Elungata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 40,205
- 33,287
naona jamaa wameanza kampeni ya kusafisha wezi hasa waliopewa pesa.
sasa ndo tutajua kati ya ushabiki na common sense kipi kina matter
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
naona jamaa wameanza kampeni ya kusafisha wezi hasa waliopewa pesa.
Mchungaji Msigwa aliposema kuhusu akili ndogo kuongoza akili kubwa, alisema jambo la maana sana.sasa ndo tutajua kati ya ushabiki na common sense kipi kina matter
Kwahiyo mpaka majaji kutoka marekani wale wazungu nao wamepewa hongo?Hivi mlitegemea washindwe?? Wakati mpaka majaji wamepewa mgao...eti mchango wa harusi,...haya ni matusi kwa nchi..nani anayeweza mpa rafikiye mchango wa mil 400 kwa ajili ya harus??
Mpaka sasa prof wa anga kashikwa na kigugumizi kutoa tamko..chea bil 5 aliyopewa mke wa kigogo magomeni....
kama majaji wenyewe wamekula mgao wa pesa za escrow unategemea ninihadi marekani?,kuna watu wataumbuka hapa, sasa mtaenda mahakama gani sasa?
wote wamekula wezi tuuKwahiyo mpaka majaji kutoka marekani wale wazungu nao wamepewa hongo?
Aibu kwa zitto wazungu aliokuwa anawapigania wamegongwa mpaka kwenye mahakama za kwao zitto mburula analeta siasa mpaka kwenye mantiki na sheria.Kampuni ya VIP Engineering and Marketing inayoshutumiwa kimakosa kwamba imefanya vitendo vya uvunjifu wa sheria kuhusiana na Akaunti ya Escrow imeibwaga Benki ya Standard Chartered katika shauri lililofunguliwa New York, Marekani. Angalia attachments hapo chini.
Weka wazungu waliokula kwa majina wako wa ngapi aibu kwa zitto hii.wote wamekula wezi tuu
sina muda wa kushindana na mtetea wafu kama weweWeka wazungu waliokula kwa majina wako wa ngapi aibu kwa zitto hii.
mahakama za kuzimu mtaenda nyie wafu ccmKama wamepigwa mpaka marekani basi waende mahakama za kuzimu pengine watashinda.
Nani anamsafisha nani? Kesi aliyeifungua ni SCB kupinga hukumua iliyotolewa awali na mahakama ya New York ambayo ilielekeza kwamba mahakama za Tanzania zinastahili kusikiliza mashauri yanayohusu SCB na VIP. sasa hii kampeni ya kusafisha wezi waliopewa pesa ni nani anaifanya Mahakama za Marekani? Tuwe waadilifu kidogo hata kama tuna mitizamo tofauti katika jambo lolote lile.naona jamaa wameanza kampeni ya kusafisha wezi hasa waliopewa pesa.
Nimesoma nyaraka hizi za ushindi wa VIP Engineering! Nilipita tu ili nisome nielewe ndo nirudi. Nimesoma, nimeelewa, ni wakati wa kuwaambia Watanzania ukweli.
Bila kupepesa macho, naona dhahiri kuwa Zitto na PAC wametumiwa katika wimbo huu wa ESCROW! Nakubali kusahihishwa kwa hoja!! Ndiyo Hoja zije!
1. Zitto na PAC katika ripoti yao wanasema "kamati imebaini kuwa madai ya Standard Chartered ya Hong Kong kwa IPTL ni halali" – Najiuliza vipi Zitto na kamati yake waliweza kuthibitisha uhalali wa Madai ya Standard Chartered wakati suala la kwamba Standard Chartered ni mdai halali liko bado mahakamani?
