1)
Miaka mingi iliopita nikiwa kijana mdogo. Niliondoka na gari la mizigo linalotoka Dar kuelekea Mwanza, tulipita njia ya Arushabkwankuw njia ya Morogoro Dodoma uilikua haipitiki, kama sijakosea jina, "magole" palikua pamefurika hapapitiki.
Tukaenda salama Arusha na kuondoka kuelekea Singida kupitia Dareda - Katesh - Singida. Enzi hizo ilikua bado ni barabara ya tope, haina hata kipande cha lami.
Cha kuvutia ilikua ni kila aina ya wanyama tuliokutana na kupishana nao njiani.
Cha kuvutia zaidi ni wenyeji wa barabrara Hiyo, wengine,hususan wa kiume, walikua hawavai nguo kabisa na tayari wana umri wa ujana, licha ya watoto. Baadhi ya wanawake walikua na kipande cha ngozi tu kinachoficha tupu zao kwa mbele. Kwa nyuma ilikua ni holela.
Tukafika Singida salama lakini hoi bin taabani. Mtu niliefatana nae alikua ni mwenyeji singida na tukaenda kwa Dada yake, tukapokewa vizuri sana tukachinjiwa kuku na kwa wali wa mafuta.
Ilikua ni Mara yangu ya kwanza kuona kuku mkubwa namna hiyo. Mguu na paja tu niling'ang'ana kuumaliza.
Siku ya pili tukaondoka Singida, kwa bahati mbaya kabisa kabla ya kufika Sekenge gari likap9nduka kiubavu, dereva alilip8tisha pembeni ya barabara kumbe lilikua ni tope tupu lililokauka juu tu.
Gari ikalala ubavu, mwenzangu akaumia mkono, ingaws hakuumia sana lakini ilibidi tumpeleke hospitali kwani alilia sana kwa maumivu.
Wenyeji wakatwambia hospitali ya karibu ni Kiomboi, tukapata gari (landrover) tukaikod8 ikatupelekea kiomboi. Moja kwa moja hospitali, wakamtazama na kumpiga sindano za maumivu, bahati alikua hajavunjika. Tukalala Kiomboi.
siku ya pili
tukaenda tukayanyua gari na mwenzangu akaondoka nalo, lilikua halijaumia kiasi cha kutokutembea wenyewe.
Mimi ikabidi nipande land-rover, kufika kimji kimoja kabla ya Sekenge nadhani panaitwa "Msisi" au "kwa Msisi", kama sijasahau. Hapo ikabidi tulale, Sekenge, njia ya zamani, mpya ilikua bado, wamezuia hakuna gari kupita.
Bahati nikapata gesti ya kupunguza machovu, kwenye hiyo gesticulating kulikua na mwanamke wa kizungu, alikua mkubwa kwangu lakini ni kijana, ni mtu wa ma adventure, alikua ni Mjerumani alitoka Kiomboi na yeye amekwama hapo kwa Msisi. Tukajuana na kupiga stori,na yeye alikua anaelekea Mwanza. Tukaunganisha tukawa safari moja.
Siku ya pili tukapata lifti ya gari la mizigo linaenda Nzega. Tukawa safari moja. Hapo Nzega ikabidi tulale. To make the long story short, hapo Nzega ndio nilikula ngoma ya kwanzà ya kizungu, bila kuitongoza wala kuiambia chochote kuhusiana na mapenzi.