa hali ya maisha yetu. Chini ya chama cha mapinduzi

Ajira hakuna ila watoto wao wana ajira masikini ajiajiri. Mungu anaona haya tena anayaona sana wala msifanye hamuoni nakuwavika watu kilemba cha ukoka. We are a nation. Watu waende wapi je hiki ni chama ama tumebadilika kuwa mtoa roho. Watu wanafuraha za kimdomon mioyoni wana kilio. Nanyie mpo kimya as if vikao vya ndani sote tulikaa.

Watu wanapotea jamani hiki ni kitu gani kweli mpaka watu wanataja watu wanafanya hizi hujuma leaders mpo cool 😎 mnakula mema ya nchi kumbukeni damu hii itawalilia si support mtu anahujumu taifa ila na jiuliza je kukosoa ni kuhujumu taifa? Kama ndio futa vyama vya upinzani hizo ruzuku tukajenge majengo Dodoma. Tumuogope Mungu hili taifa halina watu wana kosoa kwa degrees yakuangusha serikali sema chuki inatutesa.

Ukabila na udini ndio ibada ya sanamu nani atasema ukweli kama sio ninyi mlio ndani ya system na mnao ijuwa kelele za kabila moja sasa sio siri wanajuwa chuki kubwa dhidi yao why na kwa nin sasa? Mpo kimya

Sisi sote niwatanzania na hatukuchaguwa chama kitutafune kwa siri siri nawaomba mseme ukweli mnaweza nikebehi au nisuta ila nimezaliwa tangu Nyerere ila sijaona aina ya maongozi haya ndani ya ccm. Mengi hayasemwi ila Tanzania haitobaki kama ilivyo sasa watu wajao watauliza na watasoma mambo mabaya wala sio mazuri.

Nimejiuliza maswali magumu sana walimwengu nisaidie hivi kweli ungemuuliza raia wakawaida nikiongozi gani hana mahusiano na watu wake sidhani kama kuna ambaye angemtaja Kigangwala ila najuwa kuna kiongozi wamkoa Dylan angetajwa mara elfu. Wazee semeni kweli ama hasira ya Mungu inaweza hata kukisambaratisha chama chetu.
happy new year
 
Huyu kibaraka wa mabeberu alikuwa mpiga dili sasa Rais wa Wanyonge jembe jemedari Dr JPM ameziba mirija jamaa anakuja analialia hapa, huyu atakuwa CDM bila shaka..
 
Hawa unaowaambia ni akina nani?? Hao old leaders kama kingereza chamgu kiko sawa, wao wameshirikia kumpa aidia ya mauwaji dhidi ya wapinzani na watanzania wote ka.panoja wameshalaaniwa kawatazame kwanza huko waliko wana chronic illnesses za nguvu sio kwa bahati mbaya ni laana. Ni vile hujui tu hata wao wana oesa lajini hawana furaha. Kibaya zaidi ni vile wanataka sote tusiwe na furaha.
 
Mungu atashuka lini ili tukariri tarehe na kuthibitisha?

Ikiwa unapinga serikali iliyopo, na unategemea Mungu ashuke ili kukamilisha upinzani wako, wewe ni sehemu ya tatizo.

Wewe si sehemu ya kumaliza tatizo.

Hakuna Mungu atakayeshuka kukumalizia matatizo yako.

Matatizo yako utayamaliza wewe mwenyewe, kwa hatua utakazochukua wewe mwenyewe.

Ukisubiri Mungu ashuke, utasubiri mpaka ufe, hatashuka.

Kwa sababu hayupo.

Kuna watu wamesubiri Yesu arudi kwa miaka zaidi ya 2000, na hajarudi.

Hatarudi.

Habari ya Mungu kushuka na Yesu kurudi ni ujinga tu watu waliojazwa.

Deus ex machina.

Uzembe

Acha uzembe.

Pigana na hali yako.

Usimsingizie kazi yako Mungu ambaye hayupo na hivyo hawezi kushuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwenye "saccos" na Mambo yanavyokwenda "domokrasia" na utawala wa "saccos" huku Mungu hawaoni.

Hadithi yako naifananisha na majambazi ambayo hufanya huhalifu na kujikinga kwa kujifanya ktk jamii kwamba wao ni watu wema lwa kutoa misaada kwa jamii .

Tunashukuru awamu hii imewashtukia na kujizuia kushobokea misaada michafu toka kwa majambazi ambao ndio wafadhili wakuu wa "Saccos"
 
TumainiEl katika yote ulipaswa uanze na kueleza mlichomfanya Ben Saanane, mipango yenu ya mauaji ya Lissu na uovu wote mlioshiriki. Ukiri na uombe msamaha kwa hayo mliyoyatenda au kuyasimamia.

Upinzani wala hauhitaji sauti yako kuusemea. Lia mbele za Mungu wako kutubu unyama huo uliochafua mikono yako.
 
TumainiEl katika yote ulipaswa uanze na kueleza mlichomfanya Ben Saanane, mipango yenu ya mauaji ya Lissu na uovu wote mlioshiriki. Ukiri na uombe msamaha kwa hayo mliyoyatenda au kuyasimamia.

Upinzani wala hauhitaji sauti yako kuusemea. Lia mbele za Mungu wako kutubu unyama huo uliochafua mikono yako.
Mikono yangu ni safi. Nimesema na ninasema tena nilitoa maoni kutokana na wakati tuliokuwepo kwa masilahi mapana ya wahusika na taifa pia.
 
Ili Toba yako ipate maana Tutajie kwanza Mahali alipo ama Uliposhiriki Kumpeleka ndugu yetu Ben Saanane.

Otherwise tutaamini kwamba Pengine ushirika wenu wa kihalifu dhidi ya binadamu wengine umeingiwa na mgogoro Kati yenu hivyo unalia lia baada ya mrija wako wa kihalifu kukatwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumainiel ulichokiandika kuhusu Ben na kikamtokea kimerekodiwa mpaka human rights watch hata Kama hukumtenda Ben kumbuka mdomo huumba.
 
Kiranga,
You should be out of your mind. Hata hivyo nakubaliana na wewe kuwa hatua tutakazo chukua ndizo zitamaliza matatizo yetu na si kusubiria mtu mwingine afanye kwa ajili yetu
 
Back
Top Bottom