KERO Vispika vya matangazo vimekuwa kero kubwa kwenye masoko, mamlaka ipige marufuku

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hizo ni baadhi ya laana za umasikini
Nchi zinazojielewa huwezi kusikia upumbavu huo, sio kwenye mabasi wala miziki na maspika kila kona
Hata kwenye usafiri wa Umma kwenye madirisha yameandikwa heshimu wenzio unapoongea na simu
Hapo ni simu tu kuongea unaambiwa ongea taratibu
Nyie mnafurahia kelele za miziki kwenye mabasi kama sio laana ni nini?
Hao viongozi ndio kabisa utakuta nao walitoka kwenye umasikini ndio maana wanaona labda Dunia nzima wako hivyo
 
Kariakoo mitaa wanapouza vifaa vya ujenzi na umeme angalau hakuna purukushani sana
Ila kuna mitaa wanayouza nguo za wanawake kwenye meza etc aisee hatari sana wauzaji wanaimba wanapiga makofi sijui ndio mtindo gani huo wa kufanya biashara
sasa si bora hao wanaburudisha huko kariakoo kuna watu wanatembea wanauza sigara wameshika mawe wanayagonga gonga gonga kelele zinazotoka hapo ni balaa!
 
dubai ni soko kubwa sana duniani lakini hawatumii spika kufanya biashara, tanzania huwezi kumkuta mwarabu au muhindi anafanya biashara yoyote akitumia spika hii ni sisi tu ifike wakati sasa TRA ikusanye kodi ya kila spika na sisajiliwe ziwe na namba kila mwaka unalipia na kwa mwezi elfu 15000/
 
Acha uchawi wewe..., peleka umwinyi wako huko ndegelec.
 
 

Attachments

Ni uwendawazimu mtupu, wao wanafikri hiyo ndio inawavutia wateja kumbe ni kinyume chake kabisa.
 
Sio sahihi, huko ni kuwakera na kuwafanyia vurugu wastaarabu masikini na wenye vipato vidogo.
 
Lakini pamoja na changamoto zote hizi serikali bado inaweza kuwapanga watu katika umaskini wao, mbona waliamua Wamachinga waondoke baadhi ya maeneo wakaweza,.mbona walipiga marufuku boda boda kati kati ya mji wakaweza. Hapo Karume ni kupiga marufu tu hivyo vipaza sauti kwa wote na wala hakuna mtu atakayejigusa kwa sababu kiuhalisia hata havina mchango mkubwa sana wa maana kuvutia wateja kwa hao wauzaji.

Tatizo ni kwamba serikali haitimizi wajibu wake hata katika maeneo mengine rahisi sana yasiyohitaji hata gharama kubwa za utekelezaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…