Vip engineering yashinda kesi

Vip engineering yashinda kesi

Nimesoma nyaraka hizi za ushindi wa VIP Engineering! Nilipita tu ili nisome nielewe ndo nirudi. Nimesoma, nimeelewa, ni wakati wa kuwaambia Watanzania ukweli.

Bila kupepesa macho, naona dhahiri kuwa Zitto na PAC wametumiwa katika wimbo huu wa ESCROW! Nakubali kusahihishwa kwa hoja!! Ndiyo Hoja zije!

1. Zitto na PAC katika ripoti yao wanasema “kamati imebaini kuwa madai ya Standard Chartered ya Hong Kong kwa IPTL ni halali” – Najiuliza vipi Zitto na kamati yake waliweza kuthibitisha uhalali wa Madai ya Standard Chartered wakati suala la kwamba Standard Chartered ni mdai halali liko bado mahakamani?

2. Nimesoma nyaraka zote zinazohusu ushindi wa VIP Engineering taarifa mbalimbali zinazotolewa kuhusu mashauri haya, nalazimika kusema kuwa kama haya niliyogundua ni ya kweli, basi kazi bado ipo kubwa kufikia ukomavu wa kisiasa wa wanasiasa tunaodhani wanatetea Umma. Hebu twende pamoja:

(a) Standard Chartered Bank ambao wanalalamikia Mahakama za Tanzania baada ya kushindwa kuthibitisha kuwa wanalo deni halali (wanalosema eti walilinunua mwaka 2005 huku IPTL ikiwa tayari katika shauri la ufilisi) wanashitakiwa na VIP Engineering ya Ruge nchini Marekani ili kule zijulikane mbichi na mbivu hasa kuhusu uhalali wa linaloitwa deni na madhara ambayo Standard Chartered Bank imesababisha kwa VIP Engineering kwa kujiita mdai wa IPTL.

(b) Standard Chartered Bank baada ya kushitakiwa Marekani kwa woga wa kuumbiliwa tena huko dunia ya kwanza, wanaiambia Mahakama, IPTL imesajiliwa Tanzania, mtambo upo Tanzania, mashahidi wengi wapo Tanzania, tena kesi nyingine kuhusu IPTL zipo Tanzania!!! na wanaendelea kuiambia Mahakama ya Marekani kuwa shauri la Marekani lifutwe ili kesi ikasikilizwe kwenye Mahakama za Tanzania ambako wanakubali kutii amri yoyote ya Mahakama itakayotolewa. Jaji wa Marekani anakubalina na Standard Chartered Bank na kuamua kuwa mgogogo ulioanzishwa na VIP Engineering upelekwe Tanzania.

(c) VIP Engineering kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Standard Chartered inafungua shauri la madai nchini Tanzania dhidi ya Standard Chartered Bank-Shauri ambalo kimantiki ni lilelile lililokuwa Marekani.

(d) Baada ya kuona kweli kuwa VIP Engineering haiweki mzaha katika madai yake, sasa Standard Chartered Bank wanajaribu kukana walichokisema Mahakamani Marekani [WANAKANA KWAMBA WALIKUBALI KUSHITAKIWA TANZANIA, WANAKANA KWAMBA WALIJIFUNGA KUHESHIMU HUKUMU ITAKAYOTOLEWA NA MAHAKAMA YA TANZANIA – AIBU! Wanakata rufaa ambayo ndo sasa wameshindwa. Mahakam ya Rufaa inakubalina na Maamuzi ya Jaji Victor Marrero yaliyosema:

The Court reaffirms its September 10 Order, which relied on Standard Chartered's representations that it considered Tanzania an adequate alternative forum, and which the Court deems an expression of Standard Chartered's consent to the adjudication of this action in Tanzania, and to comply with any final judgment rendered by any court of competent jurisdiction there in connection with the parties' underlying dispute.

