Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.

Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.

Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.

Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.

Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.

Duh, hii ni nouma. Yaan kama ni muuza chips anakuuliza "niweke kila kitu?"
 
Pipa line rata yake Jamani asikuambie mtu. Hasa ukutane na mabrazameni na masistaduu wa Facebook Full kujishebedua picha mpaka Toilet
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...

Daaaa! Pole Mkuu.
 
Mimi siku ya kwanza itakuwa mwakani. Asanteni
 
kuna mtu alipiga magoti Amsterdam wakati wanaunga ndege waende switz. Haya ni maneno waliokuwa karibu walimsikia akisema.
"eh baba! ushukuriwe kwa kunifikisha huku juu mbinguni baba! duniani dhiki na shida nyng baba! Mweh ndaga mwalafyale mweh"

Comment zote sijacheka, ila hii. Mwisho duuuuu
 
Tuchangamkie ofa za Fastjet kabla hazijaisha. Hope hata baada ya Uongozi wa Prof. kwisha Fastjet itaendelea kutoa huduma.
 
Binafsi mara ya kwanza ilikuwa mwaka huu na fast jet.. Thank yu fast

kiukweli namshukuru Mungu ktk process zote nilikiwa mwelewa.. Sikuwa mshamba... Nilifata taratibu zote.. Na nilienda mda wa kuripoti kama ulivyotajwa.. Maana ikiwa mara ya kwanza kiukweli inabd uache swaga uheshimu muda ili nxt time uwe unajua cha kufanya


shughuli mda wa kuruka ule jamani dahhh roho ilipaaaaaaaa paaaa nadhan hii inawatokea wengi

lakini baya zaidi huko angan nikawa na mawazo mengi sana nilikiwa siamini kama tunapaa angani mithili ya kunguru khaaa


kana kwamba haitoshi safari nzima nikawa nawaza dahhhh sasa pipa likifeli hapa likadondoka itakuwaje ahahahahhaahhaahahahahahah

nilijikuta nasali safari nzima.. Dahhhhh ndege bhana

Nilishawahi safiri na mzee mmoja wa asili ya kiarabu alikua anasali safari nzima ndio wewe nini mkuu
 
Ndege siku ya kwanza unaweza kuendesha ukachafua hali ya hewa ndegeni. Chezeya Uchawi wa Mungu
 
Mkuu umeniacha hoi yaani saa wakati ndege inapaa we ndo unatia timu eapoti ha ha ha!!! hakika ulifunika mbovu. Ila wengi tumepitia huko
 
Ilikuwa mwaka 2002 toka Mza-Dsm, sikupata tabu yoyote, ila tu nilishindwa kula chakula cha "kizungu" Sandwich, tushazoea maharage na sangara. Hii mikate na majani kama mabichi ktkt ndio vitu gani, nikaona usiwe tabu, nikafunika kiboksi nikanywa soda.

Mimi hivyo vyakula vigeni kwangu sijisumbuagi hata.
 
Back
Top Bottom