Mkuu, hivi umechanua kama uyoga ukitokea wapi?
Hii ni mara ya pili nakusoma humu kwa siku mbili hizi, na kila mara nikikusoma nashawishika kukuweka kwenye kundi maalum.
Bila shaka wewe ni mtu wa makamo, maanake unayachambua hata yale ya Mwalimu na Karume.
Sasa nigeukie baadhi ya uliyoandika:
1. Unaandika kwamba "taifa limepita wakati mgumu sana wa maneno yasiyo na ukweli ndani yake, 'minong'ono'"
Hili linashangaza. Taifa litapitia wakati mgumu vipi kwa maneno yasiyo na ukweli wowote, tena ni minong'ono tu?
Kwa nini mhusika aruhusu hali hii, na kumbe anaweza kuimaliza kirahisi sana, kwa kujitokeza tu kwa sekunde mbili au tatu hivi, akionekana akichapa kazi kwa bidii zake zote?
Hata kama yeye mwenyewe hataki, kwani hawezi kutuma tu wasaidizi wake na ujumbe mahususi unaoeleweka bila ya tatizo? Memo tu, toka kwa yule kijana wake Msigwa, si ingemaliza hiyo hali ya minong'ono inayolifanya taifa kukosa raha?
2. Hili nalo unawatupia lawama hao wanaohoji, ikiwemo na hao vigogo, sijui wewe umewasikia wapi wakiteta nyuma ya mkuu wao!
Wakati hii minong'ono inaendelea nilitegemea na ninategemea Wataalamu wetu wa intelligence walijielekeza zaidi malangoni pa wateule kusikia misimamo na maoni yao kuhusu mjadala uliokuwa unaendelea mitandaoni. Bila biasness walirekodi walichokisikia na leo wanaweza wakaelewa nani mwema na Nani si mwema ndani mwao na nje ya kizazi chao.
Wewe ungekuwa na nafasi ya uongozi ungepata taabu sana.
Na nadhani ndiyo sababu hata huyo unayemhimiza awachukulie hatua hao wanaomsemea mgongoni kwake, naye anapata taabu sana.
Mara hii 'stori' ya akina Makamba sr/jr; Kinana, na wengine umekwishaisahau? Mbona utabia zako zinafanana sana na huyu mtu wako, mnao undugu? Aaaah, ni "Mzila nkende", au siyo!
Huwezi kuwa unafuatilia watu hivyo na mabo yasio ya msingi.
Viongozi wanaofanya hivyo wako 'insecure' sana. Hawajiamini. Na hakika huyu naye hajiamini, ndio maana anatumia nguvu na vitisho vingi kwa kila jambo, badala ya kushawishi.
3. Umetumia mfano wa Mwalimu Nyerere na maandamano ya wanafunzi...
Huo ulikuwa ni uongozi uliojiamini. Leo hii maandamano hayo pengine pangekuwepo na maiti na walipata vilema vya kudumu.
Kwa sababu hiyo njia ya uoga ndiyo wanayoifahamu. Hawajui lingine, bali vitisho. Hakuna vishawishi vya kueleza watu wakaelewa.
4. "Watu wa kupinga hadharani" hamuwapendi, ndiyo sababu vyama vya siasa vya upinzani mmefanya kila linalowezekana, ikiwa ni pamoja na kuwaondoa Bungeni.
Watu wanapokosa njia zilizo wazi kuwasilisha yanayowasumbua mioyoni, njia pekee ni hiyo ya minong'ono ya pembeni.
Wewe mwenyewe unajua wazi, hakuna mtu yeyote ndani ya chama cha CCM au serikalini anayeweza kusema kitu asichokipenda Magufuli, tena mbele yake?
Hapa umeonyesha unafiki uliowazi.
Ngoja nikuache, nisije nikaandika gazeti hapa.