Viongozi wangu wa CCM inatosha sasa, TEC hawatatuelewa hadi tueleweke!

Viongozi wangu wa CCM inatosha sasa, TEC hawatatuelewa hadi tueleweke!

Lazima niseme. Nguvu kubwa inafanywa na viongozi wetu wa CCM Taifa ambao pia ni viongozi serikalini kupata 'uungwaji mkono' na Maaskofu wa Kanisa Katoliki. Ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Kuanzia Mwenyekiti/Rais hadi viongozi wengine waandamizi wamekuwa 'busy' na kutafuta kukubalika na wakatoliki.

Pamoja na ukweli kuwa ili ushindi upatikane na utulivu wa kiuongozi utamalaki lazima ukubalike na TEC, sasa imekuwa 'too much'. Makada wabobezi na waandamizi (hasa tulio wakatoliki) tunatumwa bila kusemwa kwa Kardinali, Maaskofu, Mapadre na wengineo ili kusaka kukubalika kwa viongozi wetu.

Amini nawaambia viongozi wangu wa kichama na kiserikali, TEC hawatashawishika kirahisi.

Hawatasahaulishwa msimamo na Tamko lao juu ya mkataba tata wa DP World. Hawatalaghaiwa kwa ahadi za kifedha; kupokelewa uwanjani au kupewa kanzu. TEC bado wanalo la bandari na wamejipanga kuusimamia msimamo wao.

Ili CCM tujisafishe mbele ya TEC, Tamko lao liheshimiwe. Kupigana vikumbo kujisogeza kwao hakutasaidia chochote. TEC imesheheni waelewa wa mambo zaidi ya wanasiasa wa zamani na wa sasa. Si wepesi kuyumbishwa kwa ahadi zisizo na kadi; michngo ya michongo na zawadi maridadi.

CCM tumeshaanza kampeni, wenzetu vipi?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
We mzee baada ya mkataba kusainiwa leo hii mbele ya hao TEC una lolote la kusema?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Sema yote lakini usipingane na ukweli aliouandika VUTA-NKUVUTE. Inaweza isiwe kwa uwazi unaoutaka wewe, lakini uhalisia ndo upo hivyo. Hivi unajuwa matamko mangapi yametoka kuhusu suala la bandari na DPW? Tamko la TEC ndo limeonekana kushika hatamu..!! Yaani kila mtu aliibuka toka alikokuwa..!! Hiyo pekee inatosha kukuambia kuwa TEC wapo very powerful.
TEC wapo pamoja na serikali.
 
TEC wapo pamoja na serikali.
Hapana, TEC hawapo pamoja na serikali, bali serikali ndo wapo pamoja na TEC, na sababu ni kwamba wamebadirisha vipengere vyote tata vya kwenye mkataba, ambavyo ni;

1. Mkataba maximum miaka 30, siyo kama mwanzo haukuwa na mwisho.

2. Watalipa kodi zote za Serikali kwa mujibu wa Sheria.

3. Wamewekewa performance key indicators na watakuwa accessed kila baada ya miaka 5.

4. Serikali itachukua 60% ya mapato au faida.

5. Serikali ina uwezo wa kuvunja mkataba muda wowote.Si kamahapo mwazo.

6. Mkataba huu sio wa gati zote za Bandari ya Dar es Salaam gati ambazo hazipo kwenye mkataba huu zinatafutiwa Mwekezaji mwingine (hata kuwa DP World).

7. Mkataba huu hauhusishi Bandari yoyote nyingine mwambaowa Bahari ya Hindi wala maziwa makuu.

#Dawa ya TEC iliingia….😂😂
 
TEC haifanani na akina Waitara, Katambi, Mollel, Kafulila au akina Mkumbo; ambao wakiwa na njaa wanapiga sana kelele, wakirushiwa mfupa, ni kushangilia na musifia kama wehu.

TEC haiwezi kunyamazishwa au kubadilishwa katija wanachokiamini kuwa siyo sawa, kwa kurushiwa mchango au kutembelewa maofisini kwao. Kitakachobadilisha msimamo wa TEC ni Serikali na viongozi kuachana na ule mkataba wa kishenzi wa DP.
👆
 
Ile dhana ya kwamba wenye nchi ni wananchi kwa taifa la Tanzania haipo...
 
"kama hujui kiarabu hutoi mzigo bandarini",,si ndio nyie hau hamkusema,,huu ndio muda wa nyoosha maelezo,,ni mpaka mseme😂
Usinijumlishe, kwangu mimi ilikuwa maboresho yaliyoorodheshwa. Huo upuuzi mwingine niwekee ushahidi wa mimi nilipoandika au niliposema hivyo..!! Acha kusingizia na kukwepa hoja
 
Back
Top Bottom