Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Jk mbona kapita masaa hayo? Inawzekana bana! Hivi wajua kuna watu hawajawahi panda bus as means of transport from one place/state to the other

we Jerry, unajua masaa laki moja Ni sawa na miaka 11 consecutively?, hv huyu mtu alikuwa hasomi, hafanyi kazi nyingine, au vyote hivyo vilifanyika kwenye ndege, PIA unawekuta aliyepost hivyo Ana miaka 20
 
Day one on a plane is a very funny story. For me, I was deadly scared. I was wondering what if the plane fell from the sky...
 
Minashangaa humu kila mmoja anasimulia ilivyokua day 1 kukwea pipa. Kwahiyo jf members wote walisha chenga mawingu kwa mkuyati wa Chuma!?

Ngoja nikusanye nauli nami nije kwea then niwaleteeni mrejesho
 
kuna mtu alipiga magoti Amsterdam wakati wanaunga ndege waende switz. Haya ni maneno waliokuwa karibu walimsikia akisema.
"eh baba! ushukuriwe kwa kunifikisha huku juu mbinguni baba! duniani dhiki na shida nyng baba! Mweh ndaga mwalafyale mweh"

😀😀😀😀 hahaa save my ribs pls! Umenichekesha sana
 
we Jerry, unajua masaa laki moja Ni sawa na miaka 11 consecutively?, hv huyu mtu alikuwa hasomi, hafanyi kazi nyingine, au vyote hivyo vilifanyika kwenye ndege, PIA unawekuta aliyepost hivyo Ana miaka 20

Sawa mkuu noted
 
hizo kamba kawafunge huko kijijini kwenu iselamagasi, masaa laki 1 Tu Ni sawa na miaka 11, kwahiyo unataka kutuambia wewe umekuwa kwenye ndege miaka 11 bila kushuka tukichukulia kwa mfululizo, kwanza wewe Una umri gani, sidhani hata marubani na wale air host/cabin crew wamepaa na ndege huo muda.

na bado umetufunga umepaa zaidi ya masaa laki moja, duh we mkali. Ntaikariri ID yako

huu Ni ushamba mwingine

Bora ulivyomchana anadhani Masaa laki moja ni rahisi.hata dereva tax DSM anaweza kuyafikia baada ya miaka hata 30. Piga hesabu hii:kwa siku tax driver anaendesha masaa 8 kwa mwaka 8×365days=2920hrs ×35years=102200hrs
 
mi ilikuwa issue ya kusindikizwa na wanafamilia huku nikiwa na mawazo lukuki back 2005 KLM to Amsterdam then nkachange to Michgan state kisha Massachusetts.

Sikuthubutu kuinuka kwenye siti nikishakaa hadi ndege itue mwe! Mbaya zaid nlikaa na mthungu haongei ata salamu mwanzo to mwisho wa safari wa ndege ya kwanza.
 
Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.

Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.

Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.

Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.

Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.

Daaaah hiii mbavu zimenikatikaaa teh teh teeeeee
 
nimekumbuka huu uzi ulinisaidia sana siku nasafiri na ndege for the first time as nilipitia matukio ya kila mtu na kuweka kichwani ili yasije kunitokea.

Nakumbuka niliandika natarajia kusafiri na ndege lakini sikutoa feed back nafimkiri wakati ndo sasa.
 
Mimi nakumbuka 2005 nilikuwa nasafiri kwenda USA sasa nikapanda bussiness class wenzangu wamelala taa zimezimwa mimi nakomaa tu naona noma kuomba msaada eti nisionekane mgeni nilisota wakuu yule mhudumu akanistukia akaniambia unaitaji kulaza kiti chako?


nikakubali akanisaidia lakini haikuchukuwa masaa 3 akaja kuniamsha tunatua nilijilaumu sana maana nisingeona aibu nisingechoka sana!!!
 
safari yangu ya kwanza kupanda ndege ilianzia JKNIA tar 24/5/2014 nilikua naenda Dubai na ndege ya shirika la ndege la emirates. Uzi huu ulinisaidia sana as nilitumia muda mwingi kusoma post ya kila mtu na sometimes kurudia rudia.

