Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
"Nimevutiwa na hiki kipengele nimejikuta napata swali pia.
Lakini pia katika hutuba yake ya kuagana na wazee wa Dar 1985, alieleza kwa ufasaha jinsi wenyeji wa Dar (moslems in particular) walivyochangia katika harakati za uhuru.
Alikwenda mbali akaeleza mpaka baadhi ya MATAMBIKO waliyofanya wazee wa KIISLAMU akiwa peke yake wa imani tofauti.
Ninaomba kupata ufafanuzi je kuna uhusiano wa MATAMBIKO na Uislamu?
VISOMO SITA ALIVYOFANYIWA JULIUS NYERERE NA WANACHAMA WENGINE WA TANU WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA 1954 - 1961
Mtegite,
Bahati mbaya sana Mwalimu Nyerere kuna mambo yawezekana hakuwa anayajua au labda hakupenda kuyazungumza.
Kwanza ni kuwa kile kilichofanywa kwa Jumbe Tambaza si tambiko ni dua.
Mahali wanapokutana masheikh inafanyika dua na dua ziko katika Qur'an.
Hawakutani masheikh kutambika.
Dua inaweza kufuatia na kuchinja mnyama.
Mwalimu Nyerere hakuwa wa kwanza katika kufanyiwa dua ndani ya TANU.
Mwanachama wa kwanza wa TANU kufanyiwa dua alikuwa Abdul Sykes ambae mwaka wa 1954 alikutwa na kadi za TANU ndani ya ofisi yake akiwa Market Master, Soko la Kariakoo.
Kisa kirefu lakini ilihofiwa atafukuzwa kazi.
Ikafanywa dua na akachinjwa kondoo.
Mwanachama wa pili alikuwa Rashid Ali Meli.
Huyu alikuwa Bwana Fedha wa Dar es Salaam Municipal Council.
Rashid Ali Meli alitoa fedha za Municipal akampa Iddi Faiz Mafungo atie kwenye mfuko wa safari ya Nyerere UNO awahi kusafiri lakini zirudishwe haraka.
Baada ya kutoa fedha zile siku ya pili Wakaguzi wakafika ofisini kwake kumkagua.
TANU ikamfanyia dua kuomba msaada wa Allah Rashid Ali Meli anusurike.
Dua ya tatu ilifanyika ofisi ya TANU Mtaa wa Jaribu nyumbani kwa Ali Msham kuomba safari ya salama kwa Mwalimu Nyerere aliyekuwa anakwenda UNO safari ya kwanza 1955.
Mwalimu alifanyiwa dua ya nne Lindi mwaka wa 1956 na Sheikh Mohamed Yusuf Badi nyumbani kwa Suleiman Masudi Mnonji.
Dua ya tano Mwalimu alifanyiwa Mnyanjani kutafuta uelewano baina ya wana TANU katika msuguano wa Kura Tatu mwaka 1958.
Hivi ndivyo visomo vitano na ukiongeza na kile alichoeleza Mwalimu Nyerere jumla vinakuwa visomo sita.
Hapakuwa na matambiko.
Dua ofisi ya TANU Mtaa wa Jaribu Magomeni nyumbani kwa Ali Msham kuomba salama ya safari ya Mwalimu Nyerere UNO 1955.