Andersy
JF-Expert Member
- Oct 8, 2014
- 586
- 142
Nimesoma nyaraka hizi za ushindi wa VIP Engineering! Nilipita tu ili nisome nielewe ndo nirudi. Nimesoma, nimeelewa, ni wakati wa kuwaambia Watanzania ukweli.
Bila kupepesa macho, naona dhahiri kuwa Zitto na PAC wametumiwa katika wimbo huu wa ESCROW! Nakubali kusahihishwa kwa hoja!! Ndiyo Hoja zije!
1. Zitto na PAC katika ripoti yao wanasema kamati imebaini kuwa madai ya Standard Chartered ya Hong Kong kwa IPTL ni halali Najiuliza vipi Zitto na kamati yake waliweza kuthibitisha uhalali wa Madai ya Standard Chartered wakati suala la kwamba Standard Chartered ni mdai halali liko bado mahakamani?
2. Nimesoma nyaraka zote zinazohusu ushindi wa VIP Engineering taarifa mbalimbali zinazotolewa kuhusu mashauri haya, nalazimika kusema kuwa kama haya niliyogundua ni ya kweli, basi kazi bado ipo kubwa kufikia ukomavu wa kisiasa wa wanasiasa tunaodhani wanatetea Umma. Hebu twende pamoja:
(a) Standard Chartered Bank ambao wanalalamikia Mahakama za Tanzania baada ya kushindwa kuthibitisha kuwa wanalo deni halali (wanalosema eti walilinunua mwaka 2005 huku IPTL ikiwa tayari katika shauri la ufilisi) wanashitakiwa na VIP Engineering ya Ruge nchini Marekani ili kule zijulikane mbichi na mbivu hasa kuhusu uhalali wa linaloitwa deni na madhara ambayo Standard Chartered Bank imesababisha kwa VIP Engineering kwa kujiita mdai wa IPTL.
(b) Standard Chartered Bank baada ya kushitakiwa Marekani kwa woga wa kuumbiliwa tena huko dunia ya kwanza, wanaiambia Mahakama, IPTL imesajiliwa Tanzania, mtambo upo Tanzania, mashahidi wengi wapo Tanzania, tena kesi nyingine kuhusu IPTL zipo Tanzania!!! na wanaendelea kuiambia Mahakama ya Marekani kuwa shauri la Marekani lifutwe ili kesi ikasikilizwe kwenye Mahakama za Tanzania ambako wanakubali kutii amri yoyote ya Mahakama itakayotolewa. Jaji wa Marekani anakubalina na Standard Chartered Bank na kuamua kuwa mgogogo ulioanzishwa na VIP Engineering upelekwe Tanzania.
(c) VIP Engineering kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Standard Chartered inafungua shauri la madai nchini Tanzania dhidi ya Standard Chartered Bank-Shauri ambalo kimantiki ni lilelile lililokuwa Marekani.
(d) Baada ya kuona kweli kuwa VIP Engineering haiweki mzaha katika madai yake, sasa Standard Chartered Bank wanajaribu kukana walichokisema Mahakamani Marekani [WANAKANA KWAMBA WALIKUBALI KUSHITAKIWA TANZANIA, WANAKANA KWAMBA WALIJIFUNGA KUHESHIMU HUKUMU ITAKAYOTOLEWA NA MAHAKAMA YA TANZANIA AIBU! Wanakata rufaa ambayo ndo sasa wameshindwa. Mahakam ya Rufaa inakubalina na Maamuzi ya Jaji Victor Marrero yaliyosema:
The Court reaffirms its September 10 Order, which relied on Standard Chartered's representations that it considered Tanzania an adequate alternative forum, and which the Court deems an expression of Standard Chartered's consent to the adjudication of this action in Tanzania, and to comply with any final judgment rendered by any court of competent jurisdiction there in connection with the parties' underlying dispute.
(e) Kama vile haitoshi, WAKIWA TAYARI WAMESHITAKIWA NCHINI TANZANIA, baada ya wao wenyewe kuwa wameomba hivyo kwenye kesi waliyoshitakiwa nchini Marekani, wanafungua kesi dhidi ya VIP Engineering nchini Uingereza ambapo wanapinga kushitakiwa Tanzania [HAWA NDIO ZITTO NA PAC wanasema wana deni halali.
(f) Hawa ndio Standard Chartered Bank ambao Zitto na PAC wanasema kwamba mgogoro wao hauwezi kusikilizwa na Mahakama za Tanzania. Hivi haya majumuisho Zitto aliyapata wapi??? Hivi Zitto ni mweredi sana kuliko Mahakama ya Rufaa ya Nchini Marekani??? KWANINI tusiamini Zitto anatumiwa kuendesha kesi ya Standard Chartered kisiasa kwa sababu anauwezo wa kuongelea Bungeni ambako labda waathirika hawawezi kupata nafasi ya kuongelea.
(g) Wakati kukiwa na kesi nchini Tanzania, na kesi iliyofunguliwa baadaye nchini Uingereza, wakati Standard Chartered Bank ikiwa imefungua rufaa ya kukana iliyoyatamka nchini Marekani (Rufaa ambayo dhahili wameshindwa), ni kitu gani kilichofanya Mheshimiwa Barozi wa Uingereza .... atamke kuhusu yaliyo mahakamani, kama kweli haki ndo inayotafutwa. Zitto mwenyewe alitamka Bungeni kuwa alifuatwa Aibu tupu?
(h) Hivi tukijaribu kuuvaa umakini, kwa wale waliosoma ripoti ya CAG, hivi ni kweli ripoti ya PAC imezingatia mapendekezo ya CAG, au hata kuyatilia maanani, na kama haikufanya hivyo, kwanini sasa CAG alipewa kazi ya kutayarisha ripoti (wakati PAC ilikuwa na uwezo wa kugundua, kuamua na kutoa hukumu.
(i) Zitto! Huyu huyu na PAC eti kamati ilishangazwa kuona kwamba katika hali isiyokuwa ya kawaida, mahakama .... ilikwenda mbali zaidi na kupanga kiwango cha bei ya umeme kuwa USD 0.6 hadi 0.8 kwa uniti moja ya umeme. Sasa kama VIP Engineering iliweka sharti kuwa anayenunua hisa zake lazima ashushe bei ya umeme, na mnunuzi akakubali, wewe Zitto ni nani hata upinge hiyo bei ya chini! Na hutaki gharama ya umeme ishuke ili iwe nini! Hapo unamtetea Mtanzania kama unavyotaka uaminike?
(j) SASA SWALI LA MWISHO KWA WENYE AKILI: mgogoro wote unaohusu Tegeta Escrow Account unaanzia kwenye suala kuwa IPTL ime-i-overcharge TANESCO kwenye CAPACITY CHARGES SASA, ZITTO TWAMBIE, ni kampuni gani inayouza umeme TANESCO ambayo inatoza capacity charges ambazo ni za chini kuliko IPTL? Mimi nafahamu kuwa IPTL ndiyo inatoza tozo ya chini kabisa kwa maana ya capacity charges.
(k) Mpaka ZITTO na wenzako mkiweza kujibu kwa kutaja kampuni yoyote inayotoza tozo ndogo kuliko IPTL (Ili umma ujue kuwa IPTL inainyonya TANESCO) nitaendelea kusema kuwa MNATUMIWA KWA MASLAHI BINAFSI
(l) Ni wakati wa kuacha ushabiki na kujadili hoja...
Unahangaika kusafisha kilichooza.