2. Nimesoma nyaraka zote zinazohusu ushindi wa VIP Engineering taarifa mbalimbali zinazotolewa kuhusu mashauri haya, nalazimika kusema kuwa kama haya niliyogundua ni ya kweli, basi kazi bado ipo kubwa kufikia ukomavu wa kisiasa wa wanasiasa tunaodhani wanatetea Umma. Hebu twende pamoja:
(a) Standard Chartered Bank ambao wanalalamikia Mahakama za Tanzania baada ya kushindwa kuthibitisha kuwa wanalo deni halali (wanalosema eti walilinunua mwaka 2005 huku IPTL ikiwa tayari katika shauri la ufilisi) wanashitakiwa na VIP Engineering ya Ruge nchini Marekani ili kule zijulikane mbichi na mbivu hasa kuhusu uhalali wa linaloitwa deni na madhara ambayo Standard Chartered Bank imesababisha kwa VIP Engineering kwa kujiita mdai wa IPTL.
(b) Standard Chartered Bank baada ya kushitakiwa Marekani kwa woga wa kuumbiliwa tena huko dunia ya kwanza, wanaiambia Mahakama, IPTL imesajiliwa Tanzania, mtambo upo Tanzania, mashahidi wengi wapo Tanzania, tena kesi nyingine kuhusu IPTL zipo Tanzania!!! na wanaendelea kuiambia Mahakama ya Marekani kuwa shauri la Marekani lifutwe ili kesi ikasikilizwe kwenye Mahakama za Tanzania ambako wanakubali kutii amri yoyote ya Mahakama itakayotolewa. Jaji wa Marekani anakubalina na Standard Chartered Bank na kuamua kuwa mgogogo ulioanzishwa na VIP Engineering upelekwe Tanzania.
(c) VIP Engineering kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Standard Chartered inafungua shauri la madai nchini Tanzania dhidi ya Standard Chartered Bank-Shauri ambalo kimantiki ni lilelile lililokuwa Marekani.
(d) Baada ya kuona kweli kuwa VIP Engineering haiweki mzaha katika madai yake, sasa Standard Chartered Bank wanajaribu kukana walichokisema Mahakamani Marekani [WANAKANA KWAMBA WALIKUBALI KUSHITAKIWA TANZANIA, WANAKANA KWAMBA WALIJIFUNGA KUHESHIMU HUKUMU ITAKAYOTOLEWA NA MAHAKAMA YA TANZANIA – AIBU! Wanakata rufaa ambayo ndo sasa wameshindwa. Mahakam ya Rufaa inakubalina na Maamuzi ya Jaji Victor Marrero yaliyosema:
The Court reaffirms its September 10 Order, which relied on Standard Chartered's representations that it considered Tanzania an adequate alternative forum, and which the Court deems an expression of Standard Chartered's consent to the adjudication of this action in Tanzania, and to comply with any final judgment rendered by any court of competent jurisdiction there in connection with the parties' underlying dispute.
(e) Kama vile haitoshi, WAKIWA TAYARI WAMESHITAKIWA NCHINI TANZANIA, baada ya wao wenyewe kuwa wameomba hivyo kwenye kesi waliyoshitakiwa nchini Marekani, wanafungua kesi dhidi ya VIP Engineering nchini Uingereza ambapo wanapinga kushitakiwa Tanzania [HAWA NDIO ZITTO NA PAC wanasema wana deni halali.
(f) Hawa ndio Standard Chartered Bank ambao Zitto na PAC wanasema kwamba mgogoro wao hauwezi kusikilizwa na Mahakama za Tanzania. Hivi haya majumuisho Zitto aliyapata wapi??? Hivi Zitto ni mweredi sana kuliko Mahakama ya Rufaa ya Nchini Marekani??? KWANINI tusiamini Zitto anatumiwa kuendesha kesi ya Standard Chartered kisiasa kwa sababu anauwezo wa kuongelea Bungeni ambako labda waathirika hawawezi kupata nafasi ya kuongelea.
