ushuhudaunaoishi
Member
- Dec 1, 2025
- 7
- 3
Tanzania ipo katika zama ambapo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni kiini cha mijadala ya Kisiasa, uwajibikaji na matumizi ya haki za kiraia.
Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuna ongezeko kubwa la watumiaji intaneti nchini, kufikia robo ya kwanza ya Mwaka 2025, ambapo 72% ya Watanzania wanapata huduma ya intaneti, ikiwa ni hatua muhimu katika safari ya kidijitali.
Takwimu hizo zinaeleza Watumiaji wameongezeka kutoka Milioni 29 Mwaka 2020 hadi Milioni 54.1 kufikia robo ya nne ya Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Zaidi ya muongo mmoja, vijana wamekuwa mstari wa mbele kutumia Mitandao ya Kijamii kuhamasisha mijadala ya kisiasa, kupaza sauti za wananchi na kusukuma uwazi katika utendaji wa Serikali.
Hata hivyo, matukio ya Oktoba 29, 2025 (wakati wa Uchaguzi Mkuu) pamoja na kuzimwa kwa Mtandao (Intaneti) kwa siku tano yamefungua mjadala mpana kuhusu nafasi ya TEHAMA katika ustawi wa demokrasia ya taifa.
Kizazi hiki, ambacho zaidi ya 60% ya Watanzania ni vijana (kwa mujibu wa Takwimu za Sensa za hivi karibuni, Mitandao ya Kijamii imekuwa si sehemu ya burudani tu, bali jukwaa la elimu ya uraia, uchambuzi wa sera na ushiriki wa kisiasa.
WATUMIAJI WA INTANETI WANAONGEZEKA
Ripoti nyingine zinaonyesha kuwa mwanzoni mwa Mwaka 2025 kulikuwepo na watumiaji Milioni 20.2 (29.1% ya idadi ya watu), huku Milioni 6.75 wakiwa na utambulisho wa Mitandao ya Kijamii (social media identities), ambao ni 9.7% ya Watanzania.
UCHAGUZI MKUU WA 2025
Nguvu ya Wanamtandao ilichochea mijadala ya Kisiasa nchini Tanzania, baadhi ya watu waliotumia mitandao na kuwa na nguvu ya ushawishi ni Maria Sarungi, Mange Kimambi, Humphrey Polepole, Malisa na Roma Mkatoliki.
Nchi kama Nepal, Madagascar, Morocco na nyingine nyingi kuna mabadiliko ama ya kiuongozi au kiutendaji yalitokea kutokana na Vijana kutumia nguvu ya Intaneti kupambana na Watawala ambao walionekana kutowajibika inavyotakiwa.
Kilichofuata ni Vijana wengi kuingia barabarani kuandamana wakiwa na madai mbalimbali ya kupinga Serikali, hali ambayo ilisababisha wengi wao kuuawa, kujeruhiwa na wengine kukamatwa na kutuhumiwa makosa mbalimbali.
Hata baada ya kutangazwa kushinda Urais kisha kuzungumza na Dunia, Rais Samia Suluhu Hassan alikiri matukio ya vurugu za Uchaguzi huo yameathiri taswira ya nchi kimataifa, ikiwemo uwezekano wa Nchi kuwa hatarini kupata changamoto ya kukopa.
Hiyo inathibitisha kuwa Mitandao ya Kijamii ina nguvu kubwa katika ushawishi wa kufanyika kwa maamuzi au mabadiliko.
VIONGOZI WAACHE KUONGOZA KIMAZOEA
Viongozi wa mamlaka mbalimbali hasa za Serikali wanaoongoza Kizazi cha Kidigitali wanatakiwa kutambua namna ya kuishi na kuongoza kulingana na zama, ile tabia ya kuficha uwazi, haki za kiraia, uwajibikaji wa viongozi n.k vinaenda kuwa moja ya rungu litakalotumiwa na Vijana au raia kuwapiga nalo Viongozi au Serikali zao.
KUZIMA MTANDAO ILIKUWA NA FAIDA NA HASARA
Wakati Mtandao ulipozimwa Tanzania wakati wa vurugu za uchaguzo huo ilikuwa ni kama "giza la kidigitali", inawezekana ilisaidia Serikali kudhibiti vurugu lakini inawezekana iliongeza hasira kwa raia wengi kuhisi wamewekwa kwenye shimo lenye kiza wakati mchakato wa Uchaguzi ukiendelea.
