Wakuu kwa hali ilipofikia nafikiri ni wakati sahihi kumkabidhi rais Kagame bandari ya Dar es salaam aiendeshe,kisha tugawane mapato nina imani kabisa na rais Kagame endapo ataisimamia basi watanzania watanufaika na matunda ya bandari hiyo kwa haraka zaidi kuliko kuachia uozo ulipo kutoka kwa THE UNTOUCHABLE ONE.
Leo hii katika jumuiya ya Afrika Mashariki Kenya ndio nchi yenye uchumi imara zaidi ikifuatiwa na Rwanda.
Shimeshime watanzania msione aibu kwenye hili kwani linagusa moja kwa moja maslahi ya taifa.
Pia nimegundua mifumo ya CCM ina tabia ya kuwaonea aibu viongozi wake wakongwe kushindwa kuwakabili pindi wanapofanya uovu.
Nadhani uchumi unakupiga chenga kwa sasa hivi Kenya ndio inayoongoza kwa uchumi mzuri ikiwa na GDP ya usd 65 bilions tanzania ni ya pili ikiwa na usd 49.5 bilion uganda ni ya tatu ikiwa na
usd 27.6 bilion rwanda ni ya nne ikiwa na usd 8.5 bilion. Rwanda ni taifa dogo sana kiuchumi kwa tanzania.