Visa vya matapeli na watoto wa mjini

Lakini si mbaya ulipata sabuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuelewa hyo route ilikua ndefu sema kwa vile ulikua unamsindikiza jamaa asije akaona una mind kisa kapata mlupo
 
Hawa wassenge nimewavulia kofia!
Kuna jamaa yetu fala sana !Alitapeliwa na jamaa wa kujiita freemason!...
Ni hivi jamaa yetu alikua yuko vizuri sana sasa kuna siku freemason feki wakaja ofisini kwake(anauza mbao)na bonge la ndinga!Kufika wanataka mbao wakauziana pale then wakaachiana contacts(hapa ndio mission inaaza)Huku na kule wanawasiliana wakamwambia je unapenda kufanikiwa zaidi,jamaa kasema ndio.wakapanga miadi siku mamason wanafika wakamwambia sisi ni member wa freemason ndio maana tuna mafanikio tele so na wewe kama unataka tutakufikishia ombi lako kwa mkuu wetu wakapamtia 10m cash kwamba ndio wanamkaribisha ila hadi wapate kibali kwa mkuu!Jamaa yetu kuona zile m10(hapa walimtibua vuzzi) akajua hawa ndio mason wenyewe kumbe bwege anapigwa!Siku ya siku wakaja wakamwambia ombi lako limejibiwa vizuri tena ila bank una Tsh ngapi coz inatakiwa tukachanganye hela zote ndio ijulikane utaongezewa kiasi gani .Jamaa karopoka ana m70 ,wakamwambia aongeze zifike m100 ili zikienda kuchanganywa apate 1billion!!!Hapa jamaa hakupoteza mda akaenda kudro mpunga wote na kuuza nyumba ndani ya siku mbili jamaa wakaja kuchukua mpunga wao jamaa akitegemea bilioni moja!Toka siku ile hawajawai kupatkana kwenye simu na jamaa kawa pumb.u no mia!!!
 
HEAVY
 
Asee HEAVY
 
Simu yako inatoka betri miaka hii.!
No offense bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mambo ya Rohypnol HEAVY
 
Miaka ya 2000 mwanzoni tuliwahi kulizwa na wazee wa kazi.

Mzee alikuwa ana duka la kuuza baiskeli na spea zake. Basi siku ya siku jamaa wakaja wakamkuta mzee wakamwomba kama anazo shilingi moja moja awatafutie watazinunua 1 kwa sh 20, mzee akazisaka mule dukani akapata kadhaa, maana kipindi hicho zilishaacha kutumika.

Wakazinunua akapata kama 15,000/-, basi wakamwambia awakusanyie watakuwa siku fulani, walipokuja walikuta kakusanya nyingi kidogo, wakanunua, alipata kama 250,000/-.

Mzee akaambiwa akusanye zaidi maana kuna wazungu ambao wanazihitaji sana, wanataka mzigo mkubwa, kwamba kuna vito wanatumia kutengenezea.

Basi kwenye kutafuta mzee akakutana na mtu ambaye alisema anazo ila anauza kwa bei ya sh 10 kila moja maana dili limeshajulikana kwamba anauza kwa 20. Akanunua mzigo wa almost 900,000/-, maana kuna shamba aliuza kuongezea hela. Hapo alitegemea faida mara 2.

Jamaa hawakurudi tena, ikaja baadae kugundulika wale jamaa waliomuuzia mzigo wa mwisho ndiyo hao hao walionunua kwake mwanzoni.
 
Kuna jamaa mmoja Tapeli mbobevu kuna siku nikipewa story full nitaweka story yake hapa.

Ila in short jamaa yupo kituo kukubwa cha polisi maeneo ya mbezi as we speak. Katapeli Morogoro, Iringa anatafutwa na Sinza katapeli gari kama 6 hivi.

Mwenye access afatilie kesi ya huyu jamaa nimesikia ipo Gogoni hapo Mbezi. Mshana Jr

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Duuh serious??????[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji48][emoji119][emoji119][emoji119] mamaeee hao jamaa fundi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…