Virusi hawafi, kwanini mashine za kunyoa hazisambazi UKIMWI?

Mbona naskia HIV cha mtoto... eti kuna homa ya ini na njia za uambukizaji ni hatari kuliko HIV NA UKIMWI?
Inategemea mkuu,

Yote ni magonjwa mabaya sana.

UKIMWI inaonekana ni ugonjwa wa kawaida nw days sababu ya dawa, ila bila uwepo wa dawa usiombe kuusikia wala kuuona.
 
Ukifuatilia kiundani kabisa utakuja kugundua hiv vitu viwili ni tofaut.

UKIMWI/AIDS na HIV/VVU
Ok!! Kama huto jali unaweza tupa ufafanuzi kidogo kuhusu yafuatayo

[emoji117]Kama ni seli hai ambazo ujigeuza kupambana na ugonjwa wowote ule, mgonjwa mwenye tatizo la HIV, ukumbwa na magonjwa mengi kwa wakati mmoja ambapo anapo tibu gonjwa A basi B huzuka, ukitibu gonjwa A na B, basi gonjwa C, D na E huzuka na baadae utashangaa gonjwa A,B,C,D na E huzuka kwa pamoja na hupelekea KIFO sasa, nini kina sababisha mgonjwa kabla ya kutumia ARV akitumia dawa za kawaida kutibu magonjwa yale A,B,C,D na E haponi??

[emoji117]umetuelimisha kuhusu usambazwaji wa tatizo hili kuwa halisambazwi kwa ngono, na tatizo hili ni scam unaweza kutusaiidia sasa hawa nduguzetu waliokumbwa na tatizo hili na sasa hawapo duniani na waliopo hai, especially ambao hawatumii ARV wafanyeje sasa ili seli hai hizo zilishinde tatizo hilo???

[emoji120]
 
Nilimpoteza baba mzazi kwa huu ugonjwa kwenye miaka ya 1996 huko......baba aliumwa kweli,alikonda,alikuwa hajiwezi,alikuwa anatisha dah......above all alikufa.........huu ugonjwa kwa mtu anayesema haupo huwa namwangalia tu.......

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu,

Huyo jamaa ameongea vyema sana.

HIV/AIDS ni hatari mno.

Binafsi nilishuhudia watu wangu wa karibu wakiugulia huu ugonjwa hadi umauti. Mmoja alikuwa mke wa mwalimu wangu, watatu walikuwa majirani zangu.

Hawa niliowashuhudia walikuwa hawana tena nywele kwa kunyonyoka, miili ilikuwa imeshakwisha, walishaanza kuwa vichaa kama waokota makopo, na muda wote at late stage walikuwa wanatumia nepi mpaka umauti.

Kukaa nao ilikuwa changamoto sana, manake hata wakiwa wanaongea kuna mavitu meupe kama maziwa yalikuwa yanatoka midomoni, kiukweli ilihitaji uvumilivu.

*HIV/AIDS ina variant tofauti tofauti, ndiyo maana muathirika anatakiwa kuepuka kuendelea kuwa na wapenzi wengi.

Muathirika anaweza kutumia vyema ARV na zikafanya kazi vyema, ila wakati anatumia dawa akaendelea na ngono zembe akipata variant nyingine ambayo ni aggressive uwezekano wa dawa kumkataa ni mkubwa, na dawa zikikataa ndo kaburi hilo tena.
 
Kwanza pole sana mkuu.

Ndo maana mkwere alisema "akili za kuambiwa changanya na za kwako"

Wengi humu ni teenagers, uelewa wa haya mambo unaweza usiwe mkubwa kiivyo.
 
iko hivi, kama ushawahi kuuguza mgonjwa mwenye hili tatizo, uwezi kusmama kuongea wanachonongea hawa!! Especially awe ndugu yako wa karibu, tena awe ni ile type ya wanao kataaa kuikubali hali yaanj hataki kusikia habari ya ARV na anaamini labda kalogwa!!

