Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Hahaha mimi nakumbuka niliadithiwa na kuelekezwa kila kitu na nibibi yangu mama kska na dada zangu maana nilipanda utotoni sasa hii ya ukubwani nilikuwa na safiri peke yangu wakanipa darasa la kitosha tu home nimefika tu JNIA pale tuna subiri kwenye viti tuitwe si nikakumbuka niliambiwa nizime simu nikazima hata kabla hatujaingia kwenye ndege nimekuja kuwasha wakati nimeshashuka nipo kwenye tax nakuta msg kibao wananiuliza km nilishaingia tayari kwenye ndege.. ushamba ni ushamba tu hata sikuwa na wazo la kubadilisha setting za kwenye simu kutoka general or silent profile to flight mode/profile
 
Hii thread imenifanya ninekane chizi ofisini...............Humu kuna watu wana vituko sana
 
Mwaka juzi haikuwa mara yangu ya kwanza thou nilipanda na mama mmoja mkenya to USA kumbe alikuwa na ndizi kwa mkoba wake, after sometime akachukua akaila sasa hajui aweke wapi maganda ya ndizi akanigeukia nilikuwa upande wa dirishani nakusema "waweza tupa hii nje" yani nifungue dirisha nitupe maganda ga ndizi nje. Nacheka sana nikimkumbuka Yule mama
 
Mara ya kwanza kupanda ndege was 1999, mwanza - Dar, airport sikusumbuka, kasheshe kwenye ndege, sijui jinsi ya kufunga mkanda, jirani yangu ndo alinisaidia kunifundisha, akanifunga then akaufungua, akaniambia haya funga sasa, nikafunga.

Kufika Dar, sanduku silioni, baadaye naliona linazunguka kwenye ule mkanda kusogea nichukue naogopa, kweli ushamba mzigo
 
Haikuwa mara ya kwanza, coz nilishapanda sana mwz - dar au mwz - kia. Kasheshe ilikuwa ni 2006, nilikuwa naenda Nairobi, so nikapanda MWZ-JRO-NRB, ni ushamba tu wa JKIA, nilipoteaje humo ndani? siku ya kurudi nayo kidogo ndege iniache sababu ya kupotea uwanajani, nilichojifunza tu kuuliza sio ujinga vinginevyo mmh! sitasahau zile ngazi za umeme, kweli tembea uone
 
Hahahaaa, Mkuu yaani nimetoka sasa hivi kuusikiliza ila kwenye Version ambayo hadi leo bado ipo Studio.

Labda siku moja italiona jua na utaweza kuuzikiliza tena. Umenivunja mbavu. Ila ni trick ambayo Air Hostess huitumia ili kuwalaza watoto kwa kuwapa maziwa na wanachanganya na Pombe kali kidogo.
Hadi leo nikiusikia wimbo wa 'aerosmith - I don't wanna miss a thing' unanikumbusha sana ile safari...I missed everything yet siwezi kubadili kuwa ilikuwa safari yangu ya kwanza ya ndege. #sad
 
Sasa mbona hiyo ni nusu tu? Nyingine naogopa kuziandika humu ndani kwa sababu waliofanya hivyo wakisoma, wataniangukia kwa lawama. Hizi tutaongea tukikutana. Ila amini usiamini, pale Paris wameshuhudia sana vituko enzi hizo. Ni heri waliokuwa wakienda Russia maana huko mnaenda na Washamba wenzenu wa Kirusi ambao mkishaanza kunywa Vodka, mambo yanakuwa Mswano sana (harashoo).
Fundi mchundo.

Ahsante kwa kufanikiwa kunichekesha.

Hahahahahah
 
Nilisafiri na bibi kizee toka Kigoma kuja Dar, njia nzima alikuwa analalamika bora wamshushe, alilaani kitendo cha kupakiwa kwenye ndege, moja ya sentesi aliyosema ni kuwa wanawe bora wangemuua kwa sumu kuliko kumuua kwa ndege, tuliposhuka Dar baba mmoja alikuwa anamsikia akilalamika juu ya usafiri wa ndege, akamtania akamwambia bibi umesahau kanga kwenye kiti chako ndani ya ndege, akamjibu akamwambia wacha iende naweza kurudi humo ndani kuchukua nguo, wao wakaondoa ndege ghafla waanze kunizungushazungusha angani,
 
ulisema ameshapita hayo masaa laki moja, ulijuaje?
Logarithm na logbook ni vitu viwili tofauti sijui kama unafahamu Mkuu

Kwa hiyo unabisha au point yako ni nini? Log ni kifupi cha logalizm bwana log book ndio kitabu cha logalizm
 
nimecheka hadi machozi
baada ya gradu yangu
chuo.Tukarudi mkoa na maza.
Fastjet ndo imeanza.Nı mara yetu
ya kwanza wote.
1. Mama anataka kukaa akakuta juu
ya siti sehemu ya mizgo kuna mtu
kashaweka wake.Akatia,"wee
kondaa,we kondaa wéeh,hebu
njoo kwanza"
2. Nikajaribu kwenda choóni japo
sijabanwa alimradi tu nione pakoje
3.Facebuk page yangu iliomba poo.
Mara checkin in at JKİ Airport. Mara
nitupie picha alimradi kila mtu
ajue.
4. Tulivofika madreva tax wakaanza
kututukana eti "hamna lolote nyie
mtakuwa fastjet tu" hapo kisa ni
baada ya wao wanatugombania sie
hatuna time tunaenda kwny
daladala.
5. Jioni napokea simu toka kwa
mjomba: "ah mjomba nimeamini
ushamba mzigo wa
mwiba".Nkamuuliza kwanini?
Akasema,"leo sina raha. mama
yako kutwa nzima anantambia
kwny simu kisa kapanda ndege"
 
Back
Top Bottom