Viongozi wanaotukalisha barabarani ili misafara yao ipite hawajali wala kuheshimu muda wetu

Leo saa tatu asubuhi Morogoro eti Ndugai naye ana msafara wa kuzuia watu wasipite
 
Mkuu mpaka leo hujajua hatar ya kiongozi hasa namba moja kukaa foleni na magari binafsi bila sababu za msingi. Nazan umeamua utuzingue tu bana.
 
Misafara ya VIONGOZI wakubwa iko katika PROTOKALI.....wafanyeje sasa,wasipite barabarani na kuanza kutumia helikopta?!!!!!!😳😳😳
 
Kwani watu kugombea madaraka hata kwa mbinu chafu, unafikiri huwa kwa ajili ya kupiga mpunga tu?

Ni pamoja na hizo adabu za kuabudiwa.

Na tena kama hapo Dar, viongozi hawajui kabisa adha za msongamano ama foleni.

Hata kama anaenda kuangalia shamba lake jioni baada ya kazi, ng'ora litaunguruma na mtasubirishwa mpaka apite yeye kwanza.

Hizo ni itifaki kabisa, hawezi kulaumiwa kwa kusimamisha safari za raia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…