Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Yaani huu uzi siachagi kuuchungulia. Nachekaga sana comments zilizopo humu.

Mimi bado sijapanda. Ila mwaka huu naapa mbuzi aning'ate lazima nipande. Dar-kia
 
Ije ATC, Azam Airlines kule Fastjet kati Precision patakuwa hapatoshi.
 
Yaani soon JNIA kutakuwa kama Ubungo Bus Terminal. Ndege kibao (Azam, ATC, Fastjet, Community & Presisheniii). Hope wenye hela za mawazo tutakwea mipipa.
 
Lakini perfume zinakatazwa kwenye ma bag madogo (yale ambayo unaingia nayo upande wa abiri) ila ukiweka kwenye mabag makubwa ya nguo, ambayo hulipati hadi ufike, hayo unaweza na hakuna wakukuzuia.
 
Lakini perfume zinakatazwa kwenye ma bag madogo (yale ambayo unaingia nayo upande wa abiri) ila ukiweka kwenye mabag makubwa ya nguo, ambayo hulipati hadi ufike, hayo unaweza na hakuna wakukuzuia.
Zile zinazozidi ML 100 ndio unaweza kuchek in kwenye bag la chini, lakini zile zenye ML 100 and below unabeba kwenye bag lako la mkononi bila tabu
 
Du mmeniukumbusha siku natoka german
2251b0bc77b71f2b1498664e71e783ff.jpg
 
Mama yangu alikuwa hajawahi panda ndege hata mara moja so akapanga mi na mwanangu(akiwa na miezi 6)tumsindikize nairobi asafishe macho

Eeh bwana eeh ndege ilikuwa ya saa nne asubuhi lakini alinichukua kwangu saa kumi na moja asubuhi..huko njiani sasa kuelekea airport ni shida..eti tutachelewa ndege bureee

Ile tumepanda ndege tu,mwanangu akalala fofofo halafu tukatangaziwa kwamba kuna mvua huko tuendako so hali ya hewa si nzuri..sasa vile ndege inavyokuwa kama inapita kwenye makorongo,nilitamani nihame seat.mama alisali sala zote anazozijua mpaka toba eti tunakufa

Halafu mdogo wangu anasomea hayo mambo ya aviation,mama akasema kama mambo yenyewe ndo haya nampiga marufuku dogo kuendelea na hyo kozi "..eeh yesu eeh tusife leo baba ila sipandi ndege tenaa...".sahv kashasahau anataka safari ya mbali zaidi nimemwambia atafute escort mwingine mi siendi nae
Yaani humu watu wanachekesha sijawahi ona loh[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii ya kupigwa mzinga hata mie nimekutana nayo hapo JNIA 2005. Ushamba ulionipata ni kutojua kufunga mkanda, nilidhani unapita shingoni km wa gari, kumbe ni tofauti kbs. Kweli ushamba mzigo
Bora muelekeze jinsi yankufunga nasi tusije enda kuumbuka bure????[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom