Viongozi wenye tamaa wanavuna na kuiba Pesa nyingi ili waweze kununua Urais 2025

Viongozi wenye tamaa wanavuna na kuiba Pesa nyingi ili waweze kununua Urais 2025

badison

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2015
Posts
1,450
Reaction score
2,761
Sijawahi kuona utawala wa watu wenye tamaa ya fedha kama huu wa awamu ya sita Yani Bora hata na ile awamu ya 4. Namba sita ni namba mbaya sana kiutawala ni namba isiyo na faida yoyote. Viongozi hawa wenye tamaa wanavuna pesa ili waweze kununua Urais mwaka 2025.

Takukuru, jeshi la polisi, na usalama wa taifa wote wapo kimya na taarifa wanazo. Watu wanahamisha mamilioni ya Dola na kuyaweka kwenye mabenki mataifa ya nje ili waweze kununua Uraisi. Wizara nyeti ya nishati na wizara ya fedha zinauwa uchumi wa nchi kwa makusudi.

Nchi inaongozwa na deep state kwa sasa. Hamna tena namba Moja. Niwaombe tuu ndugu zangu watanzania tuendelee kuwa watulivu na tuendelee kuwasusia hawa wezi.

CCM ni chama kinachokufa na watanzania tukisusie hiki chama cha wachawi na mashetani mwaka ujao wa uchaguzi 2025 ni witiri. Na kama mnavyojua witiri sio namba nzuri kwa ccm acha wazidi kujiharibia kwani Hicho chama tayari kimenajisi na kimevunja tunu ya jamuhuri (rejea maana ya nembo ya Bibi na bwana) kina laana tayari.

Uchaguzi wa mwaka wenye namba shufwa ni rahisi kwa kwa ccm kushinda lakini uchaguzi ujao ni namba witiri. Tutawadhalilisha. Leteni na tozo ya pumzi hii nchi ni mali yenu Sisi wananchi ni wapangaji tuu kwahiyo endeleeni kututoza. Kwani mnachukua pesa alafu hakuna cha mana mnachofanya.

Nb: Jeshi la polisi halipo tena ccm kwani ata hao Askari mishahara yao inapitia benki na wanakatwa double taxation kama kawaida.
 
Back
Top Bottom