(g) Wakati kukiwa na kesi nchini Tanzania, na kesi iliyofunguliwa baadaye nchini Uingereza, wakati Standard Chartered Bank ikiwa imefungua rufaa ya kukana iliyoyatamka nchini Marekani (Rufaa ambayo dhahili wameshindwa), ni kitu gani kilichofanya Mheshimiwa Barozi wa Uingereza .... atamke kuhusu yaliyo mahakamani, kama kweli haki ndo inayotafutwa. Zitto mwenyewe alitamka Bungeni kuwa alifuatwa – Aibu tupu?
(h) Hivi tukijaribu kuuvaa umakini, kwa wale waliosoma ripoti ya CAG, hivi ni kweli ripoti ya PAC imezingatia mapendekezo ya CAG, au hata kuyatilia maanani, na kama haikufanya hivyo, kwanini sasa CAG alipewa kazi ya kutayarisha ripoti (wakati PAC ilikuwa na uwezo wa kugundua, kuamua na kutoa hukumu.
(i) Zitto! Huyu huyu na PAC eti "kamati ilishangazwa kuona kwamba katika hali isiyokuwa ya kawaida, mahakama .... ilikwenda mbali zaidi na kupanga kiwango cha bei ya umeme kuwa USD 0.6 hadi 0.8 kwa uniti moja ya umeme. Sasa kama VIP Engineering iliweka sharti kuwa anayenunua hisa zake lazima ashushe bei ya umeme, na mnunuzi akakubali, wewe Zitto ni nani hata upinge hiyo bei ya chini! Na hutaki gharama ya umeme ishuke ili iwe nini! Hapo unamtetea Mtanzania kama unavyotaka uaminike?
(j) SASA SWALI LA MWISHO KWA WENYE AKILI: mgogoro wote unaohusu Tegeta Escrow Account unaanzia kwenye suala kuwa – IPTL ime-i-overcharge TANESCO kwenye CAPACITY CHARGES – SASA, ZITTO TWAMBIE, ni kampuni gani inayouza umeme TANESCO ambayo inatoza capacity charges ambazo ni za chini kuliko IPTL? Mimi nafahamu kuwa IPTL ndiyo inatoza tozo ya chini kabisa kwa maana ya capacity charges.
(k) Mpaka ZITTO na wenzako mkiweza kujibu kwa kutaja kampuni yoyote inayotoza tozo ndogo kuliko IPTL (Ili umma ujue kuwa IPTL inainyonya TANESCO) nitaendelea kusema kuwa MNATUMIWA KWA MASLAHI BINAFSI
(l) Ni wakati wa kuacha ushabiki na kujadili hoja...
Mtahangaika kufua, lakini kaniki huo weusi ndio rangi yake. Naona kuna jitihada nyingi sana za kusafishana, lakini ukweli ni kwamba watu waliamua kugawana hela ya umma, hayo mengine nawaachia walio tayari kudanganywa.
Ova
Obama nae atakuwa amepata mgao wa escrow
Mbona zimeandikwa hoja?
leta hoja tukusikie, jibu maswali yaliyoulizw, au kama huna facts tulia usome hoja, jifunze, elewa, shiriki - tusiweza na jazba
HALAFU NAENDELEA KUJIULIZA TENA KWA SAUTI:
[*]Je TANESCO kwa mujibu wa uamuzi wa ICSID wa mwaka 2001 wanadaiwa
fedha kiasi gani na IPTL kwa maana ya fedha waliyotakiwa kuweka kwenye
Tegeta Escrow Account lakini hawakuweka?
[*]Mtu mwenye busara atusomee ukurasa wa 24 wa ripoti ya CAG, na baada
ya hapo atusomee mapendekezo yanayofuata.
[*]Ni dhambi kubwa kufanyia siasa za chuki, siasa za maslahi, siasa za
visasi kwenye chombo tukufu kama Bunge! Bunge ni chombo kitakatifu (au
kinatakiwa kuwa chombo kitakatifu)
[*]ZILETWE HOJA HAPA TUZIJADILI, Watanzania wajue pumba zipi au upi
mchele... tumechoshwa na propaganda zisizokuwa na mantiki.
[/LIST]