Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

mimi ilikua 2014 dar to mbeya. Nilikua napiga kelele kua Ticket yangu Haina City No. kumbe unapewa City No. pindi napanda.
nilipopanda nikawa nakenua meno kila mtu ananishangaa. alafu nilikua na viroba vya konyag

Seat No.
 
Hakika nimecheka sana mimi ndege nimezijulia ukubwani tena kwa msaada wa wafadhili (Msaada wa watu wa marekani) mi saa ya ndege kuondoka ndo natinga uwanjani daah!
 
Ndege tamu jamani ina utamu wake nyie achene tu aisee. tofauti na mi-YUTONG yetu ya DAR-ARUSHA ukifika kiuno chote hakifai
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...

Hahahah umenichekesha sana afu mwishoni nikakuhurumia. Pole aisee
 
My first time ilikuwa natoka Kilimanjaro napeleka wageni Mwanza 2010 July. Niliuliza wadau all about flying so sikusumbuka sana but I had to take panadol before hahahah na kwa bahati the whole year nkawa na safiri safiri sana so nshazoea now.
 
day 1 nili enjoy sanaaaa yani sanaaaa

baada ya hapo safari zilizofata ni hofu tupu as ..sipendi wakati inapoanza kuruka na wakati wa kutua. Pia hali ya hewa ikiwa mbaya safar inakuwa hovyo.

kioja changu kilikuwa kwenye pasport jamani.. nilipata ile ya muda as ilikuwa ya karatasi huyo mbio stationary kuifanyia lamination eti isiharibike. Walahi kama sio yule binti wa stationery sijui huko airport ingekuwaje ..looo!

Hahahahaha....mzee umenifumbua macho,yaani sasa hivi ndo nimegundua kwa nini hazifanyiwi lamination
 
hii thread komesha ya stress hasa hasa zile page za mwanzoni. Usipocheka basi tena....
 
Lakini sema la ukweli first experience kwenyd ndege sio mchezo.
Kund msiba flani ulitokea Arusha wa mtu wa hapa ICTR-UN sasa yule bwana alikuwa mtu wa Congo ikabidi mama mmoja local nae akaenda huko Congo kumzika jamaa.

Shida ilikuja wakati mambo tayari ndege iko kwenye run way ndo inaacha ardhi mama alishikwa na tumbo la dharura yule alipiga yowe moja kilichofwata sina kumbukumbu nacho vyema

Kwani ilibidi pilot apige turn up kwa sababu za kiafya kwani hali haikuwa muhali hata kidogo me nlijuaga watu huwa wanatapika tu

Kwenye ndege lakini yule mmama alienda some extra Miles Jamani.

Hahahahaaaaa
 
Aisee sitosahau hii siku, way back 2012. Kitu cha Dar-Paris via Zurich. Nilikuwa na mawazo kama milioni hivi, kimbembwe kwenye "connection" sasa, ilikuwa ni shida sana. Kweli huwezi kuwa mwenyeji bila kuwa mgeni.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi sikumbuki vizuri,ila nina zaidi ya masaa laki moja hewani

hizo kamba kawafunge huko kijijini kwenu iselamagasi, masaa laki 1 Tu Ni sawa na miaka 11, kwahiyo unataka kutuambia wewe umekuwa kwenye ndege miaka 11 bila kushuka tukichukulia kwa mfululizo, kwanza wewe Una umri gani, sidhani hata marubani na wale air host/cabin crew wamepaa na ndege huo muda.

na bado umetufunga umepaa zaidi ya masaa laki moja, duh we mkali. Ntaikariri ID yako

huu Ni ushamba mwingine
 
Back
Top Bottom