Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Tumeendelea kuwa na viongozi wengi ambao wao wakiona unakinzana na maoni au maslahi Yao wapo tayari kutumia mbinu zozote aidha wakuondoe au wakufanye unyamaze. Wao kwao siyo Kila uhai ni wa thamani, uhai kwao ni wa watoto wake, mke au Mme, wazazi na ndugu damu.
Hawa watu wanaongezeka Kwa Kasi na wanaonekana Kwa matendo. Wanaishi na kutamani watu wote waishi, wakisikia flani kapigwa utasikia chama Gani, flani katekwa utasikia chama Gani, wakisikia flani kawekwa mahabusu kinyume cha sheria swali lao ni chama Gani. Kama aliyefanyiwa hivyo siyo wa chama chake utasikia hayanihusu kila mmoja ashinde mechi zake.
Akitoka hapo anaingia msikitini au kanisani na kutoa neno au salamu akiomba amani, upendo na mshikamano. Hawa ndio binadamu wanaoendelea kupewa madaraka. Kiongozi anafikia hatua anasema chama kwanza mengine baadaye, au anasema yeyote atakayegusa maslahi ya chama changu ataondoka yeye......na watu wanapiga makofi.
Unajua tunaelekea wapi? Tunaelekea kurithisha watoto wetu hizi roho za kuthamini madaraka na chama kuliko watu. Tunaelekea kufanya ubaya unaofanywa Kwa asiye wa mrengo wetu uwe halali na anaofanyiwa wa mrengo wetu uwe hatia.
Tunapoelekea 2022 viongozi wa Dini wakiendelea kumtukuza mwandamu kuliko Mungu, wakishindwa kukemea badala yake wakasifia, wakishindwa kukataa wadhalimu kupewa nafasi kwenye nyumba za ibada tutaongeza wahalifu na hata hizo Dini hazitakiwepo Tena.
Niwaombe viongozi wa Dini mridhike na kile alichowapa Mwenyenzi Mungu na mjipe moyo mkuu wakusimamia ukweli na kukemea maovu pasipo na hofu ya kudhuriwa na wanadamu ambao ajuaye kesho Yao ni Mungu.