Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)


aaaah aaah umenichekesha bt ndo kujifunza
 
mimi ni kati ya wale waumini wa SABATO MASALIA, kama mnakumbuka kisa chetu cha kutaka kupanda ndege bila kuwa na TIKITI wala PASS ya kusafiria, tungefanikiwa lile zoezi, ndyo ingekuwa ni mara yangu ya kwanza kupanda ndege!

Ahahaha mlipanic brother. Hivi Mko wapi sikuhizi?
 
Ahahaha mlipanic brother. Hivi Mko wapi sikuhizi?

kila mtu alirudi kwao, lakini tunakusanya nguvu ya kurudi pale JNIA na makundi mengine yataenda KIA na MBIA, safari hii lazima tupande mapipa. Kitu kinachotusukuma zaidi ni kupanda ndege na si kueneza injili, kuhubiri tulitumia kama cover tu!
 
nakumbuka nilipiga kelele kuhusu mizigo yangu ipo wapi sikujua kwamba nikiingia ndani kuna sehemu unasubir mizigo nilijua wameshanipiga watoto wa dar nilikuwa natoka mkoni kuja dar
 

Nimeipenda hiyo sana hahaaaa
 
Wewe wa wapi, fire, compaound, uzunguni au uhindi? Mie kw walala hoi tu MESS

kaka mwadui mining?pia nimezaliwa huko aisee..i wish to know ur real name..maana pale tulikuwa tunajuana mji mzima...
 
heri yenu ushamba mlianzia airport;Mimi siku mbili kabla nilikwenda salun kunyoa nywele,nikashuka kariakoo vuta moka ya mchina matata na shati juu suruali ilikua bado ipo poa maana ilikua ya suti yangu ya harusi

Airport kwenye line nilikua najifanya busy na simu kumbe nachungulia wenzangu wananyofanya mimi ikifika zamu yangu naunganisha tuu kumbe ushamba kibao,kila kitu najibu kwa kichwa

angani full kujikaza mpaka jasho kwenye, menu tuachie hapo ......!
 
Mmenikumbusha mtoto wangu nilisafiri nae akiwa anapanda ndege mara ya kwanza ana umri wa 5 yrs,ndege ilipokuwa juu yeye alikuwa dirishani basi alipotazama chini akaona ndege kama imesimama,basi akafungue mkanda ananiambia kwa sauti baba twende tushuke ndege imeshafika unaona imesimama,basi watu waliokuwa karibu yake walicheka sana.
 

Lamination ungeweka upande wa mbele tu
 
Hivi kwa nini kutokufahamu jambo ni ushamba?!! Kuna mtu anajua kila kitu dunia hii?!! Ndio maana watu wengi wanashindwa kuuliza kwa kuwa wanaogopa kuonekana washamba.

Mimi mara ya kwanza nakwea pipa sikupata shida kabisa maana kila kitu nilikuwa nauliza.
 
umetisha mkuu
 
ahahaaaaa
 
Ilikua ni Kama siku ya tatu fast jet kuanza kufanya safari za dar Kilimanjaro kidume nikajiyupia ndani kwa 43000 tu Kwenye begi nilikuwa na bisibisi dohh nikaambiwa hiyo Hapana mbe ikabidi nimzawadie kaka mmoja baadae nikachoma ndani ya pipa Mara dege likapaa Sio masikio kuuma Kama vile yanapasuka nikaapa mm na ndege bye bye siku hizi Kilimanjaro bus dar expres kiroho safi nani anataka kuumwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…