Viongozi wetu kuwa na ndimi mbili si sawa, ni ishara ya kukosa uelekeo na msimamo

Viongozi wetu kuwa na ndimi mbili si sawa, ni ishara ya kukosa uelekeo na msimamo

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Hellow!

Mlituambia kuwa Nchi itaendelea kukopa kwa maendeleo ya taifa,

Mkaemdelea kusema, tunakopa kwa sababu tunakopesheka.

Akaibuka spika wa bunge na kuonya ukopaji wa spidi kuwa una madhara, akanangwa na kusemwa vilivyo na kupewa mipasho na kuambiwa tupishe.

Leo kiongozi yule yule anarudi kutwambia mikopo SI mizuri ina mashart mabaya, tuanzie kujitegemea wenyewe, sasa Yule Mgogo kosa lake ni kuwa ni kuwa na maono au Nini?

Ndimi mbili zinafaa kwa nyoka pekee, kwa viongozi hazifai.

ANGALIZO: Sasa kiongozi wa namna hii asiye na msimamo, anataka kuomba ridhaa Tena kutuongoza Ili iwe Nini?

TUJISAHIHISHE!

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿
 
Back
Top Bottom