uholanzi, hongkong, singapore,,, usitolee mfano TZ na hizi nchi, rudi nyuma 1700 t0 1800 uone hawa walikuwa wapi na sisi tulikuwa wapi.
unapoongelea tz jaribu, kuifananisha na nchi nyingine, za africa.. tanzania ni ya 13 kwa GDP kwa africa kenya ni ya 12. hiyo ghana ulioitaja ni ya 9 huyo kagame na ruanda yake uliowataja wako chini huko. (rejea hizi taarifa kwenye mitandao utaona)
ni kweli tanzania inasumbuliwa na ufisadi kama zilivyo nchi zote za africa (hii ni tabia ya waafrica, ambayo bila shaka hata wewe unayo).
KAGAME ni mtu ambaye amefanya yakwake kwa nchi yake na sio yote amefanya KIGALI, tena kwa msaada aliopewa na jumuia ya kimataifa wakati wa GENOCIDE.(huu ni msaada alipewa na sio mkopo kwa ajili ya kuijenga RWANDA) kwa hiyo asijisifie kabisa kwani hii ni sawa na wale wanaopewa mitaji na baba zao halafu ukawacompare na wale wanaofight wenyewe. nafikili unasikia jinsi gani watu wanavyoikimbia RWANDA.
Kama watanzania tunatakiwa tuwape viongozi pressure mda wote (waafrica, hatuwapi direct pressure watawala, tunaishi kinafiki sana).
mkuu omba upate nafasi ya kuzungukia nchi nyingi za africa, utaona jinsi gani tunavyofanana kimaisha na kiuchumi, ni uongo mtu kusema kuna nchi ya africa (ukiondoa waarabu na s/africa kuna sababu zake) imeendelea wote tuko sawa utapoongelea umasikini wa tanzania, unaongelea umasikini wa AFRICA. Tutakiwa wote tuwe wazalendo kwa africa, tufanye kazi kwa bidii, tuache unafiki, tuwape watawala direct force ya kufikia malengo.