Vipi kauli ya Kagame kuwa Rwanda ingekuwa na bandari kama ya Dar, huduma zote Rwanda zingekuwa bure?

Kilasi Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
2,325
Reaction score
723
Vyombo mbalimbali vya habari viliripoti kuhusu kauli hii ya Raisi wa Rwanda Paul Kagame kuwa Kuwepo kwa Bandari ya Dar Tanzania ilipaswa kupaa kabisa kiuchumi hasa kutokana na kuzungukwa na nchi kadhaa zinazo tegemea kusafirisha mizigo yake.

Zipo nchi nyingi duniani ambazo kwa bandari pekee zimepata kupaa kiuchumi miongoni mwao ikiwamo Hongkong ,Singapore,Uholanzi nk.Lakini kwanini Tanzania Hatuoni mabadiliko ya kiuchumi yakiwa dhahiri kutokana na bandari hii?

Miradi mingi ya kiuchumi ni mikopo toka kwa wahisani.Barabara kama ya DOM-IRINGA ni mkopo toka Benki ya Africa,na miradi mingi ni mikopo toka kwa wahisani kiasi sasa kila Mtanzania mpaka mtoto mdogo anadaiwa zaidi ya Tsh 450000(laki nne na nusu).Fedha za mapato kama ya bandari hii huenda wapi?Kuna harufu ya ufisadi wa mapato ya bandari kwa kiasi kikubwa.

Napata shaka kuona kuna benk kama M Benki imbayo tawi lake limo ndani ya jengo la ofisi za mapato.Mtu analipia pale na document yake ni halali palepale na mzigo unatoka.

Hii benki niya nani?Benki zingine ukilipia document yake mpaka mpaka iende hazina ku verify ndipo uchukue mzigo.

Naona kama mafisadi wananjia zao za kuchota hela kirahisi kama kupitia benki hii,labda ndiyo maana hatuoni mabadiliko yoyote ya kiuchumi.

Gari moja ndogo inayo pita kwenda nchi nyingine hulipia sichini ya 3000000/=(milioni tatu) na gari pale zinapita kama maji tu.Pita barabara ya Dar-Tunduma uone gari zenye number ya IT utapata picha ya hoja hii pata picha ya 300.
 
Vijana wakiacha maandamano na kuhudhuria mikutano ya vyama vya siasa na badala yake wakajikita katika kufanya kazi nchi hii itafika mbali.

Usivyo na akili undhani maandamano ni ugaidi! ni khaki ya kikatiba!! nchi haiwezi kupiga hatua had I CCM ife!
 
Vijana wakiacha maandamano na kuhudhuria mikutano ya vyama vya siasa na badala yake wakajikita katika kufanya kazi nchi hii itafika mbali.
Web huna lolote,hata tukifanya kazi kwa bidii zote,kama mafisadi wanazichota tu nakuzitorosha itasaidia nini mkuu?Dawa hawa watoke wajaribu wengine
 
Vijana wakiacha maandamano na kuhudhuria mikutano ya vyama vya siasa na badala yake wakajikita katika kufanya kazi nchi hii itafika mbali.

Sir magdalena kazi nafanya kwa bidii lakini ujira hautoshi mahitaji yangu niambie kama umeme juu mafuta juu dawa juu chakula juu nyumba juu sasa hapa nita achaje kuandamana???Amani ya Bwana iwe nawe Sr!
 
Last edited by a moderator:
Nchi hii ina kila kitu isipokuwa uongozi tu!Kagame yupo sahihi kabisa!

Kagame kwenye issue inayogusa taifa lake, kwamtu yeyote mwizi wa Mali ya umma hana urafiki, hakika nikiongozi wa mfano katika nchi zinazoendelea anajua wajibu wake kwa watu wake,Rwanda hakuna migogoro ya Ardhi, hakuna tofauti ya elimu inayotolewa kwa wanafunzi wa nchi yake, hapa kwetu ni vigumu kujua kipi kinachosimamiwa na mkuu wa nchi, Rwanda kinachochukiwa na mkuu wa nchi kinajulikana, hapendi rushwa wala rushwa wakijulikana wanawajibishwa, rais anawajibika kwa kadri .madaraka yake yalivyo, hapakwetu hadithi, kila idara inafanya inavyotaka, Angekuwa Kagame bandali isingerundikana mizigo, wala hadithi ya rushwa ingekuwa historia,Kagame akipewa bandari
 
Vyombo mbalimbali vya habari viliripoti kuhusu kauli hii ya Raisi wa Rwanda Paul Kagame kuwa Kuwepo kwa Bandari ya Dar Tanzania ilipaswa kupaa kabisa kiuchumi hasa kutokana na kuzungukwa na nchi kadhaa zinazo tegemea kusafirisha mizigo yake.

Zipo nchi nyingi duniani ambazo kwa bandari pekee zimepata kupaa kiuchumi miongoni mwao ikiwamo Hongkong ,Singapore,Uholanzi nk.Lakini kwanini Tanzania Hatuoni mabadiliko ya kiuchumi yakiwa dhahiri kutokana na bandari hii?

Miradi mingi ya kiuchumi ni mikopo toka kwa wahisani.Barabara kama ya DOM-IRINGA ni mkopo toka Benki ya Africa,na miradi mingi ni mikopo toka kwa wahisani kiasi sasa kila Mtanzania mpaka mtoto mdogo anadaiwa zaidi ya Tsh 450000(laki nne na nusu).Fedha za mapato kama ya bandari hii huenda wapi?Kuna harufu ya ufisadi wa mapato ya bandari kwa kiasi kikubwa.

Napata shaka kuona kuna benk kama M Benki imbayo tawi lake limo ndani ya jengo la ofisi za mapato.Mtu analipia pale na document yake ni halali palepale na mzigo unatoka.

Hii benki niya nani?Benki zingine ukilipia document yake mpaka mpaka iende hazina ku verify ndipo uchukue mzigo.

Naona kama mafisadi wananjia zao za kuchota hela kirahisi kama kupitia benki hii,labda ndiyo maana hatuoni mabadiliko yoyote ya kiuchumi.

Gari moja ndogo inayo pita kwenda nchi nyingine hulipia sichini ya 3000000/=(milioni tatu) na gari pale zinapita kama maji tu.Pita barabara ya Dar-Tunduma uone gari zenye number ya IT utapata picha ya hoja hii pata picha ya 300.
Mkuu hiyo millioni 3 uliyotaja is kweli gari ndogo inalipiwa jumla dollar 350 watu waclearing wanakula dollar 50 hadi 100 kwahiyo 200 yadollar inabaki bandarini fanya marekebisho

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Tuwakatae ccm/mafsad

Mmoja wa watu wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi ameonyesha nia ya kuutaka kiana. Watu humu humu JF wanampigia debe. Kwa mtindo huu nchi hata kama ingekuwa na bandari kumi tusingeendelea.
Kibaya zaidi, kuna wandishi na magezeti ikiwemo Tz Daima kazi ni kuwapaka matope wengine na kumsafisha huyo jamaa kiana. Kuna makala moja kila jumatano ktk gazeti hilo hunitia hasira. Sijui huyo mwandishi kapewa nini. Hahawaji kuona baya hata moja la huyo jamaa. Jamani njaa kitu kibaya sana
Kagame yupi sahihi maana amedhibita rushwa ktk nchi yake. Pesa za serikali yake pamoja na misaada zinatumika vizuri. Hakuna muujiza mwingine.
Tanzania tunabadilisha tu aina ya wezi madarakani. Mfupi, mrefu, meusi, mweupe, sura mbaya, handsome nk lkn sifa kuu yao moja tu: wezi wala rushwa wakubwa.
Tunahitaji Kagame wetu
 
Jamani kiongozi bora ni muhimu sana ktk kila kitu....hata tungekuwa na mgodi hela kama kiongozi mbaya hakuna kitu....Angalieni Man U..wana kila mchezaji mzuri ila kwa kuwa hawana kocha mzuri wqnashindwa ....hata nyerere alsisema ili tuendelee tunahitaji Kiongozi bora
 
Sir magdalena kazi nafanya kwa bidii lakini ujira hautoshi mahitaji yangu niambie kama umeme juu mafuta juu dawa juu chakula juu nyumba juu sasa hapa nita achaje kuandamana???Amani ya Bwana iwe nawe Sr!

Sr. Magdalena jibu uzi huu tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom