Kuna jamaa yangu kipindi hicho ndiyo kaja Dar, bado mgeni mgeni. Sasa akaenda Kariakoo day moja hivi...
Jioni jioni kakuta machinga wamepanga nguo (t-shirts) chini, wanauza. Zimefungwa kwenye makaratasi yale ya upya upya. Sasa jamaa yangu huyu ikabidi aulize kuwa wanauza kiasi gani?
Akaambiwa kila tisheti pale ni elfu 5. Si akaona bei ya kutapa na nguo ni classic. Akajaa, akazinunua 3 za elfu kumi na 5....akijua kwa bei ile amewapiga wao.
Bwana bwana...ile amefika home kaanza kutusimulia kuwa amenunua nguo nzuri kwa bei rahisi kweli. Ile kuzifungua....ha ha ha ha....ni yale ma tisheti makuuubwa oversize ya mitumba. Yamechoka mbaya, na ukilivaa unakuwa kama kituko flani.
Ikabidi moja tuligeuze dekio, moja kanyagio la mlangoni. Ha ha ha....mjini shule, tena shule hasa.