(e) Kama vile haitoshi, WAKIWA TAYARI WAMESHITAKIWA NCHINI TANZANIA, baada ya wao wenyewe kuwa wameomba hivyo kwenye kesi waliyoshitakiwa nchini Marekani, wanafungua kesi dhidi ya VIP Engineering nchini Uingereza ambapo wanapinga kushitakiwa Tanzania [HAWA NDIO ZITTO NA PAC wanasema wana deni halali.

(f) Hawa ndio Standard Chartered Bank ambao Zitto na PAC wanasema kwamba mgogoro wao hauwezi kusikilizwa na Mahakama za Tanzania. Hivi haya majumuisho Zitto aliyapata wapi??? Hivi Zitto ni mweredi sana kuliko Mahakama ya Rufaa ya Nchini Marekani??? KWANINI tusiamini Zitto anatumiwa kuendesha kesi ya Standard Chartered kisiasa kwa sababu anauwezo wa kuongelea Bungeni ambako labda waathirika hawawezi kupata nafasi ya kuongelea.

(g) Wakati kukiwa na kesi nchini Tanzania, na kesi iliyofunguliwa baadaye nchini Uingereza, wakati Standard Chartered Bank ikiwa imefungua rufaa ya kukana iliyoyatamka nchini Marekani (Rufaa ambayo dhahili wameshindwa), ni kitu gani kilichofanya Mheshimiwa Barozi wa Uingereza .... atamke kuhusu yaliyo mahakamani, kama kweli haki ndo inayotafutwa. Zitto mwenyewe alitamka Bungeni kuwa alifuatwa – Aibu tupu?

(h) Hivi tukijaribu kuuvaa umakini, kwa wale waliosoma ripoti ya CAG, hivi ni kweli ripoti ya PAC imezingatia mapendekezo ya CAG, au hata kuyatilia maanani, na kama haikufanya hivyo, kwanini sasa CAG alipewa kazi ya kutayarisha ripoti (wakati PAC ilikuwa na uwezo wa kugundua, kuamua na kutoa hukumu.

(i) Zitto! Huyu huyu na PAC eti “kamati ilishangazwa kuona kwamba katika hali isiyokuwa ya kawaida, mahakama .... ilikwenda mbali zaidi na kupanga kiwango cha bei ya umeme kuwa USD 0.6 hadi 0.8 kwa uniti moja ya umeme. Sasa kama VIP Engineering iliweka sharti kuwa anayenunua hisa zake lazima ashushe bei ya umeme, na mnunuzi akakubali, wewe Zitto ni nani hata upinge hiyo bei ya chini! Na hutaki gharama ya umeme ishuke ili iwe nini! Hapo unamtetea Mtanzania kama unavyotaka uaminike?

(j) SASA SWALI LA MWISHO KWA WENYE AKILI: mgogoro wote unaohusu Tegeta Escrow Account unaanzia kwenye suala kuwa – IPTL ime-i-overcharge TANESCO kwenye CAPACITY CHARGES – SASA, ZITTO TWAMBIE, ni kampuni gani inayouza umeme TANESCO ambayo inatoza capacity charges ambazo ni za chini kuliko IPTL? Mimi nafahamu kuwa IPTL ndiyo inatoza tozo ya chini kabisa kwa maana ya capacity charges.

(k) Mpaka ZITTO na wenzako mkiweza kujibu kwa kutaja kampuni yoyote inayotoza tozo ndogo kuliko IPTL (Ili umma ujue kuwa IPTL inainyonya TANESCO) nitaendelea kusema kuwa MNATUMIWA KWA MASLAHI BINAFSI

(l) Ni wakati wa kuacha ushabiki na kujadili hoja...

Unahangaika kusafisha kilichooza.
 
Unahangaika kusafisha kilichooza.

Kazi kwelikweli ... kama Mtanzania baada ya kupewa hoja, na kuambiwa ajibu kwa hoja ili wananchi wapambanue anaweza akaja na maneno matatu haya, inasikitisha. Hii Forum inajadili mambo makubwa na ndiyo maana mtu akileta "habari" yake anaulizwa source ni nini!!! kwanini unahangaika kuongelea "kilichooza" katikati ya suala ambalo linatakiwa kujadiliwa kwa hekima - Basi tueleze na wewe, kilichooza kwenye hoja hizo ni nini ili Mtanzania ajue! au ulitaka majibu ya "VIP naye kashinda, Standard Chartered wakome" majibu ambayo hayamfanyi Mtanzania aongeze chochote cha kumsaidia kupambanua.
 
