Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 473
- 1,682
Joseph Lazaro, beki wa zamani wa kushoto wa Coastal Union akiwa msaidizi wa marehemu Douglas Mhani enzi zile za marehemu Hamis Makene, benchi akiwa Mohamed Mwameja, kulia Saidi Kolongo, kushoto Douglas Mhani, nne Yassin Abuu Napili na sentahafu marehemu Idrisa Ngulungu, sita pale alikuwa akicheza Ally Maumba 'over the top', winga Kassim Mwajeki, winga kushoto Razark Yussuf 'Careca', nane Kassa Mussa, tisa huyu kocha wa Namungo Juma Mgunda na kumi Hussein Mwakuruzo.
Hii Coastal hadi nakufa sitokuja kuisahau, hata African Sports nakijua kikosi chake lakini kwa sababu naipenda Coastal ngoja nitoe ushauri wangu kwa viongozi.
Timu yetu jana imepambana sana, imepambana sana, maana Yanga walikuwa wanashambulia hadi nikawa naogopa, nikasema leo tunakufa 5, hadi half time tukaenda tukiwa nyuma kwa bao la offside.Ile ni offside sema mpira wetu ndio hivyo tena.
Lakini timu yetu ya Coastal kila siku kocha anayebadilika ni kocha mkuu tu, wanakuja makocha wageni wanaondoka, wanakuja makocha wazawa wanaondoka, anayebakia ni Joseph Lazaro.Kuna wakati Joseph Lazaro anaondolewa halafu anarudishwa.
Mimi nawaambia wenzangu wa Coastal, tubadilishe benchi la ufundi, Joseph Lazaro, beki wa zamani wa Yanga baada ya kuondoka Coastal Union yeye na Said Kolongo hana uwezo wa kufundisha timu kubwa kama Coastal.
Sana sana namuona kama mpiga majungu anawaharibia makocha wa kigeni ama wazawa waingie chaka aendelee kubakia yeye, kama ataendelea kuwa kocha timu yetu inarudi Championship.
Tuvunje benchi lote la ufundi, Joseph Lazaro akae pembeni, kwanini kila siku wanafukuzwa makocha anabakia yeye tu, kwani yeye ana nini.
Simba Nguvu Moja, Kesho iwe isiwe lazima tuvuke.