Aiseee!! Achani nyie
 
Kirusi ana uwezo wa kuitwa living thing pia non living thing kwa sababu, kwanza anaitwa non living thing kutokana Hana sifa za kiumbe hai ambazo zipo Saba zinazo mtambulisha kiumbe hai
1) Reproduction
2) Growth
3) Response to stimuli
4) Homeostasis
5) Organization
6) Metabolism
7) Adaptation
Kwa hiyo sasa ukiangalia hizo sifa Kirusi Hana kwa sababu hawezi kujizalisha, kukua (sio kuongezeka idadi), Hana mpangilio unamtambulisha kama seli Zaidi ya kuwa na genetic material DNA or RNA pamoja na cell wall, Hana uwezo wa kuzalisha nishati ili Kuweza kuendesha shughuli zake, Hana uwezo wa kurekebisha mazingira yake ya ndani ili kuendana na mazingira pia uwezo wa kuendana na mazingira yanayomzunguka.
Hizi ndio sababu Kirusi huitwa non living thing kwa sababu yeye kama yeye Hana hizo sifa.
Sasa ili aweze kuitwa living thing Kirusi huwa anatumia kiumbe kingine
Mfano seli nyeupe za damu ili kupata sifa husika, hutumia seli husika kujizalisha, kujiongeza kwa idadi, kutengeneza nishati n.k
Sasa tukirudi kwanini HIV haimbukizi kupitia kupitia mashine za kunyoa,
Kitu Cha kwanza kujua ni kwamba inawezekana kuambukizwa HIV kupitia kwenye mashine za kunyolea ila kuna sababu kadhaa zinazopunguza uwezekano huo na uwezo wa Kirusi kuishi nje ya mwili na kuambukiza.
1)Aina na kiasi Cha maji maji yaliopo, kwa kiasi kikubwa Kirusi huishi katika damu, majimaji kwenye mbegu za kiume, majimaji ya ukeni pia hata kwenye maziwa ya mama.
Kwa hiyo ili Kirusi kiweze kuambukizwa ni lazima mtu awe amekatwa na kutoa damu ya kutosha ili kuweza kumfanya Kirusi aweze kuendelea kuishi nje ya mwili.
2) Joto na unyevu unyevu wa sehemu husika.
3) Hali ya PH au acidity ya mazingira husika.
4) Uwepo wa jua katika sehemu husika.
Vitu hivi vikiwa havipo kulingana na Kirusi anavyotaka Kirusi husika hupoteza uwezo wake wa kuambukiza na baadae kufa.
Ndio maana kuna sterilization katika ma hospitali, lengo kuu ni kuua vidudu husika ikiwemo virusi.
N.B HIV ipo na inaua tujikinge na kuendelea kujielimisha.

Natumai nimeeleweka watu wengine watajazia zaidi...
 
Vijana wanakwambia UKIMWI ni hoax.
 
HIV anaweza asiambukize kupitia Mashine kwasababu nilisikiaga kwa Mtaalamu mmoja kuwa Mashine huwa inapata Moto wakati inatumika. Ule Moto unaweza ukamuua Kirusi(HIV).
 
Sahihi mkuu
Ndio maana utasikia kuna ukimwi wa dar, iringa, njombe nk. Huo wa. Iringa unaambiwa ni toleo la kwanza kbsa ambalo dada wa ndani yaani House girls walirudi nao huku kwetu. Ni noma.
 
Kwanza pole sana mkuu.

Ndo maana mkwere alisema "akili za kuambiwa changanya na za kwako"

Wengi humu ni teenagers, uelewa wa haya mambo unaweza usiwe mkubwa kiivyo.
Asante mkuu....waombe Mungu awaepushe na hii kitu......hata Sasa mtu kuishi kwa zile arvs ni changamoto sana.......Kama upo salama shukuru Mungu,jilinde

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Naomba mwenye picha za wagonjwa wa miaka hiyo atuwekee tuwakumbushe vijana..
 
Dah! Aisee wewe Muobgo hataree lait ningekuwa karbu yako unaniambia huo Upuuz wako ningekupiga Kofi.
Nipo kitengo cha Arv hapa Hospitaal.....
Nawahudumia wagonjwa wa ukimwi kwa kuwapa ARV NA sometime kutoa huduma ya kuwatembelea Majumban kwao kuona uhalisia wa hali zao za Afya zikoje.

Sasa wewe Njoo nikugonge Sindano yenye Virus vya HIV kisha ule Lishe nzur ya chakula na kufanya mazoezi bila kula dawa ili tuone kama Ukimwi (Upungufu wa Kinga Mwilini) utaondoka mwilini wako.

Acha kudanganya watu bhana watu wamepoteza Ndugu, Jamaa na Marafiki kwasababu ya huu Ugonjwa halagu wewe unauita Hoax/Scam!

are you serious Kijan???
 
Daah Mungu atusaidie sana,

mimi juzi kati nilikutana na mwanamke..ana mshepu yuko vizuri tako kule..., nikamuomba kupima akadai leo tutumie kondom tutapima next week.

Kweli mzee nikapiga na kondom, tukiwa katikati ya tendo..kondom ikachomoka. Nikachomoa fasta..nikavaa nyingine. Tukaendelea kama dakika 3 nikapiz.

Tukaenda kuoga ,tulivyorudi...nikaanza kumbembeleza kupima..akakubali..nikachukua vipimo kuja kupima...yeye ikasoma mistari miwili na mm mmoja. Daaah hadi sasa sina amani kabisa.

Ingawa nimeshapima mara mbili niko negative. Nimeambiwa nirudie baada ya mwezi mmoja. Nipo kusikilizia mana PEP waliniambia nimechelewa.
 
Kirusi kinakufa vizur fu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…