Kuonesha kuzima Mtandao hakumaanishi watu watafungwa midomo kutoeleza hisia zao, Vyombo vya Habari vya Kimataifa vikiwemo CNN, Al Jazeerah na BBC viliendelea kuripoti matukio kupitia video na picha zilizokusanywa na raia mbalimbali na nyingine kwa njia ya Satellite.
Mtazamo wa Wataalam wa Elimu na Usalama wa Kimtandao Prof. Razack Lokina kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ni kwamba Vijana wanapaswa kuelekezwa kutumia TEHAMA kwa usalama, kutambua Sheria za Makosa ya Kimtandao na kuepuka uchochezi.
Anasema Mitandao ya Kijamii inaleta mabadiliko ambayo hayataweza kurudishwa nyuma kwa kuamsha kizazi cha vijana waliotambua kuwa sauti yao ina nguvu na kuonya kuwa thamani ya teknolojia ni kutumia kwa manufaa ya fursa.
Amefafanua kuwa UDOM imezalisha wataalamu wengi wa TEHAMA, lakini jambo muhimu zaidi ni wanalozingatia ni kuwakumbusha wataalam hao usalama wa mifumo na matumizi salama ya mitandao.
Anasema “TEHAMA ni fursa ya ajira na ubunifu, si chombo cha kueneza chuki na vurugu.”
Naye, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko UDOM, Rose Joseph, ametolea mfano halisi wa athari za matumizi mabaya ya mifumo ya kidigitali kwa kuwakumbusha umma tukio la Wanafunzi 121 kufutiwa matokeo baada ya kubainika walihujumu mfumo wa mitihani chuoni hapo.
Hoja yake inaonyesha kuwa uhalifu wa kimtandao ni hatari, na kilichotokea katika vurugu za Oktoba 29, 2025 kinafanana na mtindo huo kwamba matendo machache ya uchochezi mtandaoni yakasababisha hasara, vifo na kukamatwa kwa mamia ya vijana.
Baada ya matukio ya vurugu baada ya Uchaguzi, pia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ilitangaza kuanza uchunguzi lengo likiwa kufanya uchunguzi huo ni kuishauri Serikali ili kuweza kudhibiti matukio kama hayo katika chaguzi zijazo.
Upande wa Jeshi la Polisi kupitia taarifa yao ya Novemba 21, 2025 na Msemaji wake, David Misime lilisema linaendelea na uchunguzi kuhusu matukio ya vurugu na kutoa wito Wananchi kutumia mitandao ya Kijamii kwa njia salama.
KIJANA AFUNGUKA: SERIKALI IREJEE NJIA KUU
Mtumiaji wa Mtandao Atanas George anasema "Lazima tuukubali ukweli kuwa tulipuuza mno juhudi za kulinda amani kupitia njia ya haki, sasa matukio ya Oktoba 29, 2025 yanatukumbusha na kutulazimisha kuwa turejee njia kuu, tuzungumze na tukubaliane hakuna Mtu mwenye haki kuliko mwingine.”
Anaongeza kusema “Kila mtu iwe kiongozi au rai awa kawaida tuna haki sawa, viongozi watimize wajibu wao, watekeleze kile ambacho wamepewa mamlaka ya kukifanya na wasitumie nafasi hiyo kukandamiza wale ambao hawana.”
Naomi, Mwanafunzi wa moja ya Chuo Kikuu kilichopo Dodoma anasema TEHAMA inavyoendelea kukua, ndivyo siasa za Tanzania zitakavyoendelea kubadilika zikiwa wazi zaidi, zenye ushindani zaidi, na zinazoendeshwa na Wananchi, siyo mifumo.
Anasema "Hii ndiyo nguvu ya Mitandao katika Tanzania mpya, nguvu ya kijana mmoja anayeshika simu yake, lakini anatikisa Taifa zima kwa kudai haki na uwajibikaji."
HIVYO…
Serikali, Watawala, Jamii wote watambue kuwa kizazi cha sasa ambacho asilimia kubwa ni Vijana kinahitaji kuona utekelezaji wa ahadi kwa vitendo na matendo hayo yawe na faida kwao na Jamii kwa jumla.
Kila kinachotokea Duniani wanaona na inawezekana wanajua kuliko hata wale waliopo madarakani, hivyo kuwafanyia porojo bila kuwajibika ni sawa na kukaribisha vita kila siku na kutengeneza mazingira ya kukaribisha machafuko kwa kuwa hawawezi kukubali