Uchawi ni nini?
Unajuaje huu uchawi na hiki ni kitu tu hujakijua lakini si uchawi?
Mfano, mtu ambaye haujui mchezo wa karata tatu, akioneshwa mchezo huo kwa mara ya kwanza, anaweza kuamini ni uchawi.
Au, tukimchukua babu wa babu wa babu wa babu yako aliyezaliwa miaka zaidi ya 140 iliyopita, ukamleta leo aone watu wanavyowasiliana kwa simu, ataona kama uchawi, wakati si uchawi, ni teknolojia tu ambayo hajaijua.
Sasa wewe hicho unachokiita uchawi unajuaje ni uchawi kweli na si karata tatu au kitu kingine usichokijua?