Katika muongozo mpya unaolenga malori ya mizigo ya mataifa mengine yanayoingia na kutoka nchini humo, Mkuu huyo wa mkoa amesema kwamba masharti hayo mapya yanalenga kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.
''Malori yote yanayobeba mizigo na yanayomilikiwa na raia wa Tanzania, na yangependelea kuingia Tanzania ama yanamilikiwa na raia mwingine wa kigeni lakini bidhaa hiyo iliagizwa na Mtanzania , tafuta lori jingine ili kusafirisha mizigo hiyo inakoelekea.''
Malori kutoka mataifa mengine hayataruhusiwa kuingia'', alisema. Bi Mghwira
Amesema kwamba serikali ya Tanzania haitakubali mazingira ya kibiashara kuwekwa katika hali ya ambayo haihusiani na ambayo inaleta utata mkubwa. 'Tusiendelee kuharibiana biashara na kuweka mazingira ya kiabiashara katika hali ambayo inaleta utata'. Alisema Bi.Mghwira
Bi Mghwira hususan alizungumzia kuhusu malori ya mizigo kutoka Kenya baada ya tangazo la rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumamosi kwamba amefunga mpaka na Tanzania pamoja na Somalia kwa madai kwamba maambukizi mapya nchini Kenya yanapitia mpaka wa Holili.
Maelekezo hayo ya Mghwira yamechukuliwa katika mkanda wa video ambao umesambaa mitandaoni nchini Kenya na Tanzania. Mkuu huyo wa mkoa ameithibitishia BBC kuwa ni kweli ametoa maelekezo hayo.
Hata hivyo, mapema hii leo Rais Magufuli amesisitiza kuwa Tanzania haitafunga mipaka yake na nchi jirani.
Kenya ilifunga mpaka wake na Tanzania pamoja na Somalia kwa muda wa siku 30 kuanzia saa sita usiku wa Jumamosi Mei 16.
BBC Swahili