Izato
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 5,441
- 11,669
Mkuu Tumaini, CCM imetoka ktk misingi yake ya asili, wazee ndani ya chama wanafumbia macho kwa yale yenye kupingana na misingi hiyo. Si kwamba hawayaoni ama kuyafurahia yanayoendelea sasa ndani ya chama chao.
Wamefungwa mikono kupitia historia zao wanyewe, kwa sababu walio wengi wana historia zisizotukuka na tena zenye kuhusiana na matendo ya kifisadi ndani ya chama na hata serikalini, kwa hiyo inakuwa ni vigumu kwao kutia neno lolote lile zaidi ya kuomba siku za utawala huu ziishe ili aje mwingine mwenye kuwahakikishia usalama wa maisha na mali zao. Wanajua wakijaribu tu kumgusa, ndipi siri za uovu wao zitawekwa bayana.
Sent using Jamii Forums mobile app