Nakumbuka reporting time ilikua saa kwanzia 7 mchana n nilifika on time nikaingia ndani with confidence kama sio first time, so kwenye kuingia hadi kupanda ndege sikupata shida maana sikuonyesha ugeni.

Nikaingia kwenye ndege siti niliyoandikiwa kuna babu mzungu aliomba akae na ndugu zake so akamwambia muhudumu n wakaniomba nihamie kwake then nikakubali.

nilikuja kuchemka baada ya kuwasha screen illiyo mbele ya siti then nikachomeka head phones nisikilize sound sasa bana nikawa nasikia sound tofauti na ninacho angalia mfano screen inaonyesha muvi kwenye head phones ina sound music but me nikaweka masikioni kama hakijatokea kitu.Baada ya kama masaa 3 kuna mzungu alikua pembeni yangu akawa anataka kucheki muvi ndo akawa anataka kuchomeka headphones zake ndo nikagundua me nilichomeka sehemu yake basi ikawa aibu sema nikavunga.

Kingine nilichomoa simu nicheze game as ndo pads sasa kwenye kurudisha nilipataje shida ikabidi nimuite muhudumu akaichomeka kilaini kumbe inaingia yenyewe ukiinyoosha fresh. by then tulifika salama ila sasa pale kuna watu wanaunganisha ndege nyingine ukiwafata tu unaweza potea maana Dbx airport ni kubwa sana na iko bize kuliko kawaida so nilipewa tahadhari mapema nikajitahidi pamoja na kuuliza nikatoka hadi nje nikakuta wenyeji wananisubiri.

Kikubwa kwa msafiri wa mara ya kwanza ni comfidence na kuuliza kila unapoona umeshindwa au hujui kitu flani. ukileta u much know utapotea bure
 
siku ya kurudi nilipanda ndege nikiwa na confidence zaidi. Nilipangiwa siti ya mbele ambayo mbele yangu hakukua na siti, utata nikajifanya nina ma comfidence tukapewa headphones nikawa najisiemea hawa wahudumu hawana akili wametupa headphones wakati hamna screen mbele yetu.

Zilikua mbili na za mm aza jirani nikazirudisha. Huyo maza mbongo alikua kushoto kwangu alikua ananiangalia kila ninachofanya hadi nikajuta kukaa na mbongo maana najua ukibugi kitu afu akiwa pembeni noma inakua zaidi kuliko angekua mzungu.

Baadae kuna mzungu kushoto akapress kwenye siti yake ikatokea screen duh nilishangaa sema ikabidi nivunge sina mzuka wa kucheki screen yao kumbe wapi sema as nilisharudisha headphones.

Pia kwenye kutoa kimeza flani kuwekea drinks na msosi sikuweza nikamuuliza mzungu wa jirani ndo akanisaidia.

Nadhani hivyo ndo vilinipa shida
 
Ndege mimi nimepanda ilikpokuja fastjet tena kwa msaada wa watu wa Marekani, USAID, (Dar-Mwanza)
 
duuh tushukuru fastjet kuja maana ndo imetufumbua macho tulio wengi hasa ndugu zangu wa Kanda za juu kusini (MBEYA, SUMBAWANGA, IRINGA na kule RUVUMA)
 
Mkuu unaingia wapi?, mi mwenyewe napitia huu uzi kwa umakini sana.Mungu atanisaidia oneday nikifly nisipate shida.
 
Leo nimecheka sana! kwa kweli ugeni kwenye suala lolote ni kichekesho
 
Ombea usianzie kwenye ndege za jeshi,utajuta! But saiv naona kwaida tu kwenye ndege za aibiria na jeshi pia
Umenikumbusha mbali sana mkuu, 1993 nilipopanda Buffallo ya JWTZ ilkuwa na ratiba ya kuzunguka weekly, kulikuwa na seats 6 tu, wengine mnakamata kamba na kupaa hivyo hivyo.

Kwa abiria nilipanda 2004 kwenda China nikitinga suti kali. kuingia naona wengine wako na vitisheti tu, nilijisikia sivyo...
 
Back
Top Bottom