Hii Escrow itatufumbua mengi sana. Nilikuwa mtetezi mkubwa wa Zitto lakini baada ya ishu ya Escrow najuta hata kwa nini nilikuwa namtetea. Sikutegemea kama angeweza kuwa muongo na mzandiki kiasi hiki.
 
Last edited by a moderator:
Rudisheni pesa zetu majambawazi wakubwa ninyi
 
Mnanichanganya sasa. Sijui lolote kuhusu sheria, mnapotumia maneno magumu ya kisheria mnanitesa na kunichosha kabisa, nachanganyikiwa. Sasa swali langu ni moja tu, je hii ishu ya escrow na wote waliohusika ni watakatifu? je hakuna pesa yoyote ya sisi walipa kodi ambayo imetafunwa? je wote waliohusika katika kutoa maamuzi yoyote wakati wa mchakato mzima tokea mwanzo hadi mwisho waliyatoa kwa nia njema? Nikiwa kama mtanzania haki yangu ni ipi katika hii ishu. msinichoshe nataka tu nijue endapo kuna eneo fulani nimedhulumiwa au laa, na kama nimedhulumiwa ni nani aliyenidhulumu.
 
Mbona zimeandikwa hoja? leta hoja tukusikie, jibu maswali yaliyoulizw, au kama huna facts tulia usome hoja, jifunze, elewa, shiriki - tusiweza na jazba

HALAFU NAENDELEA KUJIULIZA TENA KWA SAUTI:
  1. Hivi baada ya ule uamuzi wa ICSID wa mwaka 2001 katika kesi ambayo TANESCO walifungua dhidi ya IPTL, kesi ambayo ndiyo iliyoweka kiasi cha tozo ambacho TANESCO walitakiwa kulipa kwa IPTL, Je kuna uamuzi wowote ambao ulishabatilisha huo uamuzi wa mwaka 2001? Zitto twambie ripoti ya CAG inasemaje kuhusu hili?
  2. Je TANESCO kwa mujibu wa uamuzi wa ICSID wa mwaka 2001 wanadaiwa fedha kiasi gani na IPTL kwa maana ya fedha waliyotakiwa kuweka kwenye Tegeta Escrow Account lakini hawakuweka?
  3. Mtu mwenye busara atusomee ukurasa wa 24 wa ripoti ya CAG, na baada ya hapo atusomee mapendekezo yanayofuata.
  4. Ni dhambi kubwa kufanyia siasa za chuki, siasa za maslahi, siasa za visasi kwenye chombo tukufu kama Bunge! Bunge ni chombo kitakatifu (au kinatakiwa kuwa chombo kitakatifu)
  5. ZILETWE HOJA HAPA TUZIJADILI, Watanzania wajue pumba zipi au upi mchele... tumechoshwa na propaganda zisizokuwa na mantiki.

Hahahahaaaa! Hata shetani alitumia maandiko ya Biblia kwa kumjaribu Yesu Kristo ambaye alikuwa mwerevu na kuyashinda majaribu yake na kuendelea kuutangaza utukufu wa Mungu.
Isitoshe, licha ya kutumia maandiko matakatifu haikutosha kumsafisha shetani, alibaki kuwa shetani vilevile kwa kuwa alitaka kuyatumia maandiko ili kufanikisha uovu wake.
Mwishoni mwa majaribu, Yesu alisema "Nenda zako shetani!" Nami nakwambia hivi, "Nenda zako kibaraka wa Mafisadi."
(Matthew 4:6-11)
Ova
 
sasa hivi watadai VIP imeshinda kwa sababu...actually Simba trust inamilikiwa na maliah na sasha obama according to brela ya Australia.. hahaahha.
 
Hahahahaaaa! Hata shetani alitumia maandiko ya Biblia kwa kumjaribu Yesu Kristo ambaye alikuwa mwerevu na kuyashinda majaribu yake na kuendelea kuutangaza utukufu wa Mungu.
Isitoshe, licha ya kutumia maandiko matakatifu haikutosha kumsafisha shetani, alibaki kuwa shetani vilevile kwa kuwa alitaka kuyatumia maandiko ili kufanikisha uovu wake.
Mwishoni mwa majaribu, Yesu alisema "Nenda zako shetani!" Nami nakwambia hivi, "Nenda zako kibaraka wa Mafisadi."
(Matthew 4:6-11)
Ova

usiende haraka haraka, kabla hajamwambia "nenda zako shetani", kwanza alimjibu kila verse kwa verse, hivyo na wewe jibu kwanza hizo "verse za shetani" kabla hujamfukuza.
 
Hii Escrow itatufumbua mengi sana. Nilikuwa mtetezi mkubwa wa Zitto lakini baada ya ishu ya Escrow najuta hata kwa nini nilikuwa namtetea. Sikutegemea kama angeweza kuwa muongo na mzandiki kiasi hiki.

mkuu wabunge wa siku hizi si wakweli wakiambiwa sawa na komed wanakasirika pamoja na vyombo wa habari hapa tz
 
Last edited by a moderator:
usiende haraka haraka, kabla hajamwambia "nenda zako shetani", kwanza alimjibu kila verse kwa verse, hivyo na wewe jibu kwanza hizo "verse za shetani" kabla hujamfukuza.

wenye akili lazima wameona hoja (ilipo hoja) na pumba (ilipo pumba!)
Mwache aendelee na propaganda, anayo haki ya kujionesha namna anavyofikiria kwa jamii.
Tumpe tu heri ya noeli na mwaka Mpya
 
Nani anamsafisha nani? Kesi aliyeifungua ni SCB kupinga hukumua iliyotolewa awali na mahakama ya New York ambayo ilielekeza kwamba mahakama za Tanzania zinastahili kusikiliza mashauri yanayohusu SCB na VIP. sasa hii kampeni ya kusafisha wezi waliopewa pesa ni nani anaifanya Mahakama za Marekani? Tuwe waadilifu kidogo hata kama tuna mitizamo tofauti katika jambo lolote lile.

waambie hao wezi wa pesa wawe waadilifu maana kila uchwao wanatafuta vibaraka wa kuwatetea. huyo mzee wa ugolo pesa zingekuwa zake asingegawa kama njugu maana mgao ulikuwa na formula kabisa 1.6 b, 404m. Huyo waziri tiba anapigwa chini kesho!!!!
 
Tatizo watu fulani wachache wamejawa na jazba ya kushabikia vitu sensitive kimzahamzaha kila wanapoona ni fursa ya wao kujinufaisha kisiasa kwa kuupotosha umma.
Ni kweli kabisa. Kwani kama kweli ripoti ya CAG ilikuwa ndiyo inayotakiwa kutumika ili kutoa mapendekezo kwa Bunge ili nalo liweze kutoa mapendekezo sahihi kwa Serikali sasa iweje kamati ya Bunge iachane na ripoti ya CAG na badala yake kutoa mapendekezo yake kutoka katika vichwa na hisia za watu wachache?
Ni vizuri suala la kuheshimu sheria na taratibu za nchi zikaanzia katika kamati za Bunge na kuachana na mchezo mchafu wa kutumia nafasi hizo kwa ajili ya malengo binafsi. Kama kuna mtu wa kuwajibishwa kwa hakika ni Zitto Zuberi Kabwe ili atuelezee hizo tuhuma zimetoka wapi wakati ripoti ya CAG haisemi hivyo wala haijengo taswiar ya kutoa mwanya kwa mtu kufanya maamuzi ya kijinai kama ambavyo imesisitizwa katika ripoti yote ya PAC? tuambiwe kwani tunastahili kuambiwa ukweli.
 
Back
Top Bottom