Mapema mwezi Disemba mwaka uliopita 2022,waziri mkuu alizindua ugawaji wa Vishkwambi Dodoma kwa walimu wote nchini ili vikatumike kufundishia mashuleni.
Ugawaji wa vifaa hivi ulishaanza na bado unaendelea katika Halmashauri zetu kupitia idara ya Uthibiti ubora(zamani ukaguzi). Cha ajabu badala ya kugawa kwa walimu wote Kama Waziri mkuu alivyoelekeza umetoka mwongozo unaelekeza walimu wa vitengo pekee kupewa vifaa hivyo.
Nimefuatilia kwa ukaribu Halmashauri mbili Mbozi na Mpanda wanagawa Vishkwambi 7 kwa kila shule. Ukiangalia wastani idadi ya walimu kwa shule kwa mfano ni zaidi ya walimu 12, Kwa hesabu hiyo maana yake walimu wengi hawatapata vifaa hivyo. Sasa najiuliza Vishkwambi hivyo VIMEYEYUKIA WAPI?
Nilikuwa najaribu kuiweka video ya kauri ya waziri mkuu Kama rejea, akizindua zoezi lenyewe lakini imegoma. Ila ujumbe wangu umefika.
Sent from my Infinix X650B using
JamiiForums mobile app