Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

ndege kitu kingine aisee mimi nikiwa nasafiri kwa ndege silali siku 2 nzima nawazia safari ya dar-mwanza na fastjet. Outing weekend naendaga airport japo nifaid kwa macho tu
 
Mara ya kwanza ilikuwa FASTJET Dar- Mbeya-Dar kwa Tsh. 55,000x2 =110,000/= hatariiii sana
 
Wakuu kesho tena nakwea SOUTH AFRICA AIRWAYS nakwenda SYDNEY yaani hapa sijalala nafikria sijui itakuaje maana nasikia huko ni mbali kweli kweli, zaidi ya masaa 16 angani, daah sasa nikisikia kukata GOGO inakuaje? daah mpaka najiogopa Aisee! SHIKAMOO MZUNGU
 
Wakuu kesho tena nakwea SOUTH AFRICA AIRWAYS nakwenda SYDNEY yaani hapa sijalala nafikria sijui itakuaje maana nasikia huko ni mbali kweli kweli, zaidi ya masaa 16 angani, daah sasa nikisikia kukata GOGO inakuaje? daah mpaka najiogopa Aisee! SHIKAMOO MZUNGU

Karibu sana Sydney. Ukifika uni PM
 
Poa Mkuu nitaku-PM nakuja mkutanoni japo ngeli lenyewe la kuunga unga nitalisongesha hivyo hivyo hope wazungu watanielewa.

Daah ila sasa hii ya kukaa angani muda wote huo ndo sijielewi kwa mfano Napata tumbo la kuhara nafanyaje? maaana Dar mpaka Johannesburg nasikia masaa 3 hiyo sina shida, sasa hiyo Johannesburg -Sydney daah masaa 16 na dakika 25, ni hatari tupu.
 
Poa Mkuu nitaku-PM nakuja mkutanoni japo ngeli lenyewe la kuunga unga nitalisongesha hivyo hivyo hope wazungu watanielewa. Daah ila sasa hii ya kukaa angani muda wote huo ndo sijielewi kwa mfano Napata tumbo la kuhara nafanyaje? maaana Dar mpaka Johannesburg nasikia masaa 3 hiyo sina shida, sasa hiyo Johannesburg -Sydney daah masaa 16 na dakika 25, ni hatari tupu.

Usijali utazoea tu.
 
mkuu unawaza wapi utakimbilia wakati umebanwa na tumbo la kuhara!!!! kuna vyoo vya kutosha kwenye midege hiyo ya kwenda mbali, ila utastuka kidogo utakapokuta upo mwafrika peke yako ndege nzima, maana route ya joburg-Sydney weusi ni wachache sana.

Enjoy ur flight. Ukibanwa sana uliza jirani au wale crew.
 
ila itabidi nipige mipicha ya kumwaga mpaka huko Chooni nione kukoje maana yake daah! naona muujiza umenishukia aisee
 
Fantastic stories mine was from Dar to Cape Town so fun!
 
Nina miaka 35 sasa mtoto wa mjini ndege naiona kwa nje naishia kusindikiza wana tu.airport ila tandika_mbagala_kwa gude_kigilagila_lumo_kawe_buguruni_ilala_manzese nk wananikoma swaga zangu kama nimeshuka juzi toka ng'ambo maana navyowakusanya vilingeni na story za mbele utafurahi!!!
 
DAR ES SALAAM TOWER
THIS IS NOVEMBER 4082 YANKEE
REQEST LANDING CLEARANCE
26 SOUL ON BOARD (MARA YA KWANZA KUPANDA NDEGE).

N4082Y: RUN WAY 27
:smile-big::smile-big:

RUN WAY IN USE 27 N4082Y
 
Nyie wote chamtoto, mie nlitua jberg enroute to cape town, nkaulizia mabegi yangu wakati nilisha-chekin mpaka cape.

Halafu kurudi nikawa na mzigo wa ku-claim tax, nkachukua kitoroli cha mzigo nkaweka mabegi, nkaulizia nkaambiwa ni juu na unatumia escalator, jamaa akagoma kunisaidia kupanda nayo maana niliona kabisa kuna kubilingika, basi nkasema liwalo na liwe, nkapanda nacho kufika juu natakiwa nibonyeze chini kwenye mikono ya toroli ili brake ziachie, mwanaume nkajikuta nimengangania mwisho wa escalaror na watu wanapanda wananikaribia, kushuka sasa, nikajitoma na toroli tena nkawaza kubilingika, kuangalia watu kama vile wananicheka, nilivyofika chini kuuwa soo kwamba mshamba ikabidi nikimbize toroli sasa najifanya nimechelewa ndege, walinikoma mbona.
 
Minapita tu naona hapa maji marefu.
Nitakuja kusimulia siku nikichenga mawingu kwa mkuyati wachuma
 
Daaaah mm ilikuwa balaa maana ungo uligoma kutua tulipopata hitilafu sumbawanga na ilikuwa mishale ya alfajiri wee palikuwa hapatoshi maana ni full uchi na tumejipaka usembe usoni,sintasahau!!
 
Mimi sijui nitapanda lini pipa labda nisingizie ugonjwa nipelekwe INDIA kwa matibabu....
 
ilikuwa mwanza nimewahi balaa cjakaa sana nikamuona waziri shukuru kawambwa moyoni nikajisemea "nakaa karibu na waziri" du umefika mda nikawa nyuma yake ,kilichotokea mara baada ya kuingia sikuelewa nikaambiwa wewe huku anakoenda waziri ni first class nikajiangalia mara mbili mbili du cjui yule mhudumu ananikumbuka ? any way kwa vile anakutana na makubwa zaidi yangu...
 
Back
Top Bottom