Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Usifanye mchezo na mara ya kwanza kupanda ndege aisee unaweza kupata tumbo la kuhara mi nilishawahi kupanda na mhaya flani tunaelekea mwanza kutoka dar, sasa kwa kuwa alikuwa hataki ajulikane kuwa ni mshamba/mara ya kwanza kupanda ndege si akajidai kukauka kwenye ile security check ya kwanza pale chini (JKIA) baada ya pale akajidai anaunga moja kwa moja juu bila ku-CHECK IN kwenye kaunta ya (Precision) sasa ile tumefika juu (tunaitwa abiria tukapande ndege) anafika getini anaulizwa BOARDING PASS anaanza kuwaonyesha tiketi duuh! ilikuwa aibu aisee. Maana kipindi hicho check-in counter zishafungwa tukamuacha nafikiri alihamishiwa ndege inayofuata. USHAMBA MZIGO
 
Hana uwongo wwt..watu tumeanza kupanda ndege enzi hizo kipindi cha mwalimu..williamson diamonds mwadui walikua na ndege 4 tulikua tunapanda tu kwenda madhuleni tunashikia dar..ndege ilikua kawaida sana kama uda tu kariakoo to mwenge!

Masaa laki moja unajua ni miaka mingapi?
 
siku ya kwanza 2007 ndipo niliruka angani kwa mara ya kwanza. niliogopa kula chakula kwa kuhofia bill itakayokuja itanishinda kulipa..nilipigwa na njaa sana.. kila round wakipita nakataa. anyway ndo njia za kujifunza
 
Mimi mara yangu ya kwanza kupanda ndege nilifungua dirisha la pembeni maana kulikuwa na joto kali sana, dreva akamwambia konda wa ndege aniambie nifunge kioo.
Cc: Khantwe.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli siku ya kwanza kupanda ndege nilijikuta natabasamu tu bila sababu yoyote nadhani kipindi hicho niliongeza maisha angalau wiki moja.

Nilikuwa nasafiri kwenda Nigeria kwa Ethiopian airline . kitu cha kwanza nilimuuliza kaka yangu hali inakuwaje kwenye ndege akaniambia ni kawaida tu kwa hiyo sikuwa na hofu sana.

Kilichonisaidia na ndio system ya maisha yangu ni kwamba kama kitu sikijui na tupo wengi kamwe siwezi kuwa kimbelembele, nilipanga line katika mwa watu na nikapata karatasi mbili (boarding pass dar-addis Ababa na Addis Ababa - Lagos lakini kwa kuwa niliunga mstari sikujua kama zile ni boarding pass na sikujua zinahitajika wapi. Tulipoambiwa tukapande ndege nikaona watu wanatoa moja ya zile karatasi kwa wahudumu , Mimi bila kujua ni ipi nikampa ya Addis - Lagos yule dada akanambia kwa upole leta nyingine)

Nikaingia kwenye ndege katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa kubahatisha niliweza kufunga mkanda. Hadi leo sijui niliwezaje kufunga (kama hujawahi ni vr trick kidogo ) nikabahatika kukaa dirishani, asikwambie mtu robo tatu ya safari hadi Ethiopia nilikuwa naangalia chini kupitia dirishani.

Tukafika Addis Ababa ishu ikawa ni kwenda uelekeo upi maana Ethiopia wana uwanja mkubwa sana, kama kawaida nikamuona baba mmoja anaangalia boarding pass na akasema mmmh gate # ......nami nikaangalia yangu halafu nikafuata hadi nilipoona sehemu yenye maandishi sawa na yaliyopo kwenye boarding pass yangu.

Mara nikaingia kwenye ndege ambayo ilikuwa kubwa sana inaingia watu zaidi ya 300, nilipofika kwanza nikaona headphone na screan ndogo mbele ya seat yangu nikapepesa macho nikajua kuwa kila mtu ana ki-tv chake , nikasafiri comfortably baada ya kufika Lagos ndipo nilipongudua kuwa mwenye bahati sana maana nimepanda ndege ya kisasa kabisa duniani DREAMLINER (ET 902)
Big up Ethiopian Airline , thank you Jesus
 
Bora nyie mie rafiki yangu nimemkatalia kunipatia tiketi ya Mwanza Zanzibar kisa hakuna stand ya ndege angani pindi likifaki.
 
Njaa ipo kila kona mkuu
 
siku ya kwanza 2007 ndipo niliruka angani kwa mara ya kwanza. niliogopa kula chakula kwa kuhofia bill itakayokuja itanishinda kulipa..nilipigwa na njaa sana.. kila round wakipita nakataa. anyway ndo njia za kujifunza

Hii kali kuliko zote.
Safari ilikuwa ya masaa mangapi mkuu? Umepata swaumu bila kujipanga!
Tehtehheethtehh
 
Mara kwanza nilitoka Arusha naelekea Zanzibar nilijikuta napatwa na kizunguzungu ndani ya ndege ghafla nikawanaona giza,nachokumbuka nilichukua maji ambayo mzungu alikua ameshakunywa nikayanywa,jasho lilinitoka Sana huku mzungu ananishangaa tu,nilirudi hali ya kawaida na nikafika salama,mpaka leo nikisafiri kwa usafiri wowote sisahau maji ya kunywa.
 

Ulikumbuka ndugu zajo kuja kujuaga ndani yandege? Nahis ulitamani kuwaona machinga wakiuza korosho hewani....
 

dah!ungewapa tabu watu wa uhamiaji kugonga mihuri yao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…