Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
duu wote naona hamkufanya kituko kama.changu.jamani..Mimi ilikua tarehe.27 june 2013 ilikua mara yangu ya.kwanza kabisaa kupanda ndege tena nlikua naelekea china..ilikua ethiopian bas mwenzenu niliwahi masaa 3 kabla nipo kia ndege ilikua inaondoka saa tatu usiku moja kasoro nshafika kia..mwenyeji wangu ningemkuta hukohuko china so roho ilikua mkononi jamani acheni tu..tukaenda haoo adis ababa hatimaye safari ikaanza kumbee kulikua na abiria wa Thailand so ndege ikatua Thailand nkajua ndo nshafika miye..sitakaa nsahau wengine walishuka wengine walibaki nililala hata matangazo sikuyasikia na mkanda sikuutoa yaan hata wakat inatua sikusikia..nlibanwa mkojo lakini sikuthubitu ng'oo kubanduka.nikajitosa chini kama watu wengine hapo nkawa nashangaashangaa jaman sijui nifanyeje napita huku natokea huku..najiuliza begi langu ntalipataje jamani maana nlitaka kuingia nalo ndani nkaanbiwa hapana likapelekwa sijui kwenye buti ama vip..yaani ni kichekesho jamani ushamba mtupu..nkamwona mama mmoja mweusi nkajua huyu lazima ni wa home au africa bas nkamsalimia kwa kingereza mwenzangu akanjibu nkamwambia sorry madam do you speak swahili? akanambia no please! bas nkamuuliza hapa wapi? akanambia thailand My God nikashtuka mpaka akaanza kuniuliza maswali nimetoka wapi naenda wap kufanya nn hapa na pale nkamwelezea ukweli nikiamini atanisaidia..basi ndo akaniambia inavokua akanambia baada ya lisaa safar itaendelea mpaka china so mizigo yangu nisihofu na akanambia tupo wote so nisiogope..nakuambia nilimganda kama luba hmakienda huku ninae kule ninae mpaka msalani ninae yaani acheni tu..nililia siku hiyo acha.kabisa..akaingia cafe namim nikaenda nae ndo nikamwadisia mume wangu na mwenyeji wangu yaliyonikuta yaani walinicheka na kunihurumia..nilitamani nirudie hapohapo jamani maana safar yangu ilikua ya majonzi sana..yaan na vituko vinginevingine tu ndani ya.ndege.sitaki kusimulia..yaani sitakaa nisahau..ndugu zangu heri yenu nyie mlikua wajanja angalao mie mwenzenu ndo yalonikuta.yaani nlijisemea isingekua huyo mama sijui ningefanyaje jamani..namshukuru Mungu angalao saiv nishazoeazoea.ushamba mzigo ndugu zangu acheni tu...
[TD="class: td1, colspan: 2"] logbook (ˈlɒɡˌbʊk) [/TD]
[TD="colspan: 2"] [/TD]
[TD="class: td2, colspan: 2"] n [/TD]
[TD="class: td3n1, width: 1%, align: right"]1. [/TD]
[TD="class: td3n2"]a book containing the official record of trips made by a ship or aircraft; log [/TD]
[TD="class: td3n1, width: 1%, align: right"]2. [/TD]
[TD="class: td3n2"]( Brit ) Compare registration document (formerly) a document listing the registration, manufacture, ownership and previous owners, etc, of a motor vehicle [/TD]
[h=2]log[/h][SUP]1 [/SUP] [lawg, log] Show IPA
noun 1. a portion or length of the trunk or of a large limb of a felled tree.
2. something inert, heavy, or not sentient.
3. Nautical . any of various devices for determining the speed of a ship, as a chip log or patent log.
4. any of various records, made in rough or finished form, concerning a trip made by a ship or aircraft and dealing with particulars of navigation, weather, engine performance, discipline, and other pertinent details; logbook.
5. Movies. an account describing or denoting each shot as it is taken, written down during production and referred to in editing the film.
cc: Wandugu Masanja
day 1 nili enjoy sanaaaa yani sanaaaa
baada ya hapo safari zilizofata ni hofu tupu as ..sipendi wakati inapoanza kuruka na wakati wa kutua. Pia hali ya hewa ikiwa mbaya safar inakuwa hovyo.
kioja changu kilikuwa kwenye pasport jamani.. nilipata ile ya muda as ilikuwa ya karatasi huyo mbio stationary kuifanyia lamination eti isiharibike. Walahi kama sio yule binti wa stationery sijui huko airport ingekuwaje ..looo!
Ila uache wizi (plagiarism) its academic offence
free dictionary hio....
Unge acknowledge
By Free dictionary kwa sababu sio mawazo yako
Mbeya-Dar na fastjet mama mtu mzima kabeba na kuku kokoliko kufika airport kuku karuka huyooooo
Huu uzi umenifanya nicheke sana peke yangu leo!!!
Mimi sikumbuki vizuri,ila nina zaidi ya masaa laki moja hewani
1992...ndege ya serikali dar to kia...ndani ya ndege hakukuwa na vituko...kasheshe ilikuwa ni baada ya kufika....yaaani nilihajikisha kila ninayepishana nae anajua kuwa nimekuja kwa ndege
Umenichekesha sana ,hilo la madereva tax kulalamika kuhusuabiria wa fastjet lilishanikuta hata mimi.baada ya gradu yangu chuo.Tukarudi mkoa na maza. Fastjet ndo imeanza.Nı mara yetu ya kwanza wote.
1. Mama anataka kukaa akakuta juu ya siti sehemu ya mizgo kuna mtu kashaweka wake.Akatia,"wee kondaa,we kondaa wéeh,hebu njoo kwanza"
2. Nikajaribu kwenda choóni japo sijabanwa alimradi tu nione pakoje
3.Facebuk page yangu iliomba poo. Mara checkin in at JKİ Airport. Mara nitupie picha alimradi kila mtu ajue.
4. Tulivofika madreva tax wakaanza kututukana eti "hamna lolote nyie mtakuwa fastjet tu" hapo kisa ni baada ya wao wanatugombania sie hatuna time tunaenda kwny daladala.
5. Jioni napokea simu toka kwa mjomba: "ah mjomba nimeamini ushamba mzigo wa mwiba".Nkamuuliza kwanini? Akasema,"leo sina raha. mama yako kutwa nzima anantambia kwny simu kisa kapanda ndege"