Visomo (Dua) Sita Zizofanywa na TANU Mwalimu Nyerere Akishiriki Wakati wa Kupigania Uhuru 1954 - 1961

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
"Nimevutiwa na hiki kipengele nimejikuta napata swali pia.

Lakini pia katika hutuba yake ya kuagana na wazee wa Dar 1985, alieleza kwa ufasaha jinsi wenyeji wa Dar (moslems in particular) walivyochangia katika harakati za uhuru.

Alikwenda mbali akaeleza mpaka baadhi ya MATAMBIKO waliyofanya wazee wa KIISLAMU akiwa peke yake wa imani tofauti.

Ninaomba kupata ufafanuzi je kuna uhusiano wa MATAMBIKO na Uislamu?

VISOMO SITA ALIVYOFANYIWA JULIUS NYERERE NA WANACHAMA WENGINE WA TANU WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA 1954 - 1961

Mtegite,
Bahati mbaya sana Mwalimu Nyerere kuna mambo yawezekana hakuwa anayajua au labda hakupenda kuyazungumza.

Kwanza ni kuwa kile kilichofanywa kwa Jumbe Tambaza si tambiko ni dua.

Mahali wanapokutana masheikh inafanyika dua na dua ziko katika Qur'an.

Hawakutani masheikh kutambika.

Dua inaweza kufuatia na kuchinja mnyama.

Mwalimu Nyerere hakuwa wa kwanza katika kufanyiwa dua ndani ya TANU.

Mwanachama wa kwanza wa TANU kufanyiwa dua alikuwa Abdul Sykes ambae mwaka wa 1954 alikutwa na kadi za TANU ndani ya ofisi yake akiwa Market Master, Soko la Kariakoo.

Kisa kirefu lakini ilihofiwa atafukuzwa kazi.

Ikafanywa dua na akachinjwa kondoo.

Mwanachama wa pili alikuwa Rashid Ali Meli.

Huyu alikuwa Bwana Fedha wa Dar es Salaam Municipal Council.

Rashid Ali Meli alitoa fedha za Municipal akampa Iddi Faiz Mafungo atie kwenye mfuko wa safari ya Nyerere UNO awahi kusafiri lakini zirudishwe haraka.

Baada ya kutoa fedha zile siku ya pili Wakaguzi wakafika ofisini kwake kumkagua.

TANU ikamfanyia dua kuomba msaada wa Allah Rashid Ali Meli anusurike.

Dua ya tatu ilifanyika ofisi ya TANU Mtaa wa Jaribu nyumbani kwa Ali Msham kuomba safari ya salama kwa Mwalimu Nyerere aliyekuwa anakwenda UNO safari ya kwanza 1955.

Mwalimu alifanyiwa dua ya nne Lindi mwaka wa 1956 na Sheikh Mohamed Yusuf Badi nyumbani kwa Suleiman Masudi Mnonji.

Dua ya tano Mwalimu alifanyiwa Mnyanjani kutafuta uelewano baina ya wana TANU katika msuguano wa Kura Tatu mwaka 1958.

Hivi ndivyo visomo vitano na ukiongeza na kile alichoeleza Mwalimu Nyerere jumla vinakuwa visomo sita.

Hapakuwa na matambiko.

1672953489856.png

Dua ofisi ya TANU Mtaa wa Jaribu Magomeni nyumbani kwa Ali Msham kuomba salama ya safari ya Mwalimu Nyerere UNO 1955.
 
Wakati huo wanaopiga kelele sasa hivi walikuwa house niggers waliokuwa wakila keki ya mkoloni na kumsifia na kumuunga mkono.
 
"Nimevutiwa na hiki kipengele nimejikuta napata swali pia.

Lakini pia katika hutuba yake ya kuagana na wazee wa Dar 1985, alieleza kwa ufasaha jinsi wenyeji wa Dar (moslems in particular) walivyochangia katika harakati za uhuru.

Alikwenda mbali akaeleza mpaka baadhi ya MATAMBIKO waliyofanya wazee wa KIISLAMU akiwa peke yake wa imani tofauti.

Ninaomba kupata ufafanuzi je kuna uhusiano wa MATAMBIKO na Uislamu?

VISOMO SITA ALIVYOFANYIWA JULIUS NYERERE NA WANACHAMA WENGINE WA TANU WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA 1954 - 1961

Mtegite,
Bahati mbaya sana Mwalimu Nyerere kuna mambo yawezekana hakuwa anayajua au labda hakupenda kuyazungumza.

Kwanza ni kuwa kile kilichofanywa kwa Jumbe Tambaza si tambiko ni dua.

Mahali wanapokutana masheikh inafanyika dua na dua ziko katika Qur'an.

Hawakutani masheikh kutambika.
Dua inaweza kufuatia na kuchinja mnyama.

Mwalimu Nyerere hakuwa wa kwanza katika kufanyiwa dua ndani ya TANU.

Mwanachama wa kwanza wa TANU kufanyiwa dua alikuwa Abdul Sykes ambae mwaka wa 1954 alikutwa na kadi za TANU ndani ya.ofisi yake akiwa Market Master, Soko la Kariakoo.

Kisa kirefu lakini ilihofiwa atafukuzwa kazi.
Ikafanywa dua na akachinjwa kondoo.

Mwanachama wa pili alikuwa Rashid Ali Meli.

Huyu alikuwa Bwana Fedha wa Dar es Salaam Municipal Council.

Rashid Ali Meli alitoa fedha za Municipal akampa Iddi Faiz Mafungo atie kwenye mfuko wa safari ya Nyerere UNO awahi kusafiri lakini zirudishwe haraka.

Baada ya kutoa fedha zile siku ya pili Wakaguzi wakafika ofisini kwake kumkagua.

TANU ikamfanyia dua kuomba msaada wa Allah Rashid Ali Meli anusurike.

Dua ya tatu ilifanyika ofisi ya TANU Mtaa wa Jaribu nyumbani kwa Ali Msham kuomba safari ya salama kwa Mwalimu Nyerere aliyekuwa anakwenda UNO safari ya kwanza 1955.

Mwalimu alifanyiwa dua ya nne Lindi mwaka wa 1956 na Sheikh Mohamed Yusuf Badi nyumbani kwa Suleiman Masudi Mnonji.

Dua ya tano Mwalimu alifanyiwa Mnyanjani kutafuta uelewano baina ya wana TANU katika msuguano wa Kura Tatu mwaka 1958.

Hivi ndivyo visomo vitano na ukiongeza na kile alichoeleza Mwalimu Nyerere jumla vinakuwa visomo sita.

Hapakuwa na matambiko.

View attachment 2470365
Dua ofisi ya TANU Mtaa wa Jaribu Magomeni nyumbani kwa Ali Msham kuomba salama ya safari ya Mwalimu Nyerere UNO 1955.
Swadakta. Pia naomba utuletee historia ya Mwanazuoni NGULI Forojo Ganze (Master)
 
Mzee unajichanganya. Tambiko ni sadaka ya kuchinda kwa nguvu ya ziada tunayoiamini iwe ni Mungu, Alla, mizimu, majini nk. Ibada dua, maombi au kisomo kinachoambatana na kuchinja au kuua kiumbe chenye damu ni TAMBIKO. Masheikh walitambika na wala sio kitu kibaya. Hata manabii na mitume wa Mwenyeez Mungu walitambika kama hao unaowaita waganga wa kienyeji.
 
Asante kwa historia, tunaendelea kujifunza kupitia maandiko yako hasa tunaopenda kujua tulikotoka
 
Dua alizofanyiwa Bagamoyo ungejua wote walioshiriki ...Familia ya Sheikh Ramiya alikuwepo Sheikh Yahya Hussein inasemekana na ndo chanzo cha yeye Sheikh Yahya kuwa na umaarufu baadae akipewa vibali Hadi vya kusafiri nje kirahisi
The Boss,
Mashaallah.
 
Mzee unajichanganya. Tambiko ni sadaka ya kuchinda kwa nguvu ya ziada tunayoiamini iwe ni Mungu, Alla, mizimu, majini nk. Ibada dua, maombi au kisomo kinachoambatana na kuchinja au kuua kiumbe chenye damu ni TAMBIKO. Masheikh walitambika na wala sio kitu kibaya. Hata manabii na mitume wa Mwenyeez Mungu walitambika kama hao unaowaita waganga wa kienyeji.
Tai...
Yawezekana hayo kwa wengine lakini katika Uislam hakuna kutambika.
 
changamoto tu ni kwamba huwezi kumaliza kuandika uzi bila kuweka neno [uislamu]. Nadhani ni vizur tu ukataja tukio husika na kuwataja walio husika inatosha mzee wangu. Hakuna ulazima wa kutanabaisha maswala ya dini zao. Hii nchi yetu sote. Wazee wetu wote waislam kwa wakristo mpaka wapagani waliipambania kwa ajili yetu sote bila kujalisha kundi lipi lina mchango mkubwa kuliko kundi jingine. Walisimama na msimamo mmoja tu. Kuipgania TANGANYIKA,
 
Mwalimu alisimulia suala la matambiko Katika kutoa shukrani zake.

Mwalimu anacheka sana.
Anacheka pale ambapo Mashehe waliotoka kumfanyia Duwa kubadilika na kuanza kufanya Matambiko mazito mazito ndani ya Muda mchache sana.

Mwalimu anaendelea kusema Alikuwa akiruka kwenye Mashimo Huko bagamoyo (Farhan Ganzel).
Ila anaonyesha kujutia sana Maamuzi yake.

Mpaji ni Mungu.
 
changamoto tu ni kwamba huwezi kumaliza kuandika uzi bila kuweka neno [uislamu]. Nadhani ni vizur tu ukataja tukio husika na kuwataja walio husika inatosha mzee wangu. Hakuna ulazima wa kutanabaisha maswala ya dini zao. Hii nchi yetu sote. Wazee wetu wote waislam kwa wakristo mpaka wapagani waliipambania kwa ajili yetu sote bila kujalisha kundi lipi lina mchango mkubwa kuliko kundi jingine. Walisimama na msimamo mmoja tu. Kuipgania TANGANYIKA,
Bahati mbaya kama Uislam unakutaabisha.

Wapo waliotutangulia walikuwa kama wewe Uislam unawapa shida.

Wakaona tabu kuandika historia wakaitaja Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika kama sehemu ya mapambano dhidi ya ukoloni.

Wakaona shida kumtaja Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir kuwa alikuwa akiuza kadi za TANU misikitini katika darsa zake.

Kwangu mimi hii ni sehemu ya historia ya jamii yangu hivyo najifaharisha na nasikia raha kuieleza.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kwani hao mashehe hawakuwepo dar mpaka mtu asafiri mpaka Baga moyo?
 
Back
Top Bottom