Virusi vya corona: Anna Mghwira atangaza malori ya Kenya kutovuka mpaka wa Tanzania wa Holili

Hii njia tunayotaka kupita ni mbaya sana, Kuna watu wanafurahia ugomvi huu, tusimpe sababu mtu mweupe wa kuingilia mambo yetu kwa kumtumia Kenya, Kenya hapa anatumika tukisema tufuate mwisho tunaumia sote afu mzungu anapata upenyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Here we go again, Waafrika kufanya upumbavu na kusingizia wazungu wqnawahujumu, wazungu wenyewe Wana Mambo yao Huko, wala hawana muda na nyie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bifu la zama zile za mahindi, vifaranga, ng'ombe limerudi.Kenyatta anatafuta ligi kiwandani.
 
Kenya watajilaumu sana cz kuna mambo yatawagharimu....njaa haina mbabe mkuu..pesa huwezi itafuna
 
Safii, excellent move, not everyday sisi tunaonekana wapole tu tuonyeshe na sisi tunaweza kuwazuia hata raia wa nchi nyingine kuingia Tanzania

Jitahidi uje ugeuze maneno maana Ummy kukanusha hatua hiyo.
 
Lipi jema mkuu? Tukubali kuburuzwa huku tukibembeleza ujirani?
 
Haya kuna hii tena nayo kanusheni.


=======
RC MGHWIRA AWASHAURI MADEREVA WA TANZANIA KUTOTUMIA MPAKA WA HOLILI KWENDA KENYA

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kama Kenya wamefunga mpaka wakidai Tanzania kuna #CoronaVirus basi wasije nchini na kuwaambia kuwa watafanya biashara kidijitali

Ameamua hivyo kutokana na kushangazwa na kitendo cha Kenya kufunga mpaka wao wakati kipindi wao wana wagonjwa wa Corona na Tanzania hakuna, Tanzania haikufunga mpaka wake

Aidha, kutokana na hilo amewashauri madereva wa magari ya mizigo kutoka Tanzania kutotumia mpaka wa Holili mkoani humo kwenda Kenya maana kule hakuna #COVID19 ila Tanzania ndio ipo

Amesema madereva hao wasiende kusambaza #Corona kule na pia amewashauri madereva wa mizigo wa Kenya wasije Tanzania ili kuepuka kupata Maambukizi ya ugonjwa huo

Amesema madereva wa Kenya wamemuomba sana kuja nchini kufanya biashara ile yeye amewaambia wachague kati ya kufanya biashara au kufa kwa Corona

Amesema mizigo kutoka Kenya itolewe taarifa haraka ili ijulikane lini inafika mpakani Holili na ikifika hapo zitafanyika jitihada za kuhamisha mizigo hiyo bila madereva kuvuka mpaka wala kugusana ikiwezekana mashine ‘crain’ itatumika
 
Katika muongozo mpya unaolenga malori ya mizigo ya mataifa mengine yanayoingia na kutoka nchini humo, Mkuu huyo wa mkoa amesema kwamba masharti hayo mapya yanalenga kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

''Malori yote yanayobeba mizigo na yanayomilikiwa na raia wa Tanzania, na yangependelea kuingia Tanzania ama yanamilikiwa na raia mwingine wa kigeni lakini bidhaa hiyo iliagizwa na Mtanzania , tafuta lori jingine ili kusafirisha mizigo hiyo inakoelekea.''

Malori kutoka mataifa mengine hayataruhusiwa kuingia'', alisema. Bi Mghwira

Amesema kwamba serikali ya Tanzania haitakubali mazingira ya kibiashara kuwekwa katika hali ya ambayo haihusiani na ambayo inaleta utata mkubwa. 'Tusiendelee kuharibiana biashara na kuweka mazingira ya kiabiashara katika hali ambayo inaleta utata'. Alisema Bi.Mghwira

Bi Mghwira hususan alizungumzia kuhusu malori ya mizigo kutoka Kenya baada ya tangazo la rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumamosi kwamba amefunga mpaka na Tanzania pamoja na Somalia kwa madai kwamba maambukizi mapya nchini Kenya yanapitia mpaka wa Holili.

Maelekezo hayo ya Mghwira yamechukuliwa katika mkanda wa video ambao umesambaa mitandaoni nchini Kenya na Tanzania. Mkuu huyo wa mkoa ameithibitishia BBC kuwa ni kweli ametoa maelekezo hayo.

Hata hivyo, mapema hii leo Rais Magufuli amesisitiza kuwa Tanzania haitafunga mipaka yake na nchi jirani.

Kenya ilifunga mpaka wake na Tanzania pamoja na Somalia kwa muda wa siku 30 kuanzia saa sita usiku wa Jumamosi Mei 16.


BBC Swahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…