agapito
JF-Expert Member
- Jan 29, 2014
- 252
- 258
Kikao cha usuluhishi wa mgogoro wa Kongo kimefanyika leo jijini Dar es salaam. Si nia ya uzi huu kujadili maamuzi ya kikao hicho, bali kuangalia faida zitokanazo na kikao hicho. Kama nchi lazima tuangalie faida tunazozipata na hasara zake! Kama sikosei vikao vyote vya usuluhishi wa Burundi kuanzia alipoanza mwalimu Nyerere mpaka alipokuja kupokea kijiti mzee Mandela vilifanyika Arusha. Hii ilifanya jiji la Arusha kujitangaza zaidi na kuonekana kweli ni kitovu cha amani Afrika,leo hali imekuwa tofauti! Vikao vyote ni Dar hali inayosababisha vurugu kubwa na foleni zisizo za lazima katika barabara za jiji,kifupi shughuli zote za jiji zimesimama. Hebu viongozi wetu wafikiri nje ya box sasa ili vikao kama hivi vifanyike Arusha ambapo hakuna mishemishe kama Dar na pia kuzidi kuliinua jina la Geneva ya Africa.