Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 761
- 6,985
Taifa limepita wakati mgumu sana wa maneno yasiyo na ukweli ndani yake "minong'ono".
Wakati hii minong'ono inaendelea nilitegemea na ninategemea Wataalamu wetu wa intelligence walijielekeza zaidi malangoni pa wateule kusikia misimamo na maoni yao kuhusu mjadala uliokuwa unaendelea mitandaoni. Bila biasness walirekodi walichokisikia na leo wanaweza wakaelewa nani mwema na Nani si mwema ndani mwao na nje ya kizazi chao.
Kama waliifanya kazi yao vizuri natumaini niwakati wa kuhitimisha kwa kuwasilisha kwa pilato taarifa hiyo kwa ajili ya maamuzi kulinda Taifa letu.
Hii njia ilifanikiwa Zanzibar kwenye vijiwe vya kahawa pale Karume alipowasisitiza wanaume kutokaa ndani jioni na wake zao Bali wakae vijiweni wawasikie wananchi wanasema nini.
Mwalimu nyerere wakati wa maandamano ya wanafunzi kupinga ongezeko la mishahara na posho za wabunge hakutuma watu wa system kwenda kutuliza ghasia, aliwatuma wakasikilize na kukusanya mabango yote wampelekee na kwa mabango Yale alitambua hoja na agenda ya maandamano yaliyoishia manzese.
Tusiwazibe midomo wanaosema, tusiwanyamazishe, ila tuwaweke pembeni kidogo wasubiri kiongozi watakayeendana naye kufanya kazi. Watu wanaokupinga gizani si watu wema hata kidogo, tunataka Taifa la watu wakupinga adharani ili waweze kusimamia wanachokipinga kiwanufaishe na wengine. Usitake mshahara kwa unafiki huku moyoni ukiwa unadonge, system wawekeni pembeni wakashirikiane na waliowengi wanaolia kuhusu ugumu wa maisha na umuhimu wa kurekebisha mifumo. Wakiendelea kupigwa na AC wanamwaribia baba na sisi pia wanyonge wanatuaribia.
MATEMBEZINI KYERWA NA KICHANE CHA IBANANAAAA