Qute cherry
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 294
- 136
Napenda siku moja nijaribu skydiving na wewe Mbingu duniani... Nimejitahidi sasa hivi naweza kuruka kutoka kwenye ndege mwenyewe bila kuruka na mtu... Adrenaline stunt hizo kama ni moja ya ur imaginations...hahaaaaaaaaa chezea kupanda ndege lol..usingizi haaukuja hata
nikisoma hii thread nacheka sana
Nakumbuka ilikuwa Mwaka 2008 mwezi Juni nilikuwa naenda kikazi Lusaka, Zambia basi sijui hili wala lile kwenye tiketi iliandikwa saa ya ndege kuondoka mimi nikajipa kama dakika 20 hivi ndo niwe airport duuh ile kufika nikaambiwa muda umeisha daah! Nilichoka. But taratibu nikajifunza muda wa kufika airport, vitu visivyoruhusiwa kubeba kwenye ndege...HAKIKA USHAMBA MZIGO
Nakumbuka ilikuwa Mwaka 2008 mwezi Juni nilikuwa naenda kikazi Lusaka, Zambia basi sijui hili wala lile kwenye tiketi iliandikwa saa ya ndege kuondoka mimi nikajipa kama dakika 20 hivi ndo niwe airport duuh ile kufika nikaambiwa muda umeisha daah! Nilichoka. But taratibu nikajifunza muda wa kufika airport, vitu visivyoruhusiwa kubeba kwenye ndege...HAKIKA USHAMBA MZIGO
bukoba -mwanza.....vile vindege vidogo...hiyo siku kulikuwa na mvua sana asubuhi..wakati tunaingia kwenye ndege tukaambiwa tuzime simu zetu ila kuna watu nikawaona wanaendelea kutumia simu wakiwa ndani kabla hatujaondoka...ile tunaondoka tu airport kandege kakaanza kuyumba yumba mara pailot akarudia tangazo watu wote wazime simu...mimi simu yangu nilitoa na betri kabisaaaa..
Sina, kwani huwa anafanya logarithm akiwa anasafiri? una swali jingine?
uuuwi! Jf is nv boring!
Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.
Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.
Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.
Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.
Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.
Mi naona ndiyo nimecheka zaidi
Hasa nikikumbuka mi ngazi za Jomo Kenyatta airport zilivyonitoa nishai
nilivyoona ngazi zinatembea nikataka kurudi nilikotoka but toka mwa huo wa 1998 mpaka leo ngazi za hivyo sizipendi kabisa!!!!!!!!!!
Hana uwongo wwt..watu tumeanza kupanda ndege enzi hizo kipindi cha mwalimu..williamson diamonds mwadui walikua na ndege 4 tulikua tunapanda tu kwenda madhuleni tunashikia dar..ndege ilikua kawaida sana kama uda tu kariakoo to mwenge!
Kuna mzee aliingia he was kinda late yeye ndo alikuwa wa mwisho, basi alipofika mbele kidogo akapayuka maneno haya nakumbuka " BASIIIIII, KWISHAAAAA, TAYARIIIII" watu tukashituka huyu dingi vipi akasema jamani nina miaka 68 leo ndo napanda ndege kwa mara ya kwanza.
mi nilianzia ndege za kijeshi 1990, niliona powa tu, kwasasa i dont talk about ndege kwakuwa ndege is my life.Ombea usianzie kwenye ndege za jeshi,utajuta! But saiv naona kwaida tu kwenye ndege za aibiria na jeshi pia
Umenikumbusha Mbal sn 1990's uko Dar-Mwadui na Williamson Diamonds enz iZo Ndo ilikuaga habar ya mujin enz izo dec holiday mnaenda Shinyanga kwa Bib na Bab kwel zile ndege zina historia enz za Mwalim.Hana uwongo wwt..watu tumeanza kupanda ndege enzi hizo kipindi cha mwalimu..williamson diamonds mwadui walikua na ndege 4 tulikua tunapanda tu kwenda madhuleni tunashikia dar..ndege ilikua kawaida sana kama uda tu kariakoo to mwenge!
HaHAHAhaha umenikumbusha mbaali sana!kioja changu kilikuwa kwenye pasport jamani.. nilipata ile ya muda as ilikuwa ya karatasi huyo mbio stationary kuifanyia lamination eti isiharibike. Walahi kama sio yule binti wa stationery sijui huko airport ingekuwaje ..looo!