Vipi kauli ya Kagame kuwa Rwanda ingekuwa na bandari kama ya Dar, huduma zote Rwanda zingekuwa bure?

Vipi kauli ya Kagame kuwa Rwanda ingekuwa na bandari kama ya Dar, huduma zote Rwanda zingekuwa bure?

Tunakuwa wavivu kupeleka watu wetu kujifunza kwenye bandari za wenzetu Ni kwavipi wameweza kudhibiti mapato.
tunafanya mambo makubwa kwa kupapasa.
 
Tunakuwa wavivu kupeleka watu wetu kujifunza kwenye bandari za wenzetu Ni kwavipi wameweza kudhibiti mapato.
tunafanya mambo makubwa kwa kupapasa.
Mkuu hili.linaloendelea siyo sababu ya uelewa. Ni mambo yanafanywa makusudi kupiga pesa.
 
Sio Kagame tu aliyekuwa sahihi kutufikishia ujumbe wenye ukweli ndani yake. Rais Magufuli alikuwa sahihi kusitisha safari za nje ya nchi kwa wanasiasa na watendaji wa serikali, wabunge wetu kila mwaka walikuwa wanafunga safari kwenda nje kujifunza namna ambavyo serikali za wenzetu zinavyofanya kazi. Katika hao waliokuwa wanakwenda nje walikuwepo wajumbe wa kamati maalum ya bunge katika masuala ya mawasiliano na uchukuzi. Walikuwa wanakwenda nje wakati huo huo wafanyabiashara wenye roho za kinyama wakiihujumu bandarini yetu kiasi cha kupata hasara kwenye uingizaji wa mafuta.

Rais Magufuli na wasaidizi wake hawazitilii mkazo safari za nje na kwa jinsi wanavyozibana sekta zote ikiwemo bandari, wanathibitisha kuwa hakuna haja ya kupoteza fedha kwenda nje halafu kinachopatikana kutokana na hizo safari wala hakina tija ya moja kwa moja kwenye uongezaji wa ufanisi wa sekta zote zilizo chini ya serikali.

Mahitaji mengi ya Taifa yanaweza kutimizwa ikiwa tu rasilimali zitaelekezwa kule zinakopaswa kuelekezwa. Hizi mbwembwe za kwenda nje kujifunza kwa wenzetu, ni mzigo kwa bajeti zetu. Maendeleo yanaweza kupatikana na yakayagusa maisha ya kila Mtanzania cha muhimu ni kutanguliza maslahi sahihi ya Taifa na sio yale ya wafanyabiashara ambao baada ya kupata utajiri wenye harufu ya unyonyaji, huanza kuwadharau wale wale waliowatajirisha.
 
Bandarini washazoea kuiba lzma wabanwe ikiwa VP wapewe adhabu Kali kifungo+bakora za kutosha mpaka watie akili!
 
Sasa nimemkubali mh. Kagame kuwa alikuwa sahihi pale aliposema kuwa bandari pekee ingetosha kukusanya mapato ya kutosha kuweza kuendesha nchi yake bila kukimbizana maporini na wachimbaji wadogowadogo. Alipotoa kauli hiyo baadhi yetu watanzania tuliona kuwa ni dharau kwa rais wetu JK lakini kwa sasa historia imeanza kumtakasa kutokana na kile alichokisema kuanza kusimamiwa kwa ukamilifu na Serikali hii ya awamu ya tano ya mh. Magufuli.
 
Mambo mengi ambayo Rais Kagame ameyafanya kwenye nchi yake na kumletea maendeleo katika nchi yake ya Rwanda sisi Tanzania ndiyo tumeanza kuyafanya sasa. Hii imenifanya kuanza kuamini kuwa tunahitaji Rais aina ya Kagame kuweza kupata maendeleo ya kweli katika nchi yetu.
 
Watanzania sasa tunahitaji kiongozi ambaye ni dikteta mzalendo
 
Mambo mengi ambayo Rais Kagame ameyafanya kwenye nchi yake na kumletea maendeleo katika nchi yake ya Rwanda sisi Tanzania ndiyo tumeanza kuyafanya sasa. Hii imenifanya kuanza kuamini kuwa tunahitaji Rais aina ya Kagame kuweza kupata maendeleo ya kweli katika nchi yetu.
Kuna watu wanasema eti Kagame amefanikiwa kwa sababu Rwanda ni nchi ndogo!. Dunia inazo nchi ngapi ambazo ni ndogo kwa eneo lakini ni masikini kupindukia?. Seriousness haijawahi kuwepo Tanzania, JPM amekuja kivingine na anaweza kuiweka sawa hii nchi.
 
Mtanzania akiambiwa ukweli huwa anaishia kumtukana mleta ujumbe badala ya kuupima ujumbe kama unafaida maishani mwake. Umasikini wetu kwa kiasi kikubwa sana unasababishwa na sisi wenyewe. Ukitaka kuipima akili yetu jinsi ilivyo mbovu, tazama timu moja ya kigeni inapokuja kucheza na Yanga, jinsi ambavyo mashabiki wa simba watakavyofanya kila liwezekanalo kuihujumu Yanga. Na wakati mwingine Simba inapojiandaa kucheza na timu ya nje, wale watu wa Yanga wanafanya kila liwezekanalo ili mradi tu Simba ifungwe.

Uchukue mfano huo huo kwani unafaa kutumika hata kwenye masuala ya siasa. Mtu anaihujumu nchi yake pekee aliyopewa na Mungu. Zipo habari za chini ya kapeti kuwa hata mgao wa umeme ni hujuma ya baadhi ya watanzania. Mtu anauhujumu uchumi wa nchi yake mwenyewe, anayahujumu maisha ya ndugu zake wa damu!!. Paul Kagame aliposema apewe bandari yetu na fedha itakayopatikana itailisha Tanzania na Rwanda, alikuwa sahihi kabisa. Aliuona uzembe wetu, aliuona ukosefu wetu wa uzalendo.

Lakini mtanzania ukimwambia ukweli anaishia kukuita mtutsi, badala ya kupima uzito wa hoja anaishia kumshambulia mtoa hoja. Tanzania ikiwa kama mgonjwa ni lazima ipewe dozi sahihi ya dawa ili iweze kupona.
 
Wakuu kwa hali ilipofikia nafikiri ni wakati sahihi kumkabidhi rais Kagame bandari ya Dar es salaam aiendeshe,kisha tugawane mapato nina imani kabisa na rais Kagame endapo ataisimamia basi watanzania watanufaika na matunda ya bandari hiyo kwa haraka zaidi kuliko kuachia uozo ulipo kutoka kwa THE UNTOUCHABLE ONE.

Leo hii katika jumuiya ya Afrika Mashariki Kenya ndio nchi yenye uchumi imara zaidi ikifuatiwa na Rwanda.

Shimeshime watanzania msione aibu kwenye hili kwani linagusa moja kwa moja maslahi ya taifa.

Pia nimegundua mifumo ya CCM ina tabia ya kuwaonea aibu viongozi wake wakongwe kushindwa kuwakabili pindi wanapofanya uovu.
 
aisee,huyu ksgame mporaji wa almasi za congo tumpe bandari yetu!!!tutake radhi mkuu.
 
Wakuu kwa hali ilipofikia nafikiri ni wakati sahihi kumkabidhi rais Kagame bandari ya Dar es salaam aiendeshe,kisha tugawane mapato nina imani kabisa na rais Kagame endapo ataisimamia basi watanzania watanufaika na matunda ya bandari hiyo kwa haraka zaidi kuliko kuachia uozo ulipo kutoka kwa THE UNTOUCHABLE ONE.

Leo hii katika jumuiya ya Afrika Mashariki Kenya ndio nchi yenye uchumi imara zaidi ikifuatiwa na Rwanda.

Shimeshime watanzania msione aibu kwenye hili kwani linagusa moja kwa moja maslahi ya taifa.

Pia nimegundua mifumo ya CCM ina tabia ya kuwaonea aibu viongozi wake wakongwe kushindwa kuwakabili pindi wanapofanya uovu.
ondoa dharau zako hapa,kwani hapa hakuna Serikali,badili na uraia basi uende huko kwa Kagame
 
Back
Top Bottom