Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Mara ya kwanza nilipanda emirate dar-dubai-narita.

Ile kuingia tu ndan ya ndege pale dar tukapewa vitambaa vyenye kias fulan cha ubichi ili kufurta mikono. Baada ya kutambua (off course nilipiga chabo kwa jiran) ni vya kufutia mikono nusura nihifadhi mfukon nikijua ndo kimekua changu.

Nashukuru air hostess mwingine aliwahi kupita kukusanya vinginevyo ilikua aibu yangu
 
ha ha ha...wala sikumbuki siku ya kwanza ilikuwa vipi....ngoja 😛hoto:
 
Siku ya kupanda ndege sitalala. mana sijawahi kwakwel i hope sio mbal utakuwa ndo safir wangu .
 
Mimi nina kujiamini kwa asili kabisa(natural born jasiri) siku ya kwanza napanda ndege niliona kawaida tu na hata challenge ndogo nilizokutana nazo nilizichukulia kama changamoto na sio ushamba ila nilikua nahofia ajali(mpaka leo na kesho)Ila sintokaa nisahau tumepanda treni Moshi-Dar 1993 saa kumi jioni na kulikua kunanyesha mvua kubwa sana treni kila baada ya mwendo linasimama na ukiwa ndani halieleweki linarudi nyuma au linakwenda mbele sikua na amani muda wote wa safari.
 
mwaka 1999..haaikuwa mara yangu ya kwanza infact, nilienda kuiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la watoto(The World Parliament of Children-Paris), sasa ile program ilinifanya nichoke sana manake sikuwa na muda mzuri wa kupumzika mara zote tulikuwa tupo busy sana!! Sasa siku ya kurudi tumepanda Swiss Air mpaka Zurich- wakati tunasubiri connection aisee nilipiga usiingizi wa kufa mtu pale,hadi muda wa ndege umefika mi nimelala tu..wale wenzangu (wawili)wakawa wameshapanda ndege mi nakoroma pale kwenye kochi...sielewi ilikuwaje manake ndege yote bado mm tu kupanda na air hostess wameshaambiwa kwamba kuna mtu mmoja amemiss

Ikabidi ndege isiondoke wakatumwa askari wa airport kunitafuta mule ndani...nikaja kuamshwa nio na lepe la usingizi wakaniambia ndege inakusubiria...wakanipeleka hadi boarding ile naingia tu mlango ukafungwa na kila mdada ananishangaa ulikuwa wapi...!!
Kikubwa mpaka leo sijajua ile ndege kweli ikinisubiri mimi au muda wake wa kuruka ulikuwa bado haujafika.
 
baada ya gradu yangu
chuo.Tukarudi mkoa na maza.
Fastjet ndo imeanza.Nı mara yetu
ya kwanza wote.
1. Mama anataka kukaa akakuta juu
ya siti sehemu ya mizgo kuna mtu
kashaweka wake.Akatia,"wee
kondaa,we kondaa wéeh,hebu
njoo kwanza"
2. Nikajaribu kwenda choóni japo
sijabanwa alimradi tu nione pakoje
3.Facebuk page yangu iliomba poo.
Mara checkin in at JKİ Airport. Mara
nitupie picha alimradi kila mtu
ajue.
4. Tulivofika madreva tax wakaanza
kututukana eti "hamna lolote nyie
mtakuwa fastjet tu" hapo kisa ni
baada ya wao wanatugombania sie
hatuna time tunaenda kwny
daladala.
5. Jioni napokea simu toka kwa
mjomba: "ah mjomba nimeamini
ushamba mzigo wa
mwiba".Nkamuuliza kwanini?
Akasema,"leo sina raha. mama
yako kutwa nzima anantambia
kwny simu kisa kapanda ndege"
 
Naomba mwenye mdadi wa kutoa mada aturushe na sisi wa siku ya kwanza kupanda basi kwenda town....haya ya ndege sijui njiwa tunawaachia wenyewe wadosi.
 
Mimi was 2005 to USA..dah vituko vilikuwa vingi but kwa uchache nilishindwa kuflashi choo, airpot Michgan nilirukia elevator inayoshuka badala ya inayopanda nk!

Mi nilitaka kuanguka kabisa pale jomo kenyata kwani ndo nilikuwa naziona elevator kwa mara ya kwanza , sasa kitendawili ni kuzipanda kwa timing sahihi ili usije changanya madesa ...ahahahahaawadhungu ni wadhungu tu jamani.
 
Mara ya kwanza nilipanda emirate dar-dubai-narita
Ile kuingia tu ndan ya ndege pale dar tukapewa vitambaa vyenye kias fulan cha ubichi ili kufurta mikono. Baada ya kutambua (off course nilipiga chabo kwa jiran) ni vya kufutia mikono nusura nihifadhi mfukon nikijua ndo kimekua changu. Nashukuru air hostess mwingine aliwahi kupita kukusanya vinginevyo ilikua aibu yangu

Hahahah umenikumbusha mbali asee.

Ila juisi yao ya nyanya hawa jamaa sitokaa niinywe tena asilani.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Back
Top Bottom