mrsleo
JF-Expert Member
- Jan 13, 2014
- 2,588
- 3,877
Sijui kwanini nilichukulia kawaida saana
wewe ndo kama mimi, ila wakati narudi ndo nilihisi kutetemeka kidogo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijui kwanini nilichukulia kawaida saana
Siku ya kwanza kupanda ndege ilikuwa 2011, niliwahi kufika Airport nikielekea SA na Baadae Germany, Ushamba kitu kibaya sana niliachwa na ndege OR Tambo kwa kutokufuata maelekezo ya boarding gate, huwezi amini nililala Airport for one day before connecting to Frankfult
Namshukuru Mungu nimezaliwa kwenye familia yenye uwezo sana. Bibi yangu ana ndege mbalimbali, kuku, bata, kanga, kwale, njiwa etc
Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.
Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.
Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.
Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibni, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahamu yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.
Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.
Huwa napenda sana kusafiri na njuka.... naenjoy sana kuwasaidia!
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...
Mie mara ya kwanza kupanda ndege nilitoka Dsm kwenda Mwanza. Process nzima hadi niingie kwenye ndege ilikuwa 'shughuli'. Nilikaa upande wa dirishani, tulipopita Ngorongoro crater eti sikuthubutu kuchungulia nje. Kisa? Niliogopa eti nikichungulia naegemea upande mmoja hivyo nikaona kama vile ndege italalia upande ule na kuanguka! Ama kweli ushamba ni kazi!
tunataka tukusikie wewe ulivyokuwa njuka ulifanyaje!!
kuna mtu alipiga magoti Amsterdam wakati wanaunga ndege waende switz. Haya ni maneno waliokuwa karibu walimsikia akisema.
"eh baba! ushukuriwe kwa kunifikisha huku juu mbinguni baba! duniani dhiki na shida nyng baba! Mweh ndaga mwalafyale mweh"
Mbeya-Dar na fastjet mama mtu mzima kabeba na kuku kokoliko kufika airport kuku karuka huyooooo
Mbona nilishawasimulia wajukuu...au wewe hukuwepo siku hiyo??
mi siku ya kwanza kupanda ndege ilikuwa 2010 natoka dar naenda mwanza usiku kabla ya safari sikulala maana sijui ndo furaha au kimuhe muhe cha ndege. Chezeya pipa wewe.
Mimi sikumbuki mara ya kwanza ilikuwaje kwa sababu nilikuwa napandishwa ndege tangu utotoni mno.
Kitu ambacho sisahau safari moja nilikaa siti ya karibu na mama mmoja alipanda na jogoo amemuweka kwenye mfuko wa plastik kichwa kiko nje nilikaa kwa tahadhari muda wote kuangalia yule jogoo asije kunidonoa.
Duniani kuna vituko sio mchezo.kuna mtu alipiga magoti Amsterdam wakati wanaunga ndege waende switz. Haya ni maneno waliokuwa karibu walimsikia akisema.
"eh baba! ushukuriwe kwa kunifikisha huku juu mbinguni baba! duniani dhiki na shida nyng baba! Mweh ndaga mwalafyale mweh"