Mama yangu alikuwa hajawahi panda ndege hata mara moja so akapanga mi na mwanangu(akiwa na miezi 6)tumsindikize nairobi asafishe macho
Eeh bwana eeh ndege ilikuwa ya saa nne asubuhi lakini alinichukua kwangu saa kumi na moja asubuhi..huko njiani sasa kuelekea airport ni shida..eti tutachelewa ndege bureee
Ile tumepanda ndege tu,mwanangu akalala fofofo halafu tukatangaziwa kwamba kuna mvua huko tuendako so hali ya hewa si nzuri..sasa vile ndege inavyokuwa kama inapita kwenye makorongo,nilitamani nihame seat.mama alisali sala zote anazozijua mpaka toba eti tunakufa
Halafu mdogo wangu anasomea hayo mambo ya aviation,mama akasema kama mambo yenyewe ndo haya nampiga marufuku dogo kuendelea na hyo kozi "..eeh yesu eeh tusife leo baba ila sipandi ndege tenaa...".sahv kashasahau anataka safari ya mbali zaidi nimemwambia atafute escort mwingine mi siendi nae