Lokii
JF-Expert Member
- Sep 23, 2016
- 709
- 2,089
Kwa jinsi nnavyoelewa ni simple physics tu inayofanya ndege ipae, ni yale MABAWA jinsi yalivyoundwa ndo yanafanya ndege ipae, iko hivi;Hivi ni kitu gani kinafanya ndege kupaa? Maana pamoja na kusomea kumwagilia bustani JKKKT bado sijaelewa kwa nn ndege inapaa
Upande wa juu wa bawa la ndege una shape mbinuko( curved) na upande wa chini uko flat, sasa basi kutokana na ile principle ya aerodynamics au bernoulli's law hewa itakayopita upande wa juu ya bawa itakua na mgandamizo mdogo (low pressure) ukilinganisha na upande wa chini ya bawa ambapo kutakua na mgandamizo mkubwa wa hewa (high pressure).. Hii ndo inafanya ndege iweze kuelea angani
Ukiangalia hata ndege warukao angani(birds) mabawa yao yamekaa hivyo, labda wanasayansi walichukua hiyo idea kutoka huko