Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

duu wote naona hamkufanya kituko kama.changu.jamani..Mimi ilikua tarehe.27 june 2013 ilikua mara yangu ya.kwanza kabisaa kupanda ndege tena nlikua naelekea china..ilikua ethiopian bas mwenzenu niliwahi masaa 3 kabla nipo kia ndege ilikua inaondoka saa tatu usiku moja kasoro nshafika kia..mwenyeji wangu ningemkuta hukohuko china so roho ilikua mkononi jamani acheni tu..tukaenda haoo adis ababa hatimaye safari ikaanza kumbee kulikua na abiria wa Thailand so ndege ikatua Thailand nkajua ndo nshafika miye..sitakaa nsahau wengine walishuka wengine walibaki nililala hata matangazo sikuyasikia na mkanda sikuutoa yaan hata wakat inatua sikusikia..nlibanwa mkojo lakini sikuthubitu ng'oo kubanduka.nikajitosa chini kama watu wengine hapo nkawa nashangaashangaa jaman sijui nifanyeje napita huku natokea huku..najiuliza begi langu ntalipataje jamani maana nlitaka kuingia nalo ndani nkaanbiwa hapana likapelekwa sijui kwenye buti ama vip..yaani ni kichekesho jamani ushamba mtupu..nkamwona mama mmoja mweusi nkajua huyu lazima ni wa home au africa bas nkamsalimia kwa kingereza mwenzangu akanjibu nkamwambia sorry madam do you speak swahili? akanambia no please! bas nkamuuliza hapa wapi? akanambia thailand My God nikashtuka mpaka akaanza kuniuliza maswali nimetoka wapi naenda wap kufanya nn hapa na pale nkamwelezea ukweli nikiamini atanisaidia..basi ndo akaniambia inavokua akanambia baada ya lisaa safar itaendelea mpaka china so mizigo yangu nisihofu na akanambia tupo wote so nisiogope..nakuambia nilimganda kama luba hmakienda huku ninae kule ninae mpaka msalani ninae yaani acheni tu..nililia siku hiyo acha.kabisa..akaingia cafe namim nikaenda nae ndo nikamwadisia mume wangu na mwenyeji wangu yaliyonikuta yaani walinicheka na kunihurumia..nilitamani nirudie hapohapo jamani maana safar yangu ilikua ya majonzi sana..yaan na vituko vinginevingine tu ndani ya.ndege.sitaki kusimulia..yaani sitakaa nisahau..ndugu zangu heri yenu nyie mlikua wajanja angalao mie mwenzenu ndo yalonikuta.yaani nlijisemea isingekua huyo mama sijui ningefanyaje jamani..namshukuru Mungu angalao saiv nishazoeazoea.ushamba mzigo ndugu zangu acheni tu...

Pole au ndo ww ndege ikivyo anza kupaa akaanza kujikaza na kungangania kibin
 
hahaha hii thread makes me laugh jaman..daah watanzania tuna chakujivunia..amani na furaha sana..
mie nashkuru siku yangu ya kwanza ilikua 2004 nilikua na dadayangu ambae mzoefu wa pipa..so akivua viatu nami navua chap..akienda uwani namim huyoo
 
Hiyo cha mtoto ndge yangu ya kwanza kupanda ni lift ya ndege za jesh

imefka juu nina njaa hatari nkacimama kwenda kwa pilot kuomba chakula akanicmamisha mzee mmoja

mpaka natua hata embe la kumumuny

mpaka kesho ujanpandsha ndge ya jesh tena
 

[TD="class: td1, colspan: 2"] logbook (ˈlɒɡˌbʊk) [/TD]

[TD="colspan: 2"] [/TD]

[TD="class: td2, colspan: 2"]— n [/TD]

[TD="class: td3n1, width: 1%, align: right"]1. [/TD]
[TD="class: td3n2"]a book containing the official record of trips made by a ship or aircraft; log [/TD]

[TD="class: td3n1, width: 1%, align: right"]2. [/TD]
[TD="class: td3n2"]( Brit ) Compare registration document (formerly) a document listing the registration, manufacture, ownership and previous owners, etc, of a motor vehicle [/TD]

[h=2]log[/h][SUP]1 [/SUP] [lawg, log] Show IPA
noun 1. a portion or length of the trunk or of a large limb of a felled tree.

2. something inert, heavy, or not sentient.

3. Nautical . any of various devices for determining the speed of a ship, as a chip log or patent log.

4. any of various records, made in rough or finished form, concerning a trip made by a ship or aircraft and dealing with particulars of navigation, weather, engine performance, discipline, and other pertinent details; logbook.

5. Movies. an account describing or denoting each shot as it is taken, written down during production and referred to in editing the film.

cc: Wandugu Masanja

Ila uache wizi (plagiarism) its academic offence
 
Last edited by a moderator:
day 1 nili enjoy sanaaaa yani sanaaaa

baada ya hapo safari zilizofata ni hofu tupu as ..sipendi wakati inapoanza kuruka na wakati wa kutua. Pia hali ya hewa ikiwa mbaya safar inakuwa hovyo.

kioja changu kilikuwa kwenye pasport jamani.. nilipata ile ya muda as ilikuwa ya karatasi huyo mbio stationary kuifanyia lamination eti isiharibike. Walahi kama sio yule binti wa stationery sijui huko airport ingekuwaje ..looo!

Duh! hahaha
 
Unge acknowledge
By Free dictionary kwa sababu sio mawazo yako

he he he....ningekwambia logbook nini ungebisha kama ulivyombishia Masanja ndio maana nimekuwekea na tafsiri ya dictionary na inaonyesha wazi ni dictionary.....anyway sijaona kituko chako ulivyopanda ndege..... siku njema.
 
hahahahah dah hii thread ni balaa, nimecheka sana aisee
 
Nakumbuka Mara yangu ya kwanza kukwea pipa its was 2008 nikiwa chuo,baba riz alikuja mwanza wakati anaenda dsm alitupa lift.

Hiyo siku sitaisahau kwan nilianza kumlaani mkulu kwa nini alinipa lift
Wakati inatua airport nilitaman kulia kwan utumbo ulitaka kuchomoka.
 
Kwa ufupi ni kwamba panda ndege miaka nenda rudi,ndege hazizoeleki ndege zinaoogopesha zinapoyumba angani.Kuna bahadhi ya watu wana "allergy"ya kupanda ndege-hawapandi ndege kabisa.

Mimi nillipanda mwaka 1997 kwa mara ya kwanza Dar-Mwz ATC, sikuelewa kilichotokea nilishtukia tunaelea juu ya mawingu. Nakumbuka Rubani alikuwa Rubani WILILO
 
Mimi ilikuwa from Dar to Switzerland...kwenda haikua shida, ngoma wakati tunarudi kuanzia Nairobi hadi Dar!

Masikio yalikuwa yanauma hadi machozi yalitoka (wale wahudumu wanakazi ya kunambia bana pua then fanya kama unapuliza kitu pasipo fumbua mdomo, kuna hewa itatoka masikioni, kimeo tupu loh...thanks God hapana urefu hapa)
 
Huu uzi umenifanya nicheke sana peke yangu leo!!!

Mi naona ndiyo nimecheka zaidi
Hasa nikikumbuka mi ngazi za Jomo Kenyatta airport zilivyonitoa nishai, nilivyoona ngazi zinatembea nikataka kurudi nilikotoka but toka mwa huo wa 1998 mpaka leo ngazi za hivyo sizipendi kabisa!
 
  • Thanks
Reactions: ram
1992...ndege ya serikali dar to kia...ndani ya ndege hakukuwa na vituko...kasheshe ilikuwa ni baada ya kufika....yaaani nilihajikisha kila ninayepishana nae anajua kuwa nimekuja kwa ndege

Nimecheka mpaka basi!!!!!!!!!!!!!! daah!
 
baada ya gradu yangu chuo.Tukarudi mkoa na maza. Fastjet ndo imeanza.Nı mara yetu ya kwanza wote.
1. Mama anataka kukaa akakuta juu ya siti sehemu ya mizgo kuna mtu kashaweka wake.Akatia,"wee kondaa,we kondaa wéeh,hebu njoo kwanza"

2. Nikajaribu kwenda choóni japo sijabanwa alimradi tu nione pakoje

3.Facebuk page yangu iliomba poo. Mara checkin in at JKİ Airport. Mara nitupie picha alimradi kila mtu ajue.

4. Tulivofika madreva tax wakaanza kututukana eti "hamna lolote nyie mtakuwa fastjet tu" hapo kisa ni baada ya wao wanatugombania sie hatuna time tunaenda kwny daladala.

5. Jioni napokea simu toka kwa mjomba: "ah mjomba nimeamini ushamba mzigo wa mwiba".Nkamuuliza kwanini? Akasema,"leo sina raha. mama yako kutwa nzima anantambia kwny simu kisa kapanda ndege"
Umenichekesha sana ,hilo la madereva tax kulalamika kuhusuabiria wa fastjet lilishanikuta hata mimi.

Dereva tax alinikimbila akawa anawaambia wenzie "changamkieni abiria wadau imetua precisionair ,ikija fastjet tutalia ". Baadae njiani nikamuuliza dereva tax kwanini alisema vile ,akanijibu "kaka wateja wa fastjet hawapandi tax japo ni wengi kiama ,hata hao wachache wanaojitahidi kupanda - wakipanda wanatulalia sana bei ".
 
Back
Top Bottom