Vipi kauli ya Kagame kuwa Rwanda ingekuwa na bandari kama ya Dar, huduma zote Rwanda zingekuwa bure?

Vipi kauli ya Kagame kuwa Rwanda ingekuwa na bandari kama ya Dar, huduma zote Rwanda zingekuwa bure?

Mkuu..Reli ni kila kitu

Na reli inahujumiwa na wenye malori

Kama unakumbuka Hanspope alimkashifu sana Minister Magufuli kipindi akiwa ujenzi...alipopiga stop malori yenye uzito unaozisi
Ni suala la muda tu. Hayo malori ya akina Hans Pope yatakuja kuwa kama chai maharage. Baada ya Hiace na Coaster kuingia kwa wingi walienda shamba bila kufukuzwa.

Malori lazima yafanye kazi sehemu inakoishia reli. Gharama za nafaka ni kubwa kwa sababu ya malori. Ingekuwa ni usafiri wa reli, ingekuwa nafuu sana.
 
Uko sahihi mkuu....Tunahitaji reli ndio msingi wa maendeleo na usafirishaji usio na wasiwasi

Mfano hata dar...solution ilikuwa ni Reli ...haya magari piga stop kuingia mjini...mji unakuwa msafiiiiii

Hivi gesi ya mtwara si ilishaanza kutoka....Mbona bei ya umeme haijashuka?

Tulitegemea gesi hii ingeweza kutumika hata kwa electric train
 
Kagame alikubali kuitwa dikteta kwa ajili ya maendeleo ya nchi yake hapa kwetu JMP kaanza tayari baadhi wanaleta maneno oh huyo ni udikteta
Kwa maana hiyo kakame na magufuli sasa wapo sahihi kufanya mazuri ya nchi yao

Waafrica tunahitaji "development dictatorship". Na hili naliunga mkono..Hata hivyo Mbona bado magufuli sio dictator? anatekeleza sheria alizozikuta..hajatunga sheria mpya...kazitoa sheria kabatini. Hilo ndo alifanyalo..Tatizo watanzania tulizoea business as usual. Aidha hatuwezi kumlinganisha na Kagame katika suala la kile kinachoitwa "udikteta" hususani katika masuala ya pure politics..Shortly Go magufuli, go, go, go..Hata patakapohitaji kukaza buti kwa sheria mpya tunga tu ili mradi zinalenga kuleta "Development DIctatorship"
 
Vyombo mbalimbali vya habari viliripoti kuhusu kauli hii ya Raisi wa Rwanda Paul Kagame kuwa Kuwepo kwa Bandari ya Dar Tanzania ilipaswa kupaa kabisa kiuchumi hasa kutokana na kuzungukwa na nchi kadhaa zinazo tegemea kusafirisha mizigo yake.

Zipo nchi nyingi duniani ambazo kwa bandari pekee zimepata kupaa kiuchumi miongoni mwao ikiwamo Hongkong ,Singapore,Uholanzi nk.Lakini kwanini Tanzania Hatuoni mabadiliko ya kiuchumi yakiwa dhahiri kutokana na bandari hii?

Miradi mingi ya kiuchumi ni mikopo toka kwa wahisani.Barabara kama ya DOM-IRINGA ni mkopo toka Benki ya Africa,na miradi mingi ni mikopo toka kwa wahisani kiasi sasa kila Mtanzania mpaka mtoto mdogo anadaiwa zaidi ya Tsh 450000(laki nne na nusu).Fedha za mapato kama ya bandari hii huenda wapi?Kuna harufu ya ufisadi wa mapato ya bandari kwa kiasi kikubwa.

Napata shaka kuona kuna benk kama M Benki imbayo tawi lake limo ndani ya jengo la ofisi za mapato.Mtu analipia pale na document yake ni halali palepale na mzigo unatoka.

Hii benki niya nani?Benki zingine ukilipia document yake mpaka mpaka iende hazina ku verify ndipo uchukue mzigo.

Naona kama mafisadi wananjia zao za kuchota hela kirahisi kama kupitia benki hii,labda ndiyo maana hatuoni mabadiliko yoyote ya kiuchumi.

Gari moja ndogo inayo pita kwenda nchi nyingine hulipia sichini ya 3000000/=(milioni tatu) na gari pale zinapita kama maji tu.Pita barabara ya Dar-Tunduma uone gari zenye number ya IT utapata picha ya hoja hii pata picha ya 300.
Labda tumwachie Kagame kwa miaka mitano tuone kama hayo aliyoyasema ni ya kweli au porojo tu.
 
Tanzania Ina rasilimali za kuweza kuifanya itoe huduma buree au kwa gharama nafuu kwa watu wake...
Lakini tatizo la msingi lipo kwenye Elite Capture!
Ukitaka ujue nasema nini rejea:
1. Matumizi ya anasa ya viongozi na wateule
2. Kodi na tozo kandamizi
3. Mifumo isiyoendelevu
4. Roho mbaya, chuki, fitina dhidi ya wananchi
 
Mkuu, kwani wewe hupendi viongozi wako waishi vizuri? Hupendi kuwaona viongozi wako wakitumia mav8 ya maana ambayo hata Mawaziri wa vinchi kama Sweden na Denmark hawana?

Jisikie fahari kiongozi wako kuishi kifahari!

Unajua kuwakilishwa nako ni heshima? Iko hivi, kiongozi wako akitumia gari la kifahari, anakuwa amefanya hivyo kwa niaba yako, kwa hiyo ni wewe ndiye uliyetumia.
 
KWELI. Ni fahari sana asee! Tunafurahi 😭😭😭
 
Back
Top Bottom