Tatizo wabongo tushazoea machinga wanaouzaga vitu kwenye vyombo vyetu vya usafirinilikiwa na jamaa yangu tunatoka doha kuja dar na Qatar Airways wakati tunakaribia kuondoka mhudumu akawa anagawa pipi jamaa yangu akauliza 'HOW MUCH' nilicheka mpaka jamaa alitamani anizabe makofi.
Moving walkway imenikumbusha Heathrow mwaka 2011, dah miaka inakimbia kweli!!!Mimi nilihakikisha napanda ndege zote za mashirika ya Ulaya. First trip Dar-London nilipanda KLM kwa kweli nili-enjoy sana Amsterdam kwasababu connection yangu ilikuwa kama masaa sita baadae. Then nikapanda British Airways wala siku-enjoy kwasababu unatoka London mara asubuhi unakutana na mabati yana kutu! Baadae nikapnda Swiss, aisee ile airport ya zurich ndio ilikuwa mpya,Loungee inaface runway bonge la view, then kubadili terminal moja kwenda nyingine unapanda vitreni havina dereva unabonyeza tu kinaondoka mpaka kwenye terminal yako chini kwa chini,ila shughuli nilivyopanda emirates, from London mpaka Dubai ndege kubwa nzuri mpya,kasheshe from Dubai Dar, ndege imechoka, imejaa waswahili ni kelele kama basi la mbagala,yaani pale pale dubai unajihisi tayari uko kariakoo! sasa hivi nachanga nipande ile A380
Kitu kilichonitoa ushamba ni Moving Walkway bado kidogo nidondoke Amsterdam mwaka 2000
Uchumi kakawatanzania wengi wamelala, kupanda ndege mpaka apate ofa ama alipiwe na ofisi ni wagumu mno kuchangamkia fursa nje ya nchi yao. Shame on us.
Hahahajhajaj yaani umenifanya nicheke kwa sauti afu huo mwaka na mie nilikuwa chuo...huenda tulikuwa tukipishana Kafteria ya Manzese kula RBDa! Nimecheka mpaka basi.
Mimi mara ya kwanza kupanda ndege ilikuwa 2008 Precision Air. Dar to shy naenda Nzega Resolute Mine kufanya field. Kwanza nilipopata email ya tiketi yangu sikulala siku hiyo. Nilipofika airport ndio mara ya kwanza kuona ngazi za umeme. Sikuzitumia kwa sababu ya uoga. Nilikuwa nimebeba spray1 Dawa ya mswaki, Kulikuwa na nyembe na mkasi kwenye begi vyote niliviacha airport.
Nilipokuwa ndani ya ndege haikuwa shida but kuna moment nilipata mshtuko mkubwa kidogo nipige kelele kwa sababu ya ndege kuchange altitude. Niliona kama utumbo unataka kutoka.
Kituko kingine wakati narudi Dar kutoka shy. Kwa sababu tiketi nilikatiwa na kampuni na pesa ya taxi nilishakula. Sikuwa na pesa ya taxi toka shinyanga mjini kwenda airport na nilitaka kutunza pesa nilokuwa nayo kwa sababu nilikuwa narudi chuo na Boom halieleweki linatoka lini. Ilibidi niulize nauli ya baiskelipaka airport ni sh ngapi. Shinyanga daladala ni baiskeli tu mpaka leo.
Jamaa akaniambia ni 3000 tu. So asubuhi akaniijia tukaanza safari. Balaa tukapota short kati kwenye mashamba ya mpunga. Si tukapotea? Kama si ndege kubadili arrival time ningeachwa.
Nilipofika airport wafanyakazi wa pale walinicheka baalaa. Wakasema hawajawahi ona mtu anakuja airport kupanda ndege kwa usafiri wa baiskeli.
Tiketi ya hiyo safari nimeitunza mpaka leo kama kumbukumbu toka 2008.
Hatari ndugu. Nilikuwa Geology pale mwaka wa tatu hiyo 2008.Hahahajhajaj yaani umenifanya nicheke kwa sauti afu huo mwaka na mie nilikuwa chuo...huenda tulikuwa tukipishana Kafteria ya Manzese kula RB
Ulinitangulia mwaka, mi nilikuwa mwaka wa pili ila 'Ngwine' mpaka leo sijawahi kupanda ndege...ila mwaka huu ntajitoa kimasomaso japo nikwee Fast JetHatari ndugu. Nilikuwa Geology pale mwaka wa tatu hiyo 2008.