Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Ndege za masafa zina raha yake full ku-enjoy mamisosi, vinywaji, mazingira mapya n.k
 
Mi nilinunua Juice zangu 5 Washington DC nirudi nayo Tz kuhonga mchepuko wangu,kufika airport pale Washington Dulles Int. Airport (IAD) ukaguzi wakanizuia eti haziruhusiwi. Eti aidha nizinywe palepale au zitupwe kwenye dustbin....daaaaah,kuzinywa nikashindwa,basi wakazichukua wakazitupa.
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...
hahahahahahahahahahahahakweli ushamba mzigo
 
Ndege ina utamu wake ila usipande Ethiopia maana mizigo kama fuso
 
Wale waliozoea vya mteremko vya kula per diems kwenda kusoma basic computer course Dubai miezi 3 imekula kwao.
 
Naona awamu hii wamepania kurejesha Air Tanzania, Tunawatakia kila la heri. Ila ni ombi tu kuwa Wafanyakazi wa Serikali/wanaodhaminiwa na serikali mfano VIKUNDI VYA WANAMICHEZO/BURUDANI wanaosafiri kwa ndege/ATC kwenye Route zote zinapokwenda ndege hizi iwe LAZIMA kupanda AIR TANZANIA. Nchia za INDIA na KENYA wamefanikiwa kuwezesha mashirika yao ndege kwa namna hiyo (ya kulazimisha wafanyakazi wapande kwenye mashirika ya ndege ya taifa wanaposafiri kwa gharama za serikali.
 
First time 2004. Emirates from Dar to Atlanta USA via dubai and Gatwick. Nilisema kama ndege ndo zilivo mie basi. Na bado safari zangu zote ndani ya marekani zikawa kwa ndege. Atlanta Chicago. Chicago NY. Cleveland to cincinatti and back to atlanta. Then same route to Dar. Sikujua kama ningemuona mwanangu tena. Tangu hapo nimezipanda mara zisizohesabika. To Holland Sweden Norway UK Germany. Usafiri ule hauzoeleki kwakweli unatisha sana
 
halafu ndege inapopaa/kutua unapata kitu kama ashiki sana. daah!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…