Kwa kweli siku ya kwanza kupanda ndege nilijikuta natabasamu tu bila sababu yoyote nadhani kipindi hicho niliongeza maisha angalau wiki moja.
Nilikuwa nasafiri kwenda Nigeria kwa Ethiopian airline . kitu cha kwanza nilimuuliza kaka yangu hali inakuwaje kwenye ndege akaniambia ni kawaida tu kwa hiyo sikuwa na hofu sana.
Kilichonisaidia na ndio system ya maisha yangu ni kwamba kama kitu sikijui na tupo wengi kamwe siwezi kuwa kimbelembele, nilipanga line katika mwa watu na nikapata karatasi mbili (boarding pass dar-addis Ababa na Addis Ababa - Lagos lakini kwa kuwa niliunga mstari sikujua kama zile ni boarding pass na sikujua zinahitajika wapi. Tulipoambiwa tukapande ndege nikaona watu wanatoa moja ya zile karatasi kwa wahudumu , Mimi bila kujua ni ipi nikampa ya Addis - Lagos yule dada akanambia kwa upole leta nyingine)
Nikaingia kwenye ndege katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa kubahatisha niliweza kufunga mkanda. Hadi leo sijui niliwezaje kufunga (kama hujawahi ni vr trick kidogo ) nikabahatika kukaa dirishani, asikwambie mtu robo tatu ya safari hadi Ethiopia nilikuwa naangalia chini kupitia dirishani.
Tukafika Addis Ababa ishu ikawa ni kwenda uelekeo upi maana Ethiopia wana uwanja mkubwa sana, kama kawaida nikamuona baba mmoja anaangalia boarding pass na akasema mmmh gate # ......nami nikaangalia yangu halafu nikafuata hadi nilipoona sehemu yenye maandishi sawa na yaliyopo kwenye boarding pass yangu.
Mara nikaingia kwenye ndege ambayo ilikuwa kubwa sana inaingia watu zaidi ya 300, nilipofika kwanza nikaona headphone na screan ndogo mbele ya seat yangu nikapepesa macho nikajua kuwa kila mtu ana ki-tv chake , nikasafiri comfortably baada ya kufika Lagos ndipo nilipongudua kuwa mwenye bahati sana maana nimepanda ndege ya kisasa kabisa duniani DREAMLINER (ET 902)
Big up Ethiopian Airline , thank you Jesus