Mimi nilihakikisha napanda ndege zote za mashirika ya Ulaya. First trip Dar-London nilipanda KLM kwa kweli nili-enjoy sana Amsterdam kwasababu connection yangu ilikuwa kama masaa sita baadae. Then nikapanda British Airways wala siku-enjoy kwasababu unatoka London mara asubuhi unakutana na mabati yana kutu! Baadae nikapnda Swiss, aisee ile airport ya zurich ndio ilikuwa mpya,Loungee inaface runway bonge la view, then kubadili terminal moja kwenda nyingine unapanda vitreni havina dereva unabonyeza tu kinaondoka mpaka kwenye terminal yako chini kwa chini,ila shughuli nilivyopanda emirates, from London mpaka Dubai ndege kubwa nzuri mpya,kasheshe from Dubai Dar, ndege imechoka, imejaa waswahili ni kelele kama basi la mbagala,yaani pale pale dubai unajihisi tayari uko kariakoo! sasa hivi nachanga nipande ile A380
Kitu kilichonitoa ushamba ni Moving Walkway bado kidogo nidondoke Amsterdam